Nani alitangulia kati ya Yeriko Nyerere na Nashon C Elia kwenye suala la ujasusi katika dola na uchumi?

watu wengi mnamshambulia huyu kijana ambaye majuzi tu ameipa sifa nchi kwa tuzo. kama kukopi na kupaste ni rahisi kama mnavyomtuhumu, mbona ninyi hamjafanya hivyo?
 
Nimekuta mahali kitabu hiki (pichani) kinauzwa nikakumbuka Title yake inafanana na moja ya kitabu cha mwenzetu Yeriko Nyerere.
Nani kamuigilizia mwenzake? Kisheria imekaaje?

Yericko ndie mmiliki wa kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi kuanzia jina na maudhui yake, Alisajili katika mamlaka za serikali tangu 2016. Yeyote atakayeandika kitabu kwa jina la UJASUSI bila idhini au marejeo kwa Yericko atakuwa amevinja sheria.

Huyo Nashoni aliiba sehemu ya maandiko ya Yericko aliyokuwa akipost kwaajili ya matangazo ya kitabu cha Ujasusi huko FB ambako huwa anauzia kitabu kwamtindo wa kutoa makala fupi kutoka katika kitabu chake, Nashon akaungaunga na kuita kitabu, Yericko aliwahi kumfuta Nashoni nakumuonya asiendelee kuchapisha hako kakitabu akatii amri hiyo kuwa hata chapisha maudhui hayo wala jina la kitabu hicho.

Nadhani aliacha kuchapisha pale mtaa wa Agrey alipokuwa akichapa na kuuza kwa kificho sana, Hicho kinachoitwa kitabu cha Nashon sio kitabu ni kajarida ka kurasa 100+ tu. Wakati Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi cha Yericko kina kurasa 776.
 
Asante kwa maelezo mkuu. Nashon hajafanya vyema.
 
Mimi mwenye 'D' mbili za kidato cha nne Wacha nipige kimya!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…