Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Tangu jana, mara baada ya Wakili Tundu A.M. Lissu kutangaza kugombea uenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, kumekuwa na 'kuwapambanisha' Mwenyekiti wa sasa Freeman Mbowe na Lissu kwenye uchaguzi wa CHADEMA utakaofanyika mwakani.
Kuna siku nilimsikia Lissu akisema kuwa mtia-nia yeyote ndani ya CHADEMA huwasilisha nia yake hiyo kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA. Hadi hapo, taarifa rasmi za mtu fulani kugombea nafasi fulani ndani ya CHADEMA hutolewa na mgombea mwenyewe au Katibu Mkuu.
Sikuwahi kumsikia Mbowe au Katibu Mkuu Mnyika kutoa taarifa rasmi kuwa Mbowe atagombea tena uenyekiti wa CHADEMA Taifa kwenye uchaguzi ujao. Sasa, nani hasa anatuaminisha kuwa Mbowe na Lissu watapambania uenyekiti wa CHADEMA?
Binafsi, naona kumeshakuwa na maridhiano na makubaliano baina ya Mbowe na Lissu kuachiana nafasi hiyo ya uenyekiti. Kama Mzee Mtei alivyomwachia Hayati Bob Nyange Makani; Makani alivyomwachia Mbowe ndivyo sasa Mbowe anavyomwachia Lissu.
Endapo Mbowe atagombea, mchuano utakuwa mkali na CHADEMA haitabaki salama baada ya uchaguzi huo. Kwa kauli za Lissu juu ya uchaguzi huru na haki na endapo atashindwa, namuona (kama nilivyomuona Mchungaji Msigwa) Lissu akiondoka CHADEMA.