Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa DSM?

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa DSM?

Picha zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao kuonyesha ufahari wa hali ya juu wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa dar es salaam.

Ofisi hiyo imekuwa tofauti kabisa na ile ya Mkuu wa mkoa aliyepita bwana Sadick, ofisi ya Makonda ina kompyuta kadhaa za apple,mapambo mengi ya kila aina yanayoashiria ufahari na utukufu wa hali ya juu kuliko hata ofisi ya rais.

Nani aligharamia ufahari huu wakati hata ikulu haijabadili muonekano? Kulikuwa na umuhimu wa kuweka ufahari huo katika kipindi hiki cha kubana matumizi?
Nini kilipungua katika ofisi ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa mpaka ufahari uongezwe katika jiji ambalo limezungukwa na wananchi wenye hali ngumu na maisha yasiyoridhisha.

View attachment 348618
HAHAHA HATA MIE NINGEKARABATUI ATII
 
Akili mbofu sana hizi, computer za apple sasa zinakuzingua nini?? acha ushamba, usilemaze akili kiasi hicho! Nyi ndo wale mtu mwenye gari unaona wa ajabu sana.
Kwanza ebu weka picha ya ikulu na pia ya ofisi ya sadick kabla ili tulimganishe!
 
Anakarabati ofisi au kairemba,, mwanaune anapenda urembo wakati watt wanakaa chini hyo pesa angenununua madawati
Kompyuta moja ya apple madawati mengi sana....naona bunge walibana wakapata za madawati
 
Vijana wengi wanapenda sana kujikweza ndio tatizo. Ofisi ya serikali sio dhambi kuwa mzuri Bali ilitakiwa iendane na aina ya serikali ziwe sawa na mikoa mingine amepita hadi baadhi ya ofisi za mawazir lakini ndio ujana huo
Tatizo mmezoea kuona makabati ya bati yamejaa mafaili mpaka milango yake haifungi.
 
Ukimjua aliyegharamia halafu wewe itakusaidia nini? Kwa mfano akiamua kutumia sehemu ya mshahara wake kwa ajili ya kununua computer au mapambo kuna shida? Acheni hizo.
Sheria hairuhusu kutumia pesa binafsi kwenye ofisi ya umma
 
Namuunga mkono Makonda kunadorisha office...office nyingi za umma zinatia aibu chafu na kila kitu cha kizamani...hazina hata motisha wa kufanyia kazi humo
.
Ni kweli mkuu unayosema lakini hujajibu swali lake la kuwa nani kagharimia?
 
Hahahahahaaaaa. Yaani mmemtafuta Makonda mmemkosa. Sasa mnaanza kuwa na wivu na ofisi yake. Imewauma sana kuona Ofisi yake inakuwa na hadhi nzuri kuliko Ofisi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Mtaa wa Ufipa licha ya kupokea mamilioni ya fedha za ruzuku
Swala ni kuwa tuko kwenye kubana matumizi hivyo hoja ya mtoa mada ni kuwa kwa wakati huu labda hilo la kupendezesha ofisi lisingekuwa kipaumbele na anaona kama gharama ya kupendezesha ofisi hiyo itakuwa kubwa ndio akataka kujua nani kalipa ni serikali au mfadhili? Tujikite kwenye hoja ya msingi. Maana anasema hata JPM mwenyewe pale ofisini kwake hajarekebisha toka alipotoka JK. Hayo mengine tuyaache twende kwenye hoja mkuu maana yeye kaanzisha kampeni ya madawati na vyumba vya madarasa labda watu walitegemea angeegemea huko kwani muda mwingi viongozi kama yeye huwa hawakai ofisini wanatakiwa kuwa field. Kumbuka hospitali nako bado vitanda havitoshi lakini pale ofisini kwake kila kitu Sadik alikiacha hivyo hakukuwa na shida sana ya makabati na mapambo
 
Picha zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao kuonyesha ufahari wa hali ya juu wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa dar es salaam.

Ofisi hiyo imekuwa tofauti kabisa na ile ya Mkuu wa mkoa aliyepita bwana Sadick, ofisi ya Makonda ina kompyuta kadhaa za apple,mapambo mengi ya kila aina yanayoashiria ufahari na utukufu wa hali ya juu kuliko hata ofisi ya rais.

Nani aligharamia ufahari huu wakati hata ikulu haijabadili muonekano? Kulikuwa na umuhimu wa kuweka ufahari huo katika kipindi hiki cha kubana matumizi?
Nini kilipungua katika ofisi ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa mpaka ufahari uongezwe katika jiji ambalo limezungukwa na wananchi wenye hali ngumu na maisha yasiyoridhisha.

View attachment 348618
Yaani wewe ni wa hovyo kabisa
Unataka mkuu afanyie kazi chooni?
Pale panaitwa bomani panastahili kuvunjwa kabisa kuondoa taswira s kikoloni
Serikali inaruhusu kupokea michango kutoka kwa wafadhili haswa ikiwa kama hiyo ya kurekebisha ofisi zake,hiyo ofisi sio ya makonda ni ya serikali
Chadema mnapenda sana uchafu,ndio maana lowassa kahamishia ofisi mikocheni toka ufipa kwenye banda la kuku
 
Niliona FB sikuona shida kwa kuwa japo ofisi imependeza ameonyesha uzalendo kwa kuwaunga mkono wazawa waliojiajiri...
Picha hizi mimi nimeziona thru waliotengeneza hii ofisi...ambao binafsi nawakubali kwani hawana hata gharama kubwa kama angeagiza fenicha za Mchina ambazo wala hazidumu kwanza
 
Alafu hizi kampeni chafu dhidi ya viongozi na waajiri wa serikali hazitazaa matunda, HII PICHA YA HII OFFICE NDO PIA ILIWEKWA HAPA JF IKIDAIWA NDO ILIKUWA OFFICE YA JULIET KAIRUKI, aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa TIC. Sasa sijui wanapokezana kuingia hiyo office!
Acha propaganda,yeye mwenyewe,lemutuz,walishapost picha instagram
 
Niliona FB sikuona shida kwa kuwa japo ofisi imependeza ameonyesha uzalendo kwa kuwaunga mkono wazawa waliojiajiri...
Picha hizi mimi nimeziona thru waliotengeneza hii ofisi...ambao binafsi nawakubali kwani hawana hata gharama kubwa kama angeagiza fenicha za Mchina ambazo wala hazidumu kwanza
Sijui tenda ilitangazwa au kila mtu anaokota mafundi,walilipwaje?
 
Picha zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao kuonyesha ufahari wa hali ya juu wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa dar es salaam.

Ofisi hiyo imekuwa tofauti kabisa na ile ya Mkuu wa mkoa aliyepita bwana Sadick, ofisi ya Makonda ina kompyuta kadhaa za apple,mapambo mengi ya kila aina yanayoashiria ufahari na utukufu wa hali ya juu kuliko hata ofisi ya rais.

Nani aligharamia ufahari huu wakati hata ikulu haijabadili muonekano? Kulikuwa na umuhimu wa kuweka ufahari huo katika kipindi hiki cha kubana matumizi?
Nini kilipungua katika ofisi ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa mpaka ufahari uongezwe katika jiji ambalo limezungukwa na wananchi wenye hali ngumu na maisha yasiyoridhisha.

View attachment 348618
Mlango sijaupenda,angeubadilisha na huo pia,au bado uko kwa fundi?
 
Back
Top Bottom