Namtumbo: Wazazi waacha kupeleka Watoto Shuleni wakiaminishwa Yesu Kristo anakaribia kurudi

Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Ngollo Malenya amefanya msako wa Wanafunzi ambao hawajaripoti Shule za Msingi na Sekondari Vijijini ambapo katika hali isiyo ya kawaida alipofika Kijiji cha Chengena kwenye msako wa nyumba kwa nyumba amebaini uwepo wa Mtumishi wa Mungu Erick Manyanya (33) Mwinjilisti wa Kanisa la Country Living ambaye amefungua Kanisa Kijijini hapo akiwahubira Wazazi wasiwapeleke Watoto Shule kwakuwa Yesu Kristo atarudi muda sio mrefu kuchukua kondoo wake hivyo badala ya kwenda Shule wajiandae kumpokea Yesu.

Erick ni Kijana ambaye alikuwa anasoma Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambaye anadai baada ya kusoma vitabu na kuijua imani yake vizuri akaacha Chuo na kwenda kuanzisha Kanisa hilo Namtumbo “Nimesoma UDOM sikuhitimu elimu yangu sababu ni baada ya kuijua imani yangu vizuri katika vitabu, maana tumeambiwa Mtu hatoishi kwa mkate tu bali kwa kila neno linalotoka katika kinywa cha Mungu, mpaka nafika Chuo Kikuu nipo katika mikono ya Wazazi baada ya kujitambua Mimi nachagua njia yangu inayonipa furaha, nyakati zinazokuja chap- ya mnyama itasurutishwa, kitabu cha ufunuo wa Yohana kuna namba 666 sasa huo wakati upo karibu yetu”

DC Ngollo amesema Erick amefanikiwa kuwarubuni Wazazi mbalimbali ambao ni wa dhehebu la Wasabato Kijijini hapo na wameachisha Watoto wao Shule ili wajiandae kumpokea Yesu ambapo hadi sasa Watoto 13 tayari wameacha kwenda Shule na wameaminishwa kuwa elimu ya Mungu haipaswi kuchangamana na Elimu Dunia inayotolewa na Shule za Serikali na binafsi.

DC Ngollo akiwa na Kamati ya Usalama wa Wilaya ameagiza kukamatwa kwa Mwinjilisiti Erick na Mwinjilisti mwenzake anayemsaidia kazi za Kanisa Anthony Mkomela kwa mahojiano zaidi.

Pia soma

Hii itakuwa ipo maeneo mengi mikoani,inatakiwa kuwa na ufuatiliaji.
 
Kuna changamoto mkuu bora serikali iingilie kati tena ningefurahi raisi akiwa mkiristo ndipo akataze haya maujinga maana now mama wa watu akisema neno basi utaskia udini wakati watu wanapotosha jamii
Hatari sana
Waafrika tunalaana. Mtu ata akiambiwa na kiongozi wake wa dini kuwa ampe mkewe akalale nae ili ampe mimba itakayosaidia kuzaa mtoto mwenye nguvu za kupambana na shetani au wachawi, atakubali.
Hatari sana.
 
Huyo kijana, inabidi akamatwe, apelekwe kwenye kambi ya jeshi, atiwe mijeredi mpaka akili ikae sawa, huu ujinga wa kikristo, unaleta madhara Sana, haiwezekani nchi ikawa na vikanisa viiiingi kila eneo,
Ni watu tu,wanaotafuta umaarufu kwa nguvu.
 
Baba pipa mama mfuniko mtoto maji.
Yesu kama Yesu anakuja hivi karibuni😁
Hapo Kenya yupo,anayesema yeye ndio Yesu,ni mwafrika mwenzetu,watu hawamuamini,mpaka aje mweupe labda,ndio watamuamini,na amefikishwa mahakamani,akajitetea kama yeye sio Yesu,basi aletwe huyo Yesu.Watu waache tabia za kumrajq vibaya Yesu/Nabii Issa.Waislamu na wakristo wote wanaamini,atarudi tena mwisho wa dunia.
 
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Ngollo Malenya amefanya msako wa Wanafunzi ambao hawajaripoti Shule za Msingi na Sekondari Vijijini ambapo katika hali isiyo ya kawaida alipofika Kijiji cha Chengena kwenye msako wa nyumba kwa nyumba amebaini uwepo wa Mtumishi wa Mungu Erick Manyanya (33) Mwinjilisti wa Kanisa la Country Living ambaye amefungua Kanisa Kijijini hapo akiwahubira Wazazi wasiwapeleke Watoto Shule kwakuwa Yesu Kristo atarudi muda sio mrefu kuchukua kondoo wake hivyo badala ya kwenda Shule wajiandae kumpokea Yesu.

Erick ni Kijana ambaye alikuwa anasoma Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambaye anadai baada ya kusoma vitabu na kuijua imani yake vizuri akaacha Chuo na kwenda kuanzisha Kanisa hilo Namtumbo “Nimesoma UDOM sikuhitimu elimu yangu sababu ni baada ya kuijua imani yangu vizuri katika vitabu, maana tumeambiwa Mtu hatoishi kwa mkate tu bali kwa kila neno linalotoka katika kinywa cha Mungu, mpaka nafika Chuo Kikuu nipo katika mikono ya Wazazi baada ya kujitambua Mimi nachagua njia yangu inayonipa furaha, nyakati zinazokuja chap- ya mnyama itasurutishwa, kitabu cha ufunuo wa Yohana kuna namba 666 sasa huo wakati upo karibu yetu”

DC Ngollo amesema Erick amefanikiwa kuwarubuni Wazazi mbalimbali ambao ni wa dhehebu la Wasabato Kijijini hapo na wameachisha Watoto wao Shule ili wajiandae kumpokea Yesu ambapo hadi sasa Watoto 13 tayari wameacha kwenda Shule na wameaminishwa kuwa elimu ya Mungu haipaswi kuchangamana na Elimu Dunia inayotolewa na Shule za Serikali na binafsi.

DC Ngollo akiwa na Kamati ya Usalama wa Wilaya ameagiza kukamatwa kwa Mwinjilisiti Erick na Mwinjilisti mwenzake anayemsaidia kazi za Kanisa Anthony Mkomela kwa mahojiano zaidi.

Pia soma

Huyu yeye kasoma mpaka chuo kikuu,lakini wenzake hataki wasome.Na wapo pia wachungaji wasiotaka wagonjwa kupelekwa hospital kwenye matibabu,kama ni maradhi ya kuambukiza ni hatari,yanaweza kusambaa kwa waumini wengine.
 
Hapo Kenya yupo,anayesema yeye ndio Yesu,ni mwafrika mwenzetu,watu hawamuamini,mpaka aje mweupe labda,ndio watamuamini,na amefikishwa mahakamani,akajitetea kama yeye sio Yesu,basi aletwe huyo Yesu.Watu waache tabia za kumrajq vibaya Yesu/Nabii Issa.Waislamu na wakristo wote wanaamini,atarudi tena mwisho wa dunia.
Daaah Kenya hawajawah kua serious kabisa🤣
 
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Ngollo Malenya amefanya msako wa Wanafunzi ambao hawajaripoti Shule za Msingi na Sekondari Vijijini ambapo katika hali isiyo ya kawaida alipofika Kijiji cha Chengena kwenye msako wa nyumba kwa nyumba amebaini uwepo wa Mtumishi wa Mungu Erick Manyanya (33) Mwinjilisti wa Kanisa la Country Living ambaye amefungua Kanisa Kijijini hapo akiwahubira Wazazi wasiwapeleke Watoto Shule kwakuwa Yesu Kristo atarudi muda sio mrefu kuchukua kondoo wake hivyo badala ya kwenda Shule wajiandae kumpokea Yesu.

Erick ni Kijana ambaye alikuwa anasoma Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambaye anadai baada ya kusoma vitabu na kuijua imani yake vizuri akaacha Chuo na kwenda kuanzisha Kanisa hilo Namtumbo “Nimesoma UDOM sikuhitimu elimu yangu sababu ni baada ya kuijua imani yangu vizuri katika vitabu, maana tumeambiwa Mtu hatoishi kwa mkate tu bali kwa kila neno linalotoka katika kinywa cha Mungu, mpaka nafika Chuo Kikuu nipo katika mikono ya Wazazi baada ya kujitambua Mimi nachagua njia yangu inayonipa furaha, nyakati zinazokuja chap- ya mnyama itasurutishwa, kitabu cha ufunuo wa Yohana kuna namba 666 sasa huo wakati upo karibu yetu”

DC Ngollo amesema Erick amefanikiwa kuwarubuni Wazazi mbalimbali ambao ni wa dhehebu la Wasabato Kijijini hapo na wameachisha Watoto wao Shule ili wajiandae kumpokea Yesu ambapo hadi sasa Watoto 13 tayari wameacha kwenda Shule na wameaminishwa kuwa elimu ya Mungu haipaswi kuchangamana na Elimu Dunia inayotolewa na Shule za Serikali na binafsi.

DC Ngollo akiwa na Kamati ya Usalama wa Wilaya ameagiza kukamatwa kwa Mwinjilisiti Erick na Mwinjilisti mwenzake anayemsaidia kazi za Kanisa Anthony Mkomela kwa mahojiano zaidi.

Pia soma

Afya ya akili.
Hapo Chengena nimeishi wakati tunajenga barabara ya lami.
Kuna komoni nzuri sana na nyama ya ndovu.
 
Back
Top Bottom