Nani amelipa Tsh Milioni 200 tangazo la Tanzania kwenye jengo la Burj Khalifa, Dubai?

Mleta mada una uhakika kuwa malipo yalifanyika? Je, umeleta invoice au receipt?
Je, rangi za bendera zilizooneshwa si zenyewe? Sasa kama ni zenyewe tatizo liko wapi??
Jaribuni kuwa positive japo siku moja moja!
Lile ni jengo lina sifa yake... Na kama nchi inayojitahidi kurudi ulimwenguni kutoka kusikojulikana ni wazi kuna jitihada kutumia kila aina ya upenyo upatikanao!!
Kwa hili hakuna baya! Labda kama unaushahidi wa maovu mengineyo_
 
Acha kulalamika lalamika.Biashara yoyote ni matangazo.Wewe unatumia ngapi,kununua bando za kuingia mitandaoni,kama kampuni za simu,zisingetangaza vifurushi vyao,wewe utajuaje wana vifurushi vya bei gani,vya aina gani,na kila biashara bila matangazo,huwezi kuwafikia wateja wengi kwa wakati mmoja.Katika vitu vya kusaidia biashara(Aids to trade)ni matangazo.Tanzania bila kujitangaza,na kuonekana,hakuna atakayejuwa kama tuna vivutio vya kitalii,vya aina gani,madini ya aina gani, mazao,mifugo samaki matunda,mbogamboga,bahari,maziwa,mito,miti,wanyama nk.Tanzanite iko Tanzania tu,lakini ilipokosa kutangazwa,ilikuwa wanunuzi,wakinunua nchi jirani na nchi za mbali,wakigongwa bei lakini kwa matangazo,wanunuzi watajuwa iko Tanzania tu,dunia nzima.
Na ka mifugo ni hivyo hivyo,kuna nchi mifugo yao inakula makaratasi na mabox ,kutokana na kukosa majani, nyama inakuwa sio nzuri.Lakini Tanzania wanyama wanakula majani,wanunuzi wa nje,wakijuwa hivyo,watataka mifugo inayokula majani.Na kila bidhaa ndio hivyo hivyo,kahawa,parachichi,katani,nk.Katani ya Tanzania,ndio inasafirishwa kwenda nje,falme za kiarabu,kutengeneza Jipsum,wanasema jipsum ya kataini ya Tanzania ni bora,lakini hiyo katani inasafirishwa nje,kutoka Tanzania na wageni kama wasudani,utafikiri wao ndio wanalima katani,sisi wenyewe kazi yetu ni kulalamika tu.Kukiwa na fursa,fatilia,ufanye biashara,acha kulalamika.
 
Nilivyoona Mawaziri mliokwenda Dubai nikajua tu lazima kuna kitu tutalizwa.
Acha nongwa mwanakwetu hata marekani kawekeza UKRAINE! Malengo ni kinazaliwa nini na utavuna kiasi gani! Tusiwe na mawazo ya kula mpaka mbegu! Tule kiasi nyingine tuzipande tuvune!
 
Unajua faida yake wewe hilo tangazo?

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Ngorongoro si inakaribia kuuzwa tena, au hujui?
 
Baadhi ya watanzania,kazi yao kulalamika,fursa za kupata kipato,zikija anabakia kulalamika.Wageni wanazitumia hizo fursa,mpaka wao wanashangaa wanasema watanzania ni watu wa ajabu,wakati nchi ina fursa nyingi za kufuatilia ofisi zinazohusika,wao ni kulalamika.Leo mgeni,anakuja Tanzania anazifuatilia fursa,na kuzifanyia kazi.Utamkuta mgeni ndio anasafirisha bidhaa kadhaa nje,madini,mazao kama katani,leo katani inakwenda falme za kiarabu,wamegundua katani ya Tanzania ndio nzuri,kutengeneza jipsum,wasafirishaji wa hiyo katani,ni wageni sio watanzania,sisi ni kulalamika tu,kwa jambo hata mtu hana ushahidi nalo.
 
Ndo umeishia hapo kufikilia
 
Ndo umeishia hapo kufikilia
Badala ya kufuatlia fursa za kibiashara na uwekezaji,utaona baadhi ya watanzania wanafatilia matangazo ya biashsra ya uwekezaji.Na kuhoji matangazo yamelipiwa shilingi ngapi,bila matangazo,huwezi kuuza ulichonacho nacho.
 

Ujinga Mzigo” hilo kwangu ni tusi kubwa
Sikukuudhi kwa chochote bali nimechangia mawazo yangu tu Ila wewe ukaamua ku comment kwa kusema hivyo

Nisome michango yangu katika jamii utanijua mimi ni mtu wa aina gani
Sina makuu wala kuchokoza na kutukana kama sijachokozwa

Sikupendezwa na jibu lako na lilinikera kama matusi yangu yamekuuma naomba radhi sana
 
Kwa dunia ya leo kama hawezi kujua umuhimu wa kujitangaza au kutangaza ulichonacho ili kivutia wateja na wawekezaji basi una shida mahali
Hivi unajua gharama ya tangazo la voda dk 1 tu kwenye television
Mimi natamani tungeweka utaratibu wa kutangaza hata kila mwenzi angalau kivutio kimoja watu waone fursa, siku nyingine waweke mountain Kilimanjaro nk
Tusijifunge na fikra za kujifungia ndani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…