Mamlaka ya uendeshaji wa jengo refu zaidi duniani la Burji Khalifa lililoko Dubai hutoza kati ya dola 67,000 hadi 87,000 ambazo kwa ubadilishaji fedha kwa haraka haraka inafiki Tshs. Milioni 157 hadi 200 hivi kwa dakika 3 kuweka tangazo kwenye jengo lote la Burji Khalifa.
Fedha hii kwa nchi masikini kama hii bado ni kubwa na ingeweza kufanya jambo la maana. Jana Februari 28 jengo hilo limetangaza bendera ya Tanzania kwa dakika 3 na wenye Serikali yao wakatutangazia neema kwamba nasi tumeonekana Dubai.
Hebu tuzionee huruma fedha za walipa kodi wanaojikamua huku sisi viongozi tukiishi kwa anasa.
View attachment 2134765
Acha kulalamika lalamika.Biashara yoyote ni matangazo.Wewe unatumia ngapi,kununua bando za kuingia mitandaoni,kama kampuni za simu,zisingetangaza vifurushi vyao,wewe utajuaje wana vifurushi vya bei gani,vya aina gani,na kila biashara bila matangazo,huwezi kuwafikia wateja wengi kwa wakati mmoja.Katika vitu vya kusaidia biashara(Aids to trade)ni matangazo.Tanzania bila kujitangaza,na kuonekana,hakuna atakayejuwa kama tuna vivutio vya kitalii,vya aina gani,madini ya aina gani, mazao,mifugo samaki matunda,mbogamboga,bahari,maziwa,mito,miti,wanyama nk.Tanzanite iko Tanzania tu,lakini ilipokosa kutangazwa,ilikuwa wanunuzi,wakinunua nchi jirani na nchi za mbali,wakigongwa bei lakini kwa matangazo,wanunuzi watajuwa iko Tanzania tu,dunia nzima.
Na ka mifugo ni hivyo hivyo,kuna nchi mifugo yao inakula makaratasi na mabox ,kutokana na kukosa majani, nyama inakuwa sio nzuri.Lakini Tanzania wanyama wanakula majani,wanunuzi wa nje,wakijuwa hivyo,watataka mifugo inayokula majani.Na kila bidhaa ndio hivyo hivyo,kahawa,parachichi,katani,nk.Katani ya Tanzania,ndio inasafirishwa kwenda nje,falme za kiarabu,kutengeneza Jipsum,wanasema jipsum ya kataini ya Tanzania ni bora,lakini hiyo katani inasafirishwa nje,kutoka Tanzania na wageni kama wasudani,utafikiri wao ndio wanalima katani,sisi wenyewe kazi yetu ni kulalamika tu.Kukiwa na fursa,fatilia,ufanye biashara,acha kulalamika.