DOKEZO Nani ameruhusu uwanja wa Biafra-Kinondoni uliokuwa unatumika kwa shughuli za umma umegwe kwa mfanyabiashara?

DOKEZO Nani ameruhusu uwanja wa Biafra-Kinondoni uliokuwa unatumika kwa shughuli za umma umegwe kwa mfanyabiashara?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Nchi ya wachuuzi kila eneo wao wanawaza kujenga frames tu. Wao wanaita hivyo viwanda. Coco beach imechukuliwa, biafra imechukuliwa, ujenzi wa frames utafika kila kona ni swala la muda tu.
 
Walaaniwe waliowezesha haya kufanyika
Pale walianza kuwapangisha watu magereji,wauza mavitanda,madalali wa magari,
Wakaja wale wazee wa coster special hire
Sahv serikali ya mtaa inapigania waAchiwe kisehemu kdg cha michezo tu
Enzi zetu hapo tumecheza sana mpira uwanja mmoja huo kunachezeka mechi hata 4
Huko kuna watoto wa care kule kuna wanangu wa blackboard kutoka blok 41
Sahv pamejaa mafuso ya mchanga na uchafu mwingine
Hii serikali haijuwi kabisa umuhimu wa maeneo ya wazi

Ova
 
Nchi ya wachuuzi kila eneo wao wanawaza kujenga frames tu. Wao wanaita hivyo viwanda. Coco beach imechukuliwa, biafra imechukuliwa, ujenzi wa frames utafika kila kona ni swala la muda tu.
Uchafu mtupu

Ova
 
Soon wataenda uwanja wa magunia msasani napo
Sijui kama patapona

Ova
 
Kwa masikitiko makubwa, sisi wakazi wa Kinondoni tunapaza sauti zetu kulalamikia kitendo cha kumegwa kugawiwa kwa sehemu kubwa ya uwanja wa wazi wa Biafra kwa mfanyabiashara binafsi ambaye tayari ameanza ujenzi wa yadi ya magari ya kuuza.

Hatua hii imechukuliwa bila kushirikisha wananchi ambao ndio watumiaji wakuu wa eneo hilo kwa shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi. Eneo hilo limekuwa chini ya Halmashauri ya Manspaa ya Kinondoni ambao wamekuwa wakilisimamia.

View attachment 3411055
Uwanja wa Biafra umekuwa sehemu ya kihistoria na maisha ya kila siku ya jamii ya Kinondoni, ambapo kwa muda mrefu umetumika kama jukwaa la mikutano ya hadhara, majadiliano ya kijamii, na hata minada ya bidhaa inayowasaidia wafanyabiashara wadogo kupata kipato, ambapo eneo hilo ufanyika mnada wa kila jumamosi.

Tunaamini kuwa rasilimali za umma hazipaswi kutolewa kwa watu binafsi bila kufuata taratibu za uwazi na ushirikishwaji wa jamii. Mpaka sasa tunashindwa kuelewa mamlaka zimewaza nini kuchukua uamuzi huo! na kwanini iwe sasa?

Tunatoa wito kwa mamlaka za juu ikiwemo Wizara ya TAMISEMI, TAKUKURU kufuatilia kwa ukaribu suala hili na kufanya tathmini ya kina kwa kushirikiana na wakazi wa eneo hili ili kama kuna mazingira tatanishi ya kukosekana kwa uwajibikaji wahusika wawajibike.

Tukumbuke uwanja huo wa Biafra umekuwa muhimu katika matumizi ya umma ikizingatiwa eneo hilo lipo sehemu ya katikati ya Mji, maeneo ambayo ni nadra kupata viwanja vya wazi kwa ajili ya shughuli za umma mfano mikutano ya kisiasa au matamasha, michezo na masuala mengine ambayo yanaleta umma pamoja.
Wahuni aliowasema Polepole ndiyo wameuza uwanja huo...#KATAA_WAHUNI.
 
Daah viongozi wote wamepaacha wazi hapo ila sasa hivi wameanza kupamega kazi ipo maeneo si yapo huko nje ya mji kwani lazima wauzie magari mjini..
 
Daah viongozi wote wamepaacha wazi hapo ila sasa hivi wameanza kupamega kazi ipo maeneo si yapo huko nje ya mji kwani lazima wauzie magari mjini..
Kuna miaka fulani kinondoni alikuwepo diwani lupiana
Alikuwa na bar inaitwa vijana jirani kulikuwa uwanja garden
Yule fala kwenye mazungumzo anasema anataka katika ya uwanja awake mnara wa kampuni ya sim,mm nkamwambia hivi weee unataka watu,watoto wakacheze wapi
ohh mnara sijui unaingiza kipato blahblah ....ila lupiana alikujaga kata moto

ova
 
Kuna miaka fulani kinondoni alikuwepo diwani lupiana
Alikuwa na bar inaitwa vijana jirani kulikuwa uwanja garden
Yule fala kwenye mazungumzo anasema anataka katika ya uwanja awake mnara wa kampuni ya sim,mm nkamwambia hivi weee unataka watu,watoto wakacheze wapi
ohh mnara sijui unaingiza kipato blahblah ....ila lupiana alikujaga kata moto

ova
Kama wamevamia hapo basi maeneo mengi yatavamiwa aisee..
 
Aliyeruhisu ni awamu ya sita.uwanja ule wamemuuzia mwarabu wa Dubai aitwaye do world ili kujenga supermarket kubwa yenye bidhaa zilizotengenezwa dubai
 
Kuna watu hawana aibu kabisa. Mtu akiona kiwanja cha wazi tamaa inamjaa.
 
Hii issue nimeshawah igusia, inahusu sana serikali haswa ngazi za chini, kuanzia mwenyekiti wa mtaa, mtendaji, diwani, ofisi ya ardhi manispaa, na mwisho kabsa ofisi ya manispaa yenyewe, ss ukiangalia kwa makini, mwenye kiti wa mtaa+ mtendaji+diwani hapa lazma washakula rushwa, yaan hamna explanation ingine. We unaona kabsa eneo la wazi ambalo linatakiwa kutumika na jamii iliyoizunguka anatokea boya flan ana hela anahonga honga serikali za mtaa na diwani paap ikifika manispaa unaona mtu ana tittle deed, hili swala kwakweli ni Tanzania nzima lipo. Hapa najib hii thread kuna kesi ya malalamiko sisi wananchi tumeshaipeleka mpaka kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro juu ya uvamizinwa eneo la wazi, hii kesi inakaribia miaka 3 sasa hvi (2025) na bado walalmikaj tunazungushwa hamna jibu la maana linalotolewa kwa wahusika wenyewe ambao ni manispaa ya Moshi mjini. Tulifuatilia tukagundua tunayemlalamikia anahonga sana hela ofisi ya mkurugenzi wa manispaa yaani inawezekana mkurugenzi mwenyewe barua ya malamiko yetu hazimfikii zinaishia kwa wasaidizi wake. Hamna hatua yoyote imechukukiwa kwa mfanyabiashara tunayemlalamikia, zaidi yeye nikujigamba nakusambaza maneno kwamba amesha mwaganmilioni 25 huko ofisi za manispaa. Ss imagine kama mtu openly anaweza jigamba hivyo, huo uozo wa rushwa ulivyotanda kuanzia serikali za mitaa, diwani mpaka huko manispaa. Lazma niseme ukweli hapa Hii yote inatokana na watu kupewa uongozi badala yakuchaguliwa na wananchi, hichi kitu kimakera, kukatisha tamaa na kwakweli hatuna Imani kabsa na serikali yetu. Hii story ni ni ndefu hope one day ntaipost humu watu muisome kwa kina
#backbenchers
#UpuuuziUnaendelea
#manispaainanukarushwa
 
Uwanja wa Kawe hapa karibu na soko la samaki baada ya nyumba ya Kikwete wote umepigwa bati unajengwa majengo ya maana..Zamani vijana na watoto walikuwa wakicheza mpira hapo ila kwa sasa ni mwendo wa kumiliki nchi tu.

Nikiweza kupiga picha kesho nitakutumia uone. Yani hakuna uwanja wa wazi unaachwa, kila open space wanagawana. Watoto wetu wacheze wapi?

Soma Pia:
Nusu ya uwanja wa BI Afra uliopo Kinondoni haumilikiwi na wananchi tena ila unamilikiwa Waarabu.

Inasemekana Abdul mtoto wa mwenyekiti wa CCM kautoa nusu ya uwanja wa Bi Afra kwa kampuni kubwa ya magari kutoka uarabuni inayojulikana kama Jan Japan, ambayo inamilikiwa na Muhammad Jan ila hisa 75 za kampuni hii zinamilikuwa na Muarabu wa Dubai.

 
Back
Top Bottom