Nani anafadhili tamasha la Kizimkazi? Malengo yake ni yapi?

Nani anafadhili tamasha la Kizimkazi? Malengo yake ni yapi?

Weka ushahidi tuone. Acha kupayuka payuka hovyo🤣
Ushahidi ni huu: Samia atahudhuria tamasha akiwa na gari ya ikulu, wapamba wa ikulu, askari wa serikali, magari ya serikali na viongozi wa serikali!
 
Je kama hili Tamasha ni undercover ya kitu Fulani ?....ivi..
 
Hivi kwanini serikali isihamishe wale raia pale Kizimkazi tuwape wawekezaji lile eneo
 
Kiukweli kwa kule zanzibar kuna matamasha ya kiutamaduni maarafu na yote ni matamasha yapo east coast, huko east cost ndio unapata kizimkazi,makunduchi,paje,michamvi,jambiani n.k.

Kati ya hizi pwani za east coast, tamasha maarufu zaidi ni tamasha la makunduchi( nafikiri wenyewe wanaita tamasha la mwakatogwa" ) na ilo la kizimkazi ndio linaitwa "tamasha la kizimkazi".

Kwa zanzibar , watu wa east coast na makunduchi ndio wajanja wao, hata serikilani na viongozi mbalimbali wanatoka huko, kwahyo ili tamasha likifika viongozi mbalimbali wa serikali wanendaga huko kutambika na wao.

Matamasha haya yapo tangu enzi na enzi, mm niliwai kuishi zanzibar kwa miaka kama mitano hivi, kipindi cha hizi tamasha,nikweli harakati mbalimbali zinapungua mjini, na watu mbalimbali wanaelekea east coast kwenye hizi tamasha, sisi waswahili wapwani ya tanganyika matamasha kama haya yapo ila tunaitwa "madogoli", na hizi tamasha za east coast ya zanzibar ni mfano wako, ni tamasha la pure pure la kiasili.

Nafikiri Mama ni mtu wa kizimkazi, ndio maana hili tamasha this time limefanyiwa promotions sana sana.

N.B
Kwa zanzibar tamasha maarafu la kiasili ni lile la makunduchi na siyo ili la kizimkazi.
Na ile sauti za busara huwa ni nini ati!
 
Kula maisha kizimkazi! Unajipo baada y maokoto y bandari. Ila itakutokea puani. Ngoma mbichi hii
 
Back
Top Bottom