Namshauri Ummy Mwalimu Waziri wa Afya kutengua Kauli ya kuruhusu Clinic binafsi katika hospitali za umma

Waziri Ummy Mwalimu ameruhusu madaktari wa serikali kutumia hospitali za umma kama private clinics baada ya saa za kazi. Jambo hili lina ukakasi lakini ndiyo hivyo tena sisi wananchi hatuna namna bali kukubali kwa kuwa hoja ikisha kubaliwa na kupitishwa na CCM ndiyo maamuzi ya mwisho.

Sasa kwa kutumia busara hizo hizo za CCM basi uamuzi huo usiishie kwa madaktari tu bali pia watumishi wote wa serikali waruhusiwe kutumia mali na ofisi za umma kwa shughuli zao binafsi. Waalimu wafanye tuition mashuleni baada ya muda wa kazi, wahandisi, madereva, wahasibu nk.

Serikali isifanye ubaguzi wala upendeleo katika hoja hii. Wananchi wote wanalipa kodi hivyo wana haki ya kutumia rasilimali za umma kwa usawa. Ikiwezekana shughuli zote za umma zibinafsishwe kwa sababu serikali imeshindwa kuzisimamia.
Mi ndio sijamwelewa kabisa huyu mwanamama, km amechoka na uwaziri si akapishe wengine. Unawezaje kutumia vitendea kazi vya serikali kwa shughuli binafsi. Hawa hawana hata washauri? Tusubiri vituko huko mahospitalini. Hata kwa busara ya kawaida huwezi kutoa tamko km hilo, huwezi kuhudumia mabwana wawili kwa wakati moja. Eti wagawane mapato, nani anacontrol hayo mapato. Jambo la hovyo kwangu mimi.
 
Ummy akumbuke kuwa madaktari na manesi wanafanya kazi kwa shift! Wale wa shift ya usiku asubuhi wao siyo muda wa kazi, kwa uamuzi wake wa kijinga hao wa naweza kuendelea na kazi na hivyo kuleta mgongano. Kwamba wengine watafanya kazi kama muda wao wa kazi na wengine watafanya kama wako katika private clinics!

Serikali imethibitisha bila chenga kuwa imeshindwa kusimamia watumishi wake na rasilimali za umma!
 
Nawasalimu wote humu jukwaani

Ama kweli miluzi mingi humpoteza mbwa, niende moja kwa moja kwenye hoja

Mh waziri wa Afya baada ya kurudishwa kwenye wizara hii ya Afya na Mheshimiwa Rais alipoingia madarakani mwaka 2021, amekua ni mtu wa matamko hata ambayo si saizi yake, yanayomshushia hadhi

Nitaanza na maamuzi yake kadhaa na baadhi ya matamko kupitia wizara ya afya halafu tuulizane huyu Waziri anatosha kweli

1. Mheshimiwa Waziri mnamo mwaka 2021 alikuja na tamko kua maduka yote ya dawa(pharmacies) yaliyo karibu na hospitali za umma kwa umbali fulani waliopendekeza yaondolewe kwakua yamekua yakisababisha hospitali nyingi za umma kutokuleta dawa hospitalini

Sasa kuna maswali kadhaa hapa, wakati yanasajiliwa sheria ilikua inasemaje au kila anaepata cheo anakuja na sheria zake bila kujali kua nchi ilikua ikiendelea hata bila uwepo wake.

baadae akaishia hewani mpaka leo haieleweki nini kinaendelea ni kwa sababu tu aliona alichokifanya si sahihi, kwa sababu kama lengo ni kupunguza maduka ya dawa karibu na hospitali za umma sheria ilitakiwa ianze na maduka yanayofunguliwa siyo yaliyokuwepo kwa sababu sheria ya awali iliyaruhusu kuwepo.

Imagine mikoa midogo kama Daresalaam ambayo kila centre ni mji na unahitaji huduma zake, mtu alifungua duka eneo la katikati ya mji husika, leo hii unamwambia atoe duka aende mbali mita 300m kwa sheria ipi, mfano yale maduka ya Mwananyamala hosp, Muhimbili hosp n.k yaende wapi, ruhusu watu wahuishe vibali vyao mheshimiwa, sheria imewakuta,Muungwana akikosea huchutama

2. Suala la Doctors kuanzisha private clinics kwenye hospitali za umma,

Yaani kuna wakati ukisikia kitu kinatamkwa na kiongozi anaetegemewa na taifa mpaka utumbo unaunguruma kwa hofu, unajiuliza huyu hakuwaza kabla ya tamko hili, au ndo ukishakua mtu wa vyombo vya habari kila muda unataka kuonekana tu

Muda wa dakitari kutoka kazini kwa muda wa serikali na kama hana emergency yoyote ni saa tisa na nusu alasiri na wakati mwingine huondoka na kuwaahidi wagonjwa ambao hawakubahatika kuonwa kwamba angewaona kesho yake.

sasa iweje serikali inayotoa huduma(services) na si biashara ianze kuruhusu watu kufanya biashara kwenye taasisi za umma..?

Wagonjwa wangapi wameshindwa kwenda hospitali za private sababu ya gharama wakakimbilia serikali halafu wanafika huko wanakuta nao wameanzisha vitengo vya private ambavyo unalipia gharama alizojipangia mtoa huduma, Let's say mm ni dakitari, sasa kuliko nipambane kuwahudumia wagonjwa wangu ishirini niwamalize waende nyumbani si bora ni delay niwaone hata watano halafu hao 15 waliobaki nivute vute ifike muda wangu wa kutoka niwaweke private nipige hela, kusema ukweli inachochea hata uzembe makazini na kutengeneza mianya ya Rushwa, mbona Fast Track ilikua inatosha tu,

kwanini nchi yetu hii aliyeshiba hua hamkumbuki mwenye njaa

3. Matamko mara wafamasia kupewa mitaji sijui ya biashara(hypothetical), wataalamu wa maabara sijui kufanywaje yaan shaghala bhagala

Mara mtu kaosha vifaa vya theater kwa mikono anasimama waziri ndiye anayetoa tamko,
Mara mgonjwa na mpenzi wake wanakiss wodini waziri ndiye anayetoa tamko (cheap politics)
Na mengine mengi sana

Mbona mambo ya ushoga na Mashoga mlikaa kimya au yenyewe hayana madhara kiafya..?

Hebu tuboreshe Afya ya jamii na taifa kwa ujumla bila kutafuta faida za kisiasa (political mileages) kwa kukesha kwenye vyombo vya habari

Mbona NEMC ilifungia mabaa na kumbi za starehe sikumsikia Jaffo akiitisha waandishi wa habari, suala walilimaliza wao wenyewe, Fanyeni delegation of power, hata usipokuwepo mambo yaende, tusijimilikishe nafasi za Umma.

Ni hayo tu
 
Ushoga hakuna tamko, ya bandari midomo mizito, nakazia Uzi wako.
JamiiForums1709643988.jpg
 
Waziri Ummy ni mjanja, lengo lake ni kuhamisha mjadala wa wawekezaji wa DP World kwenye bandari zetu zote. Anataka sasa tujadili huu uwekezaji mpya wa madaktari wetu wazalendo kwenye hospitali na zahanati zetu zote nchini.

Ni uwekezaji mzuri wa kuleta ufanisi kwenye hospitali na zahanati zetu. Unapaswa kuigwa hata huko kwenye bandari zetu. Wafanyakazi wetu wa bandari waruhusiwe kufanya kazi hizo wakati wa private times zao na tukagawana mapato yatakayopatikana. Uamuzi huu hauhitaji kupata ridhaa ya bunge letu. Shule zetu za serikali ambazo nazo ufanisi wake si mzuri, zinaweza kuiga uwekezaji huu kwa walimu wake etc.
 
Waziri Ummy Mwalimu ameruhusu madaktari wa serikali kutumia hospitali za umma kama private clinics baada ya saa za kazi. Jambo hili lina ukakasi lakini ndiyo hivyo tena sisi wananchi hatuna namna bali kukubali kwa kuwa hoja ikisha kubaliwa na kupitishwa na CCM ndiyo maamuzi ya mwisho.

Sasa kwa kutumia busara hizo hizo za CCM basi uamuzi huo usiishie kwa madaktari tu bali pia watumishi wote wa serikali waruhusiwe kutumia mali na ofisi za umma kwa shughuli zao binafsi. Waalimu wafanye tuition mashuleni baada ya muda wa kazi, wahandisi, madereva, wahasibu nk.

Serikali isifanye ubaguzi wala upendeleo katika hoja hii. Wananchi wote wanalipa kodi hivyo wana haki ya kutumia rasilimali za umma kwa usawa. Ikiwezekana shughuli zote za umma zibinafsishwe kwa sababu serikali imeshindwa kuzisimamia.
Sijaamini alichokisema waziri!
 
Serikali imeshindwa kabisa kuendesha na kusimamia shughuli za afya kama ilivyo kwenye bandari.

Uamuzi uliotolewa na Waziri Ummy Mwalimu utakuja kuleta mgogoro wa kimaslahi kati ya Serikali na madaktari.

Suluhisho. Serikali iingie ubia na wafanyakazi wote wa sekta ya afya, sio madaktari pekee, kwenye huo ubia Serikali imiliki asilimia 40, wafanyakazi wote wamilikishwe asilimia 20 ... asilimia 40 inayobaki watafutwe wawekezaji kwenye soko la hisa.
 
Ummy akumbuke kuwa madaktari na manesi wanafanya kazi kwa shift! Wale wa shift ya usiku asubuhi wao siyo muda wa kazi, kwa uamuzi wake wa kijinga hao wa naweza kuendelea na kazi na hivyo kuleta mgongano. Kwamba wengine watafanya kazi kama muda wao wa kazi na wengine watafanya kama wako katika private clinics!

Serikali imethibitisha bila chenga kuwa imeshindwa kusimamia watumishi wake na rasilimali za umma!
Hii nchi kuna siku wataikodisha serikali kwa private groups.
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]Wameanza na bandari kwanzaa kupima upepoo.. sasa Waziri anataka madaktari wawe na ofisi zao ndani ya majengo ya serikali..
 
Nipo na Coaster STL ngoja niende Chanika Gmboto nikalambe abiria kwenda Chanika 2 kwa 4 sikosi 50,000/- mafuta ya Serikali mama kasema kila mtu ale usawa wa kamba yake
 
Waziri Ummy ni mjanja, lengo lake ni kuhamisha mjadala wa wawekezaji wa DP World kwenye bandari zetu zote. Anataka sasa tujadili huu uwekezaji mpya wa madaktari wetu wazalendo kwenye hospitali na zahanati zetu zote nchini.

Ni uwekezaji mzuri wa kuleta ufanisi kwenye hospitali na zahanati zetu. Unapaswa kuigwa hata huko kwenye bandari zetu. Wafanyakazi wetu wa bandari waruhusiwe kufanya kazi hizo wakati wa private times zao na tukagawana mapato yatakayopatikana. Uamuzi huu hauhitaji kupata ridhaa ya bunge letu. Shule zetu za serikali ambazo nazo ufanisi wake si mzuri, zinaweza kuiga uwekezaji huu kwa walimu wake etc.
Sahihi. Siyo kwamba ni mjanja, ameelekezwa kuja kutangaza kitu cha ajabu kama hiki almradi kuhamisha mjadala Wa watanzania juu ya DPw kwenye social media mbalimbali.
Huu mjadala wa Bandari hauhami kwa utoto kama huu.
 
Waziri Ummy Mwalimu ameruhusu madaktari wa serikali kutumia hospitali za umma kama private clinics baada ya saa za kazi. Jambo hili lina ukakasi lakini ndiyo hivyo tena sisi wananchi hatuna namna bali kukubali kwa kuwa hoja ikisha kubaliwa na kupitishwa na CCM ndiyo maamuzi ya mwisho.

Sasa kwa kutumia busara hizo hizo za CCM basi uamuzi huo usiishie kwa madaktari tu bali pia watumishi wote wa serikali waruhusiwe kutumia mali na ofisi za umma kwa shughuli zao binafsi. Waalimu wafanye tuition mashuleni baada ya muda wa kazi, wahandisi, madereva, wahasibu nk.

Serikali isifanye ubaguzi wala upendeleo katika hoja hii. Wananchi wote wanalipa kodi hivyo wana haki ya kutumia rasilimali za umma kwa usawa. Ikiwezekana shughuli zote za umma zibinafsishwe kwa sababu serikali imeshindwa kuzisimamia.

Maajabu ….haya
 
Nadhani kauli ya waziri ni ngumu kuielewaa kama hujui namna utaratibu unafanya kaziii ilaa Jambo linaloelewekaa[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom