Namtafuta Mama Yangu popote alipo

Namtafuta Mama Yangu popote alipo

Huu uzi unataka kufanana na na wa holoholo unaitwa "Nakuchukia Baba Yangu" sijui hili taifa limelaaniwa na nani jamani badala ya vijana wamshukuru mungu wao wanawachukia wazazi wao pumbavu na mimi holoholo nikiwemo
 
Acha kudeka,kuna wamama ni wakakx mbaka unaweza kudhani sio mama yako.
 
Anaongea kinyume chake ila unajua kutokanana anachokiongea anamaanisha kabisa wewe sio mwanangu na Mimi sio Mama yako sometimes anakwambia nenda kamtafute Mama yako alipo, kuna treatment ya Mama kwenda kwa mtoto na kuna kipindi niliwahi kumhoji Mzee kwani Mimi Mama yangu yupo wapi? Hakuwahi kunipa jibu linaloeleweka sababu nilishagundua huyu sio Mama yangu
Maskini.pole sana .huenda ni mamako kabisa ila hasira zinamzid nguvu
 
Kuna mtu anatafutwa kwa hiyo staili yako?
Hakuna. Kuna taarifa nyingi sana bado inatakiwa ili tuweze kumsaidia katika kumtafuta mama yake halisi. Kwa hayo aliyoyaandika ni kama taarifa tu kwamba anamtafuta mama yake kwa vile haridhiki na huyu anayeishi naye.
 
Unasema sio mama yako kisa hana tabia kama zako??

Hiyo ni kawaida na kuna tabia zipo zaidi kwa wanawake na sio wanaume. Inabidi uelewe kua mama yako ni mwanamke na sio mwanaume kama wewe na baba yako..

Wazazi huwa wanazingua sana sometimes ila haiondoi tittle yao ya kua ni wazazi. Mapito yao na yako ni tofauti, si ajabu elimu yako na yao ni tofauti, jinsi wewe unachukulia mambo na wao ni tofauti.

Wewe ni mkimya mama ni muongeaji hapo pia kuna utofauti .
Nimekuelewa mkuu lakini sababu zinazopelekea kuamini kua huyu sio Mama yangu ni nyingi mno nyingi sana laiti km ungekua upande wangu ungelitambua hilo
 
Sawa kaka Ila kama unahisi si mama yako kwa ajili ya vitendo vyake unaweza kukosea kwa sababu kila mama ana tabia zake za kibinadamu Ila kama unahisi si mama yako kutokana na viashiria flani solid. Then waulize wakubwa wa ukoo wako, lazma wanajua

Japo kila geti ambalo limefungwa mbele yako kwa muda mrefu bhasi ujue kuna gharama utailipia kulifungua. Na kikubwa zaidi, usisahau wema wa huyo mama hata kama ni mdogo kwa kiasi gani
Mema hayakosekani mkuu ila mabaya yanapozidi mema hakuna mema tena, suala la kuuliza nimewahi kumuuliza Mzee akanipa jibu la mkato tu still bado nimebakia kuona huyu sio Mama yangu
 
Bro nakuheshimu sana na naheshimu mawazo yako na mtazamo wako uwe hasi au uwe chanya, ila tu usinishutumu kwa vitu nisivyovifanya halafu Mimi sio Mtoto tena nimekua mtu mzima sasa ila nilichoandika hapa ukielewe km kuna Mama aliwahi kumtelekeza mwanae sehemu na yupo anaishi ajue mwanae yupo hai na ameshagundua Mama aliehisi ni Mama yake miaka yote zaidi ya 30 sio Mama yake
Kwa hiyo unamtafuta mama ambaye hajawahi kukutafuta? What is the point? Kama hajakutafuta ina maana hana haja na wewe.
 
Mema hayakosekani mkuu ila mabaya yanapozidi mema hakuna mema tena, suala la kuuliza nimewahi kumuuliza Mzee akanipa jibu la mkato tu still bado nimebakia kuona huyu sio Mama yangu
Tafuta ukweli lakini kumbuka usisahau wema hata kama ni mdogo. Kama hukukudhuru na akachangia hata kidogo kukuza, inakupasa umshukuru hata kama kwako hana thamani
 
Back
Top Bottom