Nani ameiroga Afrika, Zimbabwe imetuma wanamichezo 9 na viongozi 67 Paris kwenye mashindano ya Olympics

Nani ameiroga Afrika, Zimbabwe imetuma wanamichezo 9 na viongozi 67 Paris kwenye mashindano ya Olympics

Wakati wakipita juu ya mto wakiwa kwenye boti kila mmoja alijiuliza mbona wengi sana baadaye inatoka taarifa kuwa wanamichezo ni 9 na ma-afsa wa serikali kutoka wizara mbalimbali ni 67 na watakaa kwa siku 16 zote za olimpiki hapa paris.

Sijajua Bongo aka nchi ya kitu kidogo tumepeleka wangapi maana wasanii tu tunapeleka nje kwa kodi zetu , MUNGU ATUSAIDIE


USSR
Acha afisa wa REVINUE ya Zimbabwe ale maishaa.
 
Kuna watu wanaamini eti VIONGOZI wa Afrika eti wataleta maendeleo.
Ugonjwa mbaya sana huu wa kushindwa kuona na kusikia.
 
Ni kama nilivyoandika, tumedanganywa vya kutosha. Nyerere alikuwa ni picha tu Ikulu, aliyekuwa anatutawala ni mzungu Muingereza, kwa miaka yote ya Nyerere.

Waafrika bado tunatawaliwa mpaka tugeuke tuwe kama anavyofanya Ibrahim Traore wa Burkina Faso.

Anaebisha namuwekea ushahidi.
Story za kwenye alqasus hizi
 
Hata CCM wanafanya mbona...Mradi wa Milioni 10 unajadiliwa kwa posho ya Milioni 89?Na bado haukamiliki.
 
Sisi fedha yetu na maliasili zote kashika nani?

Tanzania leo huwezi kuagiza au kununuwa chochote nje bila kutumia fedha za 'kigeni", zetu zimekaa show tu?

Hivi fedha za kigeni zina thamani zaidi ya dhahabu, ardhi, mifugo na madini yetu?

Fikiri.

Ingekuwa hawatutawali kuchumi saa hizi wangekuwa wanatupoigia magoti kwa mali ghafi tulizonazo.

Qalioweka misingi ya nchi hii waliiweka mibovu kwa makusudi kabisa. Tulikuwa tunahitaji watu kama Ibrahim Traore kuanzia uhuru.
Kudos
Imebidi nijicheke mwenyewe, Nashukuru sana, kuna kitu umenisaidia kuwaza.
Inauma sana, mbugani kwetu waarabu wanashindana kuwinda wanyama wetu kujifuraisha na wengine wamewachukua kwenda kutengeneza Mbuga kwao, lakini hakuna shida yoyote, sasa kule vijijini ukikamatwa na kanyama ka nyani umekwisha!! Yaani nyama zetu wahsnzi wachezee sisi wenyewe hata kula makosa ya kisheria.
 
Mwafrika kwenda Ulaya kwa mabwana wakubwa zake ni sifa kubwa.

Sote tuna uhuru wa kujiliwaza tu, lakini tunaendeshwa na wazungu, tena tulivyotawaliwa sasa kiutumwa mambo leo ni pabaya zaidi kuliko utumwa wa kununuliwa kwa shanga na vioo.

Tumejazwa ujinga na umetujaa.
hao wameenda kupiga per diem na vacation ya bure punguza chuki na walaya naamin kama team yao ya mpira ingefuzu msimu uliopita basi serikali nzima ingehamia Qatar ni
 
Wakati wakipita juu ya mto wakiwa kwenye boti kila mmoja alijiuliza mbona wengi sana baadaye inatoka taarifa kuwa wanamichezo ni 9 na ma-afsa wa serikali kutoka wizara mbalimbali ni 67 na watakaa kwa siku 16 zote za olimpiki hapa paris.

Sijajua Bongo aka nchi ya kitu kidogo tumepeleka wangapi maana wasanii tu tunapeleka nje kwa kodi zetu , MUNGU ATUSAIDIE


USSR
Tatizo kwa michuano ya Olimpiki ni ule utaratibu wao. Kwamba huamui tu mwenyewe idadi ya wanamichezo wa kushiriki kwenye michuano hiyo. Kuna viwango lazima kuvifikia ili mshiriki atimize vigezo.

Sasa, kwa mazingira hayo, michujo husababisha nchi nyingi za Afrika kupeleka wanamichezo wachache na kwa michezo michache kwani ndiyo waliotimiza vigezo.

Pia, Olimpiki wenyewe huwa na mialiko ya viongozi mbalimbali wa kushuhudia michuano hiyo.

Wao huamini, kuwepo kwa viongozi kwenye hiyo michuano kunaweza kuwa chachu kwao kuweka mipango mizuri ili michuano ijayo kuwa na wanamichezo wengi wenye vigezo.

Ova
 
Back
Top Bottom