Kile kitabu ndo kinakuelekeza .Unafunga kula kadri unavyojisikia,unasali kwa imani.Na unamuachia Mungu yeye ndo atajibu maombi yako.Actually mt Rita alikuwa ni mtu wa Imani sana,yaani hata ambapo kibinadamu haiwezekani.Yeye maimbi yake kwa Mungu na Imani yake mambo yaliwezekana.Mfano mtu aliewahi olewa hairuhusiwi kuwa mtawa.Ila yeye alipofiwa na mmewe ,kisha na wanae.Aliomba kuwa mtawa kwenye shirika la mt Augustino ila aligonga mwamba.Aliendelea kumwomba Mungu ,na baadae akaenda tena kuomba kuwa mtawa hapo hapo alipokataliwa mwanzo.Baadae alikubaliwa.Yaani hii sala hii sala inakufanya kujenga imani kwa mambo magumu unayoyafanya ambayo kibinadaamu ni magumu,ila kwa Mungu yanawezekana na unatoboa kabisa.
N:B mimi si mkatoliki ila huwa ninasali novena mfano hii ya Rita,Antony wa Padua na nyingine nyingi.