Namuogopa mpenzi wangu nikisikia sauti yake

Namuogopa mpenzi wangu nikisikia sauti yake

amen mkuu.
Copied
Muelewe na ujitahidi kuweka heshima mbele sana kwa huyo mwenzio kwani anatambua uzuri ulionao ila hawezi zuia wivu alionao kwako hata kusababisha maelewano hafifu baina yenu lkn wewe kama mama kiungo shikilia upendo amani ndani ya nyumba yeye atakuja kwako akinyenyekea huo upendo na uvumilivu ulionyesha na kutenda vyema kwake!
 
Honestly mkuu hata mim kuna saa nahisi ana elements za kiutawala.
Wazungu huwa wanaamin kabla ya maisha haya tulishaishi maisha mengine tukiwa watu wengine.Kama ni kweli basi nahisi huyu alikua mtawala aliyeheshimika na kuogopewa
Ni hivyo mi nimekaa na watu juzi tu nikaambiwa naunguruma na kupiga makelele huku tunaongea tu.
Ni mtazamo tofauti..
Huko juu kusini, hakuna kuremba wala geita we utachezea vichapo tu ni visu , mapanga kwaheri
 
wanawake ambao wako decent kama wewe...nowadays ni wachache mno yaani ni kama kutafuta bikra kwa changudoa, so rare.

wanaume tunapenda wanawake wanaotuheshimu...yaan sio mbishi, sio mropokaji anayesikiliza n kuelewa.

kwa hiyo ishu ya mtu wako hiyo ndo nature yake...you can't deal with a reality ishi naye tu hivyo hivyo, kama anakujali ni sawa...ukute yeye kuwa mkali ni defensive mechanism yake coz ataki ujue weakness yake.
 
Wala usijali ila zingatia ushauri niliokupa pengine usikufae leo ukakufaa siku zijazo
Huna cha kunishauri Lumbi, tupo kwenye mitandao usijifanye unawajua watu kuliko uhalisia, wewe kama umeguswa kunywa maji mengi pita kimya kimya.
 
Hello people.

Ndugu zanguni nina hali fulani hivi siielewi.

Nampenda sana shemeji yenu na kwa jinsi alivyo nimejikuta namuheshimu sana ila nahisi kama heshima imezidi hadi imegeuka woga hivi.

Japo huwa ananisaidiaga financially akijisikia ila nahisi ninamzidi kipato na simtegemei ila sijui kwanin sauti yake imekua na mamlaka sana kwangu,yaan nikisikia tu sauti yake sijui kwanini hata tone yangu inabadilika na kuwa ya upole na unyenyekevu mkubwa na huwa nalipima neno kabla ya kumwambia.

Kuna siku alinikasirisha sana na sikutaka tena kuendelea na mahusiano nae akawa akipiga sipokei then kwa hasira nikapanga akipiga nipokee then nimfokee nimjibu mbovu then nikate nimblock lakini cha ajabu nilivyopokea na kusikia sauti yake tu sikuweza tena kuongea nae kwa sauti ya ukali kama nilivyopanga na maneno makali niliyokua namwambia kwenye sms ukiniambia nimwambie kwa mdomo siwezi so nikaishia kuwa mpole kama mwanakondoo tu.

Sio mkatili wala sijalogwa ila nikimzingua ni mkali sana ila anajali na anajitahidi sana kunionesha upendo lakini sijui kwanini namuogopa hadi nakosa ujasiri wa kutoa madukuduku yangu kwake.

Mimi ni mwanamke.
Kuna wakati unaweza ukawa na maradhi na ukajihisi upo sawa. Unaweza ukalogwa na usijue kua umelogwa.
 
Kwa alivyo na misimamo hata ningekua bakhresa kipato hakiwez kumyumbisha.
Kwanza nikimzingua hajali kuwa mim ni boss kazin kwangu wala nini ni mwendo wakufokewa hadi ulie kama mtoto.
Na sio kama hana kipato.
Ana kazi nzuri tu,hapa naandika yuko zake angan huko safar ya kikaz na siku zote ananichukulia kama sina kipato na hajawahi kula hata mia yangu.Ni type ya wanaume masikin jeuri hababaishwi na hela ya mtu
Jipe muda.
Usiache kuja hapa kutoa mrejesho.
 
Kwa hiyo sina kasoro mkuu?
Lakin si inashauriwa kwenye mahusiano pakiwa na shida mkae muyaongee?Sasa mim nabakia kulia tu au kuitikia tu,hata kumbishia siwezi au hata kumkatisha akiwa anaongea siwezi hata kama nina hasira na unakuta nina vitu nataka kusema.Nikikabwa sana nakimbilia kumuandikia sms kwa mdomo siwez kumwambia.Na akikasirika ni mkali hata ukilia hajali
Umerogwa
 
Back
Top Bottom