Nani aliyetulaani wana wa mkoa wa Mara?

Mkuu wanafahamu sana wakurya wana wivu uliopitiliza pia majungu
Usidanganye watu wakurya hawapo hivyo. Wakurya hawana tabia ya kuongelea kwapani. Lao ni ndio au hapana na hawabebi umbea Wala majungu. Hao unao wasema wametoka Tarime au? Think again!
 
Walikufanya nn Baba swalehe ?
Alidandia mke wa mtu halafu wakam mind. Kule Sio uzaramoni mjomba, kule ni kwa wanaume na ndio maana ulishindwa kumudu mitikisiko.
 
A
Kuhusu Wakurya Mimi binafsi hunidanganyi. Hawa watu ni wafitini na watu wa kujipendekeza na kuchongea wenzao makazini. Waulize Polisi sasa hivi wanavyolia kwa kuongozwa na Mkurya. Ni wanafiki kuliko kawaida.
Acha uongo na unafiki wewe Bila Bila a.k.a 0 0 IGP Sio mkurya.
 
Mkuu kama hutojali hebu funguka kidogo kuhusu hiyo chui republic. Niliwahi kusikia habari yake wakati flan nikiwa mdogo ila memory ilifuta kwa sasa sikumbuki lolote
Ilikuwa 1978-79 Sidhani Kama ulikuwa duniani wakati huo.
 
Swala la romantic kwao liko kushoto, hafu wabahili hatari mi nilivopewa story zao nikaona uongo Mpaka yaliponikuta mazito
Wewe utakuwa ni kihaba tu, hebu nitajie kabila lolote hapa Tanzania linalogawa pesa tu kama US Aid.
 
Wacha wajifariji, usicheze na stress, hao wanaowasema wana majungu saa hizi bapo banana wanapiga ugali wa muhogo na mix kichuri na ukizinguwa unapewa live hapohapo.

Sijaelewa mtu anaposema eti mtu kama John Heche eti akutete, haya ni maajabu kwakweli.
 
Hizi ndoa za kina Shilole mwanzo na mwisho wake upo wazi kwa kila mtu, ukiweza kudumu miezi 6 fanya jubilee kabisa.
 
Nawakubali Wakurya sana hawana double standards . Wako very straight
Hapo umewatendea haki Wakurya, Mkoa wa mara una lugha na makabila zaidi ya 10 na yana desturi na tabia tofauti kabisa. Ukianzia kwa wajita na wakwaya huko majita hadi kwa wakurya, wasimbiti na wajaluo huko Tarime/Rorya kuna tofauti sana so sio vyema kwa mtoa mada kuongeleaa tabia ya kabila moja toka Mara na akawaunganisha wana mara wote.
 
Soma upya mada inasemaje? Mtoa mada amehoji maendeleo ya mkoa wa Mara na hajaongelea kabila hata moja, ila nyege za wachangiaji ndio wameingiza makabila without knowing how, na kuna malaya wawili humu wamepigwa chini na jamaa kutoka huko Mara hasira zao na stress zao wamekuja kuzituwa humu.
 
Mumuogope Mungu, mbona mnayoyaongea mimi mkurya (Mwireghi) wa kijiji cha Itiryo wilaya ya Tarime siyaoni? Unajua asili ya koo katika makabila mengi ya Tanzania? Unajua kwa nini tulikuwa na mapigano ya koo? unadhani ni chuki miongoni mwetu? wakulima na wafugaji wanvyopigana ni kwa sababu ni koo tofauti ndani ya kabila moja? Mbona wanaJF wanaparurana kila siku humu kwa sababu ya itikadi zao za kisiasa tena kwa matusi mazito sana, wangekuwa wanaonana uso kwa uso si ingekuwa balaa. mbona waireghi, watimbaru, wanyabhasi na koo zingine tunaishi vizuri sana, tunaoana, tunafanya biashara pamoja tena kipindi hiki ambako wizi wa mifugo haupo kwani imeisha. Wakati mwingine ni vizuri kuchangia kitu ulicho na hakika nacho, si tu umezaliwa unasikia wakurya wakorofi na wewe unaamini hivyo hivyo, mambo yanabadilika sana. Tatizo la wakurya hawapendi longolongo akipewa ofisi walozoea misheni town wanakiona cha moto, na sisi wabongo wengi tulishazoea dili. Mwisho Wakurya ni miongoni mwa makabila mazuri na rahisi sana kuishi nao ukiacha matatizo machache kama ya domestic violence na haya yanaendela kupungua
 
Na mimi sikuwa namjibu mtoa mada, kuna wachangiaji wameamua kuattack kabila moja na kunitoa kwenye mada. Nikiwa muhusika wa hilo kabila naona si sahihi. Nimekupata mkuu
 
Na mimi sikuwa namjibu mtoa mada, kuna wachangiaji wameamua kuattack kabila moja na kunitoa kwenye mada. Nikiwa muhusika wa hilo kabila naona si sahihi. Nimekupata mkuu
Mwanaume yeyote rijali angetamani azaliwe Mkurya ila ndio hivyo kuzaliwa ni jambo auto sawa na mimi nilitamani nizaliwe Finland ila haikuwa hivyo.
 
Kwani mnatumia vigezo gani kusema mkoa wa Mara uko nyuma kimaendeleo? mbona ndio hali halisi ya nchi hii?kuna mkoa usiokuwa na imani za kishirikina nchi hii? Hizo rasilimali kama madini zingewanufaishaje wana Mara kama zilikuwa mikononi mwa wageni? Wakati biashara ya sangara ikiwa kwenye peak wavuvi walikuwa wakiuza kilo moja kwa Sh 600 hadi 1000. Wenye viwanda wakichakata na kupeleka ulaya wanauza USD 20 kwa 1kg. Tarime tulikuwa tunalima kahawa sana, lakini chama kikuu cha ushirika (Mara cooperative union- MCU 1984) kwa kushilikiana na serikali wakakiua kwa kuwakopa wakulima kahawa bila kulipa, wakaacha kulima kwani huwa hatupendi upumbavu. Wilaya ya Rorya na Musoma vijijini ni wilaya zenye ardhi duni sana na walitegemea ziwa victoria (samaki hakuna) wamefaidi wahindi na wabongo wachache (Mawakala).
 
Labda ni mtani wa kabila mojawapo Mara, hawajui Mara kuna makabila mengi pengine kuliko mkoa mwingine wowote hapa Tanzania. Sasa mtu kafanya kazi na mtu mmoja au wawili inakuwa kama amefanya kazi na makabila yote. sisi Wakurya ni miongoni mwa watu wasio na unafiki wala longolongo.
 
Umenena vyema sana na kweli umefika tarime/Rorya, hii ndo hali halisi na wachangiaji wengine wajifunze kuacha kuokota maneno na kujifanya wajuaji kumbe hakuna kitu. Sota imechoka kwa kuwa samaki nao wameisha na ardhi ya kilimo ni duni sna na sio wafugaji. Naamini ulipita centre ya Kabwana pia kuna hospital nzuri sana. Miaka ya 1980 hadi tisini wakati machimbo ya dhahabu Nyamongo yakiwa mikononi mwa wananchi ndo wakati mji wa Tarime uliamka na kuchangamka, walivyobinafsisha mgodi, wakaua kilimo cha kahawa, tukaibiana ng'ombe kupeleka Kenya kidogo tuliyumba. Lakini tunasonga mbele
 
Wabongo wengi ni watu wa kukariri tu, ni sawa na imani ya kijinga kusema wahehe wanakula mbwa mnyama wakati kwao mbwa maana yake ni maharage,

Au kuwasifu wachaga wizi wakati wachaga wengi wapo smart na Muhimbili ina madaktari wengi wachaga wanaokoa maisha yao kila siku nyau hawa.

Dar es salaam au Mzizima ni ya Wazaramo, kwa ukarimu wa Wazaramo kuwakaribisha hawa nyau sasa hivi kila siku wanawadharau Wazaramo kwa kuwakaribisha kwenye Bandari salama yao.

JF zamani ilikuwa ni kisima cha fikra pevu lakini sasa kimejaa wahanga wa stress za maisha hasa baada ya mchina na ujio wake wa Smartphone za bei poa imekuwa tabu wanafunzi wanaacha kufanya home work zao nao wajifanya wajuwsji shenzi kabisa.
 
Mkuu umenena kweli kabisa, miaka ya hivi karibuni kuna watoto wachache wamefanya humu kama kijiwe cha wahuni tu. Huwa napitia thread nyingi kila siku baada ya kazi na huwa nasikitika sana. Ingawa wengi bado wanatoa michango mizuri na mizito na ndo maana lazima nipite humu. Hii thread ya leo imenilazimu kucomment kwani bahadhi wanaongea uongo usio na lazima yoyote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…