Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 524
- 829
Kwa masikitiko makubwa, sisi wakazi wa Kinondoni tunapaza sauti zetu kulalamikia kitendo cha kumegwa kugawiwa kwa sehemu kubwa ya uwanja wa wazi wa Biafra kwa mfanyabiashara binafsi ambaye tayari ameanza ujenzi wa yadi ya magari ya kuuza.
Hatua hii imechukuliwa bila kushirikisha wananchi ambao ndio watumiaji wakuu wa eneo hilo kwa shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi. Eneo hilo limekuwa chini ya Halmashauri ya Manspaa ya Kinondoni ambao wamekuwa wakilisimamia.
Pia soma ~ Bado siamini CCM imetoa eneo la Biafra kwa mfanyabiashara wa showroom wakati lilikuwa tija zaidi kijamii
Tunaamini kuwa rasilimali za umma hazipaswi kutolewa kwa watu binafsi bila kufuata taratibu za uwazi na ushirikishwaji wa jamii. Mpaka sasa tunashindwa kuelewa mamlaka zimewaza nini kuchukua uamuzi huo! na kwanini iwe sasa?
Tukumbuke uwanja huo wa Biafra umekuwa muhimu katika matumizi ya umma ikizingatiwa eneo hilo lipo sehemu ya katikati ya Mji, maeneo ambayo ni nadra kupata viwanja vya wazi kwa ajili ya shughuli za umma mfano mikutano ya kisiasa au matamasha, michezo na masuala mengine ambayo yanaleta umma pamoja.
Pia soma ~ Meya Kinondoni: Kuna mapungufu yaliyofanyika; Serikali iliwapa CCM Uwanja wa Biafra kwa ajili ya kuendeleza michezo