Namtafuta mwanadada anaitwa Neema, wa pale Moshi

Namtafuta mwanadada anaitwa Neema, wa pale Moshi

Huyu mwanadada tulikutana naye mwaka 2007, nikiwa naishi old moshi, na yeye akiishi kwao mtaa wa rau Moshi.

Tulikuwa na mahusiano, kipindi hicho na nilitegemea awe ubavu wangu wa kushoto, ila kutokana na kupotezana, ilishindikana.

Alisoma, majengo sekondari Moshi; mrefu wa wastani na ulikuwa mweupe, pia tulikuwa tukionana pale tulipokuwa tukienda kwenye ibada, kanisa la kristu mfalme.

Hitaji langu kwa sasa, nikuone tu na niweze kukusalimia.

Popote ulipo, naomba ujitokeze.​
Sema na Mimi vizuri aiseee huyu mtu kwa Sasa yupo Dar ya Salaam, alipata olewa ila ndio hivyo Tena ndoa ndoano...
Nitafute nikilink nae, uweze msalimia tu.
 
Namtafuta Muna Abdillah mtoto wa kisomali......nilikuwa nasoma nae madrasa pale Ustadhi Rama...kasulu mjini....natamani kupata Mawasiliano yake,katika watu ambao wameishi kichwani mpaka leo ni huyu....
Sijui yuko wapi KWA sasa,alikuwa akiniletea sambuza,kastam,maandazi n.k maana kwao walikuwa na Hotel...huyu mtu hanitoki kichwani zaidi ya miaka 18 sasa...kila nikikaa huwa namkumbuka.....yuko wapi Muna?
 
Alishapata mwingine na mwinginee na mwingineeee ...na mwingineeeee ...na mwingineee na mwingine... na wewe utakuwa mwingine kwa mara nyingine
 
Sema na Mimi vizuri aiseee huyu mtu kwa Sasa yupo Dar ya Salaam, alipata olewa ila ndio hivyo Tena ndoa ndoano...
Nitafute nikilink nae, uweze msalimia tu.
Utatumia njia gani kumpata?
 
Back
Top Bottom