shatisuruali
JF-Expert Member
- Jul 28, 2016
- 966
- 3,050
Wale wa Kijitonyama Mipakani B pale uwanjani wanajenga nini?
TP nasikia na wenyewe umezungishiaa mabatiWale wa Kijitonyama Mipakani B pale uwanjani wanajenga nini?
Nani akuachie?Hakuna mtu ana huruma na mtu safari hii ni mwendo wa urefu wa kamba tuHizo open space watuachie wajameni, zile beach zetu za bure pia watuachie aisee.
Du kwa hio, ule ukarabiti unaofanyika pale ni yy anafanya ?Kuna fununu kuwa viwanja vya Mnazi Mmoja vinamilikiwa na l Rostam
Dar mmelegea sana. Wananchi waamke waende hapo wakang'oe hayo mabati..
Kwa masikitiko makubwa, sisi wakazi wa Kinondoni tunapaza sauti zetu kulalamikia kitendo cha kumegwa kugawiwa kwa sehemu kubwa ya uwanja wa wazi wa Biafra kwa mfanyabiashara binafsi ambaye tayari ameanza ujenzi wa yadi ya magari ya kuuza.
Hatua hii imechukuliwa bila kushirikisha wananchi ambao ndio watumiaji wakuu wa eneo hilo kwa shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi. Eneo hilo limekuwa chini ya Halmashauri ya Manspaa ya Kinondoni ambao wamekuwa wakilisimamia.
Uwanja wa Biafra umekuwa sehemu ya kihistoria na maisha ya kila siku ya jamii ya Kinondoni, ambapo kwa muda mrefu umetumika kama jukwaa la mikutano ya hadhara, majadiliano ya kijamii, na hata minada ya bidhaa inayowasaidia wafanyabiashara wadogo kupata kipato, ambapo eneo hilo ufanyika mnada wa kila jumamosi.
Tunaamini kuwa rasilimali za umma hazipaswi kutolewa kwa watu binafsi bila kufuata taratibu za uwazi na ushirikishwaji wa jamii. Mpaka sasa tunashindwa kuelewa mamlaka zimewaza nini kuchukua uamuzi huo! na kwanini iwe sasa?
Tunatoa wito kwa mamlaka za juu ikiwemo Wizara ya TAMISEMI, TAKUKURU kufuatilia kwa ukaribu suala hili na kufanya tathmini ya kina kwa kushirikiana na wakazi wa eneo hili ili kama kuna mazingira tatanishi ya kukosekana kwa uwajibikaji wahusika wawajibike.
Tukumbuke uwanja huo wa Biafra umekuwa muhimu katika matumizi ya umma ikizingatiwa eneo hilo lipo sehemu ya katikati ya Mji, maeneo ambayo ni nadra kupata viwanja vya wazi kwa ajili ya shughuli za umma mfano mikutano ya kisiasa au matamasha, michezo na masuala mengine ambayo yanaleta umma pamoja.