Namuogopa mpenzi wangu nikisikia sauti yake

Namuogopa mpenzi wangu nikisikia sauti yake

Sasa mwanamke ulitaka uwe na kibesi kwa mwanaume wako ugundue Nini? Kwahiyo kuwa mnyenyekevu unaona kama umelogwa? Huo ndio umwanamke na inaonyesha unampenda kwahiyo ukae kwa kutulia
Sipendi hali ya kuwa bubu ilhal nina nyongo moyoni nataka kuzitoa
 
Umenikumbusha na wa kwangu tukiwa tunachat nikimkera anakuaga mkali kwenye sms ila nikimpigia simu au tukiwa live tuyamalize maneno yote yanamuisha Yani anakuwa siyo yule wa kwenye sms.....hii inafanya hata ugomvi uwe mkubwa vipi ,na solve kwa muda mfupi
 
Jipe muda.
Labda msi ishi pamoja.

Tena huyo unayemzidi kipato?
Ni swala la Muda.
Kwa alivyo na misimamo hata ningekua bakhresa kipato hakiwez kumyumbisha.
Kwanza nikimzingua hajali kuwa mim ni boss kazin kwangu wala nini ni mwendo wakufokewa hadi ulie kama mtoto.
Na sio kama hana kipato.
Ana kazi nzuri tu,hapa naandika yuko zake angan huko safar ya kikaz na siku zote ananichukulia kama sina kipato na hajawahi kula hata mia yangu.Ni type ya wanaume masikin jeuri hababaishwi na hela ya mtu
 
Kwenye maisha yako,Kuna mtu alikuwa na saut kama ya dear wako,ulikuwa unamuogopa,inawezekana ni baba,kaka,ndugu,
Cha kushangaza mkuu sijawahi kuwa na mtu mwenye kauli juu yangu hapo mwanzo.
Maisha yangu nimekua naongoza watu.Nimezoea watu ndo wananisikiliza mimi mpaka alivyokuja huyu mwanaume maishani mwangu ndo yeye amekua mtu pekee ambae ana sauti ya mamlaka kwangu
Baba alishafariki siku nyingi
 
Ndo uanamke wenyewe huo wala usiogope...Sio hawa akina Mwajuma hashikiki,mdomo mrefu,macho makavu na maneno pipa zima kwa wanaume zao.
 
Umenikumbusha na wa kwangu tukiwa tunachat nikimkera anakuaga mkali kwenye sms ila nikimpigia simu au tukiwa live tuyamalize maneno yote yanamuisha Yani anakuwa siyo yule wa kwenye sms.....hii inafanya hata ugomvi uwe mkubwa vipi ,na solve kwa muda mfupi
Story of my life😂.
Kwenye sms unajimwambafai ila ukiambiwa uyarudie live mdomo haufunguki😂
 
Back
Top Bottom