Vijana wengi wanapenda sana kujikweza ndio tatizo. Ofisi ya serikali sio dhambi kuwa mzuri Bali ilitakiwa iendane na aina ya serikali ziwe sawa na mikoa mingine amepita hadi baadhi ya ofisi za mawazir lakini ndio ujana huo
Ebu tuweni wakweli jamani....
Hapo unacho kisema wewe kimekuonyesha ufahari kwenye hiyo ofisi ya mkuu wa mkoa ni kipi hasa..!!
Au tuanze kuchambua kila kimoja baa da ya kingine?
1- APPLE
Hiyo ni aina ya computer ilio tengenezwa na kampuni ya Apple, kama aina nyingine yeyote.
1- TABLE
Hiyo ni meza ya kawaida kabisa tena imetengelezwa kwa nabaki ya vijipande vya mbao na kuwekwa kwenye muudo wa worden sheet kisha kufanyiwa mgandamizo, kisha hiyo wooden sheet imenakshiwa kwa aina nyingine ya mbao mtelezo ilio izunguka. Kimtazamo inavutia, ingawa haipo imara na unaweza ipata kwenye maduka yanayo uza office goods.
3- SOFA SET
Hivyo ni viti vya kawaida sana na unaweza ukavipata popote ulipo kwa urahisi na pia unatengenezewa kwa muundo, rangi na hata material kama utakavyo taka.
4- KABATI
Hapo naona kabati la kawaida kabisa, tena limetengenezwa kwa mbao ghafi ya bei ya chini kabisa ile nyeupe. Zaidi naona imeparazwa vizuri kwa mtelezo mzuri na kupakwa king'arishi saaafi huku ikuwa imepambwa na ngao yenye rangi ya dhahabu.
5- TABLE & CHAIRS
Naona pembeni kuna meza ilio zungukwa na viti vya kawaida kabisa, kwa huku uswahilini tunaweza tukapaita au panaonekana kama eneo lililo tengwa kwaajili ya chakula.
6- LIGHTS & PAINT
Hapo naona taa za kisasa na ofisi imepakwa rangi vizuri na tena inavutia.
Haya mseme sasa huo ufahari mnao usema ninyi upo wapi?
Kumbukeni kwamba serikali hutenga budget ya ukarabati wa ofisi pia (ingawa sina hakika ni kila baada ya muda gani).
Hivyo bado namsifu Makonda kwa matumizi mazuri ya pesa za ukarabati wa ofisi
Picha zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao kuonyesha ufahari wa hali ya juu wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa dar es salaam.
Ofisi hiyo imekuwa tofauti kabisa na ile ya Mkuu wa mkoa aliyepita bwana Sadick, ofisi ya Makonda ina kompyuta kadhaa za apple,mapambo mengi ya kila aina yanayoashiria ufahari na utukufu wa hali ya juu kuliko hata ofisi ya rais.
Nani aligharamia ufahari huu wakati hata ikulu haijabadili muonekano? Kulikuwa na umuhimu wa kuweka ufahari huo katika kipindi hiki cha kubana matumizi?
Nini kilipungua katika ofisi ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa mpaka ufahari uongezwe katika jiji ambalo limezungukwa na wananchi wenye hali ngumu na maisha yasiyoridhisha.
View attachment 348618