Brojust
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 349
- 1,024
Dah sema maisha haya, Hii ishu ya kiboko ya wachawi inanikumbusha mambo mengi sana nakumbuka kipindi forex ndio ipo on fire mwaka 2017,2018,2019 nilipataga kazi kwa bwana mmoja anaitwa Fransisco Magnetics pale makumbusho Tanzanite tower floor number 6. Nikawa manager na baada ya mwezi mmoja tu akasema yeye anaenda likizo kumbe ndio anasepa na hela za watu waliowekeza, Nikabananishwa kumbe ana transaction ya zaidi ya 1B yaani mpaka leo hajawahi kukamatwa na bado anaonekana mitandaoni. Kilichonisaidia baadhi ya mali zake hasa furniture ziliuzwa ili mimi kutoka chini ya mikono ya polisi. Mungu aendelee kuwalaani wote wanaotafuta pesa kwa kudhulumu watu