Nawasalimu wote humu jukwaani
Ama kweli miluzi mingi humpoteza mbwa, niende moja kwa moja kwenye hoja
Mh waziri wa Afya baada ya kurudishwa kwenye wizara hii ya Afya na Mheshimiwa Rais alipoingia madarakani mwaka 2021, amekua ni mtu wa matamko hata ambayo si saizi yake, yanayomshushia hadhi
Nitaanza na maamuzi yake kadhaa na baadhi ya matamko kupitia wizara ya afya halafu tuulizane huyu Waziri anatosha kweli
1. Mheshimiwa Waziri mnamo mwaka 2021 alikuja na tamko kua maduka yote ya dawa(pharmacies) yaliyo karibu na hospitali za umma kwa umbali fulani waliopendekeza yaondolewe kwakua yamekua yakisababisha hospitali nyingi za umma kutokuleta dawa hospitalini
Sasa kuna maswali kadhaa hapa, wakati yanasajiliwa sheria ilikua inasemaje au kila anaepata cheo anakuja na sheria zake bila kujali kua nchi ilikua ikiendelea hata bila uwepo wake.
baadae akaishia hewani mpaka leo haieleweki nini kinaendelea ni kwa sababu tu aliona alichokifanya si sahihi, kwa sababu kama lengo ni kupunguza maduka ya dawa karibu na hospitali za umma sheria ilitakiwa ianze na maduka yanayofunguliwa siyo yaliyokuwepo kwa sababu sheria ya awali iliyaruhusu kuwepo.
Imagine mikoa midogo kama Daresalaam ambayo kila centre ni mji na unahitaji huduma zake, mtu alifungua duka eneo la katikati ya mji husika, leo hii unamwambia atoe duka aende mbali mita 300m kwa sheria ipi, mfano yale maduka ya Mwananyamala hosp, Muhimbili hosp n.k yaende wapi, ruhusu watu wahuishe vibali vyao mheshimiwa, sheria imewakuta,Muungwana akikosea huchutama
2. Suala la Doctors kuanzisha private clinics kwenye hospitali za umma,
Yaani kuna wakati ukisikia kitu kinatamkwa na kiongozi anaetegemewa na taifa mpaka utumbo unaunguruma kwa hofu, unajiuliza huyu hakuwaza kabla ya tamko hili, au ndo ukishakua mtu wa vyombo vya habari kila muda unataka kuonekana tu
Muda wa dakitari kutoka kazini kwa muda wa serikali na kama hana emergency yoyote ni saa tisa na nusu alasiri na wakati mwingine huondoka na kuwaahidi wagonjwa ambao hawakubahatika kuonwa kwamba angewaona kesho yake.
sasa iweje serikali inayotoa huduma(services) na si biashara ianze kuruhusu watu kufanya biashara kwenye taasisi za umma..?
Wagonjwa wangapi wameshindwa kwenda hospitali za private sababu ya gharama wakakimbilia serikali halafu wanafika huko wanakuta nao wameanzisha vitengo vya private ambavyo unalipia gharama alizojipangia mtoa huduma, Let's say mm ni dakitari, sasa kuliko nipambane kuwahudumia wagonjwa wangu ishirini niwamalize waende nyumbani si bora ni delay niwaone hata watano halafu hao 15 waliobaki nivute vute ifike muda wangu wa kutoka niwaweke private nipige hela, kusema ukweli inachochea hata uzembe makazini na kutengeneza mianya ya Rushwa, mbona Fast Track ilikua inatosha tu,
kwanini nchi yetu hii aliyeshiba hua hamkumbuki mwenye njaa
3. Matamko mara wafamasia kupewa mitaji sijui ya biashara(hypothetical), wataalamu wa maabara sijui kufanywaje yaan shaghala bhagala
Mara mtu kaosha vifaa vya theater kwa mikono anasimama waziri ndiye anayetoa tamko,
Mara mgonjwa na mpenzi wake wanakiss wodini waziri ndiye anayetoa tamko (cheap politics)
Na mengine mengi sana
Mbona mambo ya ushoga na Mashoga mlikaa kimya au yenyewe hayana madhara kiafya..?
Hebu tuboreshe Afya ya jamii na taifa kwa ujumla bila kutafuta faida za kisiasa (political mileages) kwa kukesha kwenye vyombo vya habari
Mbona NEMC ilifungia mabaa na kumbi za starehe sikumsikia Jaffo akiitisha waandishi wa habari, suala walilimaliza wao wenyewe, Fanyeni delegation of power, hata usipokuwepo mambo yaende, tusijimilikishe nafasi za Umma.
Ni hayo tu