Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Ukiwa kiongozi Mkubwa na wa cheo kikubwa kama kuwa Mkuu wa Mkoa yaani Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa na kiongozi mwenye Ndoto ya kuja kuwa kiongozi Mkubwa siku za usoni .
Siyo Vyema sana kuelemewa na hisia mpaka kufikia hatua ya kulia na kutoa au kububujikwa Machozi Hadharani.Kiongozi unapaswa kuwa jasiri na Ngozi ngumu uwapo mahali popote pale penye tukio la aina yoyote ile la kugusa hisia. .Nimeona jana katika matembezi ya Amani yaliyowashirikisha viongozi mbalimbali wa Dini Mheshimiwa Makonda akizidiwa hisia Mpaka kufikia hatua ya kutoa Machozi japo hii siyo mara ya kwanza.maama nakumbuka pia akiwa kanisani na akiwa RC wa Dar es salaam napo imewahi kutokea hivyo.
Kiongozi unatakiwa udhibiti hisia zako na kuwa imara muda na wakati wote.Embu fikiria labda wewe ndio Amiri Jeshi Mkuu halafu kukatokea vita kama ile ya Tanzania na uganda .halafu ukaletewa taarifa mbaya ya vifo vya askari wako au kurudishwa nyuma kwa vikosi vya jeshi lako.
Sasa badala ya kujibu kwa ujasiri na kwa kauli za kishujaa na kuwatia moyo Makamanda walioleta taarifa kwa kuwaambia kuwa ni lazima tushinde vita hii kwa gharama yoyote ile kulinda ardhi yetu na kupigana kwa ajili ya askari na mashujaa wetu waliopoteza maisha. na kwamba Damu zao zilizomwagika zinakwenda kuleta ushindi na kuwa wamekufa kimwili lakini kiroho bado tupo nao na tunaendelea pale walipoishia wao.
na kwamba wewe kama Amiri Jeshi Mkuu umeshaongea na Nchi marafiki na wapo tayari kusaidia kutoa silaha nzito nzito za kisasa kabisa na ndege nzuri kabisa ambazo nyingine siyo za kutumia rubani na kwamba mambo mbalimbali ya kiteknolojia unakwenda kuwawezesha askari wako wa vikosi vyote ikiwepo teknolojia ya kudungua ndege za adui,Vifaru vya kisasa vipo njiani vinakuja na pia kuongeza askari katika uwanja wa mapambano.
Sasa badala ya kuwapa moyo na kuwaambia maneno hayo yenye kuwaongezea ujasiri na nguvu za kuendelea kupambana na morali kwa askari wote .wakute wewe umeanza kulia na kububujikwa na machozi yasiyokatika.unafikiri watajisikiaje? unafikiri watakuchukuliaje?unafikiri utakuwa umewavunja Moyo kiasi gani? Unafikiri utakuwa umewakatisha tamaa na kushusha morali ya kupigana kwa kiasi gani?
Unajua kiongozi ni pamoja na kuwapa morali unaowaongoza,kuwajaza ujasiri ,kuwaonyesha kuwa ushindi ni lazima upatikane hata kama mazingira ni mabaya na magumu. lakini ni lazima kila mmoja ajitoe kwa jasho na Damu kutetea Ardhi yetu na Taifa letu au jambo fulani.
Ndio maana ya kuitwa kiongozi .kwamba wewe ni lazima uwaongoze njia watu tena njia ya ushindi na matumaini.ni lazima uwajaze ujasiri na matumaini hai hata kama moyoni una maumivu lakini usoni ni lazma uonyeshe ujasiri na utayari wa mapambano.wewe ndiye unatakiwa uwafute machozi na kuwashika mkono walio nyuma yako badala ya wao ndio waanze kutafuta vitambaa vya kukufutia machozi.
Embu angalia namna Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Samia baada ya Kifo cha Rais wetu wa Awamu ya Tano Hayati Daktari Mwalimu John Pombe Joseph Magufuli kufariki Dunia.mliona namna alivyo tujaza ujasiri watanzania? Mliona namna alivyotoa kauli za kiuongozi na kuleta matumaini.mnakumbuka Kauli yake ya kuwa huu sio wakati wa kuangalia mbele kwa mashaka bali wa kuangalia na kutizama mbele kwa Matumaini.
mnakumbuka pia kauli yake ya kuwa kazi iendelee? Unafikiri kwanini alitamka maneno hayo? Vipi kama angeanza kububujikwa na machozi muda wote? Mnafikiri Watanzania wangekuwa katika hali gani? Si wote tungekata tamaa?
Mnakumbuka alipokwenda kuwapa pole watu wa Hanang mkoani Manyara waliofariki kwa kusombwa na udongo ulioporomoka kutoka mlimani? Mnakumbuka kauli zake za kijasiri kama kiongozi alizozitoa licha ya kuwa na majonzi mazito Moyoni na kifuani pake?unafikiri ni kwanini hakububujikwa na machozi? Je mliona na kukumbuka wakati hayati Benjamini Mkapa anatangaza kifo cha Muasisi wa Taifa letu Hayati Mwalimu Nyerere mwaka 1999 October?
Vipi wakati Mama yetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia wakati anatangaza kifo cha Hayati Mwalimu Daktari John Magufuli mkoani Tanga? Je mliona sura yake ilivyokuwa na namna alivyojikaza kijasiri? Unafikiri kwanini hakulia hadharani? Jibu ni kwa sababu ni kiongozi na anafahamu dhamana kubwa aliyonayo katika kulifariji Taifa na kulipa Matumaini.
Ukiwa kiongozi kuna namna ya kujiweka .ndio Maana ni muhimu sana kwa kiongozi kutofautisha wewe kama mtu binafsi na husia zako na kiongozi mwenye watu nyuma yako.
Ok naomba niweke kalamu yangu chini mara moja.nitatoa semina wakati mwingine ya uongozi hapa jukwaani kwa vitu vya msingi kwa kiongozi kuvijua na kuviishi. Lakini kwa ufupi ni kuwa viongozi wanatakiwa wamchukulie na kumuiga Rais Samia kama Darasa lao.maana nikimuangalia Rais Samia naona ni chuo cha uongozi kitembeacho.na ndio maana namfuatilia kila siku awapo hadharani na yale afanyayo na kuzungumza .
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.