Namuombea msamaha hayati Magufuli kwa makosa aliyoyatenda


..serikali, ambayo ni taasisi aliyoiongoza na kupelekea kufanya uovu ipo. hivyo serikali inapaswa kuomba radhi kwa makosa hayo.

..pia kuna chama ambacho alikuwa mwenyekiti wake, na alitenda kwa kutumwa na kuongozwa na chama hicho. hivyo chake chake kinapaswa kuomba radhi kwa mabaya yaliyotokea.

..Ni kweli Jpm amefariki, lakini walioathirika kutokana maamuzi yake mbaya wapo, hivyo wanastahili kutambuliwa na kuombwa msamaha.

..Mema ya Jpm yaandikwe ili wananchi wajifunze na kuyaendeleza. Mabaya ya Jpm nayo yaandikwe na kukemewa ili yasirudiwe tena.
 
Hapo umekosea, hakuna kitu kibaya kama kutoa uhai wa mtu kabla ya mda wake, ni dhambi kubwa na haisameheki duniani
 
Na pia narudia swali lako , akina nani wanaombwa msamaha na kwa makosa gani?
Haiwezekani watu wakaomba msamaha tu hewani
 
Clear
 
Siyo kwa Kigezo cha Mabaya machache na mazuri mengi. Nijuavyo ni mabaya mengi mno na mazuri machache sana.
 
Go with what is right even if we have different perceptions.
 
umesahau kuua wapinzani wake, kufirisi watu, kunyang'anya watu mali zao, nk
 
Rais wa sasa alisema kuwa Rais huwa hakosei sasa kama Rais hakosei Magufuli atakua hajakosea chochote.
 
Acha Ufala! 80% walimpenda, unaitoa wapi hiyo taarifa? Hivi Angeangaika kuiba kura kama alipendwa kiasi hichi? Au alipendwa na machizi wasio na sifa ya kupiga kura?
 
Kuna upotoshaji mkubwa sana unafanywa

1. Wanaosema marehemu hasemwi kwasababu hawezi kujitetea n.k. wanatumia kigezo dini.
JPM au kiongozi mwingine si viongozi wa dini bali wa nchi.

2. Wanaosema kumsema marehemu si utamaduni wetu, JPM na Viongozi wengine kama Nyerere si viongozi wa mila au tamaduni. Ni viongozi wa nchi

Viongozi wa nchi ni wa watu wote wakiwemo Wachawi, Majambazi, vibaka, wabakaji, wasomi, watu wa dini, wasio na dini, wafanyakazi, wafanyabiashara, wavivu, wapiga deal n.k.

Hawa nao wana nafasi yao katika kujadili viongozi kama kundi 1 na 2 hapo juu.

Kwa wanaoamini ni vibaya kumsema marehemu kwa dini hiyo ni imani yao.
Wanaoamini si utamaduni wetu huo ni utamaduni wao.

Imani na tamaduni za baadhi zisiwafunge wengine wenye haki zao

Muhimu kila mtu awe na ''Liberty'

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Mauwaji aliyofanya ni makosa madogo?

Watoto wamebaki ukiwa

Wanawake wamekuwa wajane

Familia zilivurugwa na wasiojulikana

Teuzi za kikabila

Wizi was pesa za uma kuxitumia bila kufuata bajeti

Kupeleka miradi ya maendeleo Kwa kufuata alikopigiwa kura na huku akijua nao wanalipa Kodi ni kosa dogo hilo.

Acha kututania

Bora amekufa na adhabu yake huko kuzimu iongezeke mara dufu.

Acheni mungu aitwe mungu
 
Hizi kelele za matusi kwa Magufuli zina mwisho ngoja Mabeyo astaafu kwanza, hii aibu ya matusi haivumilika hawa mende naona wamekosa ya kufanya, hukumu ni hapa hapa, haya mavuvuzela ndio yatakayo mwangamiza Samia na ndio yanayo mteta kila siku, tunatunza charts zao na voice note, muda utaongea, sasa hivi tunavunja vichuguu vyote hawa siafu watakuja tu. time never reverse
 
Ni vyema kuandika ili vizazi vijavyo vifahamu.

By the way msamaha wa jamaa ni kitabu chenye page kama 600 hivi. Maana huwezi kufukia yote kwa uzi mmoja wenye bullets tatu.
 
Kenge we
 
Kwa hiyo hawa wanaobambikiza tozo ndo malaika, wao hawastahili kuomba msamaha kwa kuwasababishia wananchi ugumu wa maisha huku wakijificha kwenye uviko, vita ya ukraine na kwenye kivuli cha marehemu?
 
mtamsema sana lakini hamtashinda mtamtumia CAG kumchafua lakini hamtashinda jpm bado atakumbukwa
 
Vipi na tuliopoteza wapendwa wetu ambao mpaka leo hatujui walipo? Lissu tunamwachia mwenyewe maana bado yupo hai akiamua kumsamehe au akidai fidia atajua mwenyewe

kaamulize mkapa aliwapoteza watu wangapi zanzibar pemba. makufuli kapoteza nani? kila siku azory azory
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…