Swali la msingi sana. Tunakatwa kodi kwenye kila huduma tunayofanya, tunalipa kodi za maeneo tunayoishi( Majengo), Tunalipa kodi kwenye usafiri, tunalipa kodi kwenye mishahara yetu (PAYE) tunalipa kodi kadha wa kadhaa...... jumlisha idadi ya watanzania na leo tunaambiwa eti only 2mill Tanzanians ndio wanaolila kodi lolKwahiyo kodi tunazotoa zaenda wapi
Sio kila mtu anaweza kuelewa hivi.Si ndio, hili jambo kamishina alishaliongea likaleta mjadala ila still naona bado halieleweki.
Hizi kodi za manunuzi kila mtu analipa, kila mtu si anafanya manunuzi? Mkurugenzi wa benki akinunua mkate si analipa kodi? Akiweka mafuta si analipa kodi? Ila akipokea mshahara anakatwa kodi ya mshahara. Sasa kodi inayoongelewa ni hii kodi ya mshahara.
Kwa ufupi anasema ajira ziongezeke, ujasiriamali uongezeke na ule usio rasmi urasimishwe.
Msikie huyu watu hawatumiwi pesa , unajifanya unaishi nje ya nchiNani anaekubali alipwe kwenye m pesa au Benki Ili akatwe? Hapo ni kama mtoa pesa Yuko mbali ,harafu kama hela ni nyingi hawamkubali ukazitoa chap Kwa mara Moja Benki ndio maana watu wanafanya miamala Kwa Fedha mbichi.
Bodaboda, mama ntilie, mawinga, fundi gereji, seremala, wakulima, wavuvi na wamachinga waanze kulipa direct tax.Raisi anaongelea direct tax, Indirect tax kila mtu analipa.
1. Je, ni Watanzania wangapi wanalipia LUKU ya umeme kuna kodi mle na kila siku tunalipa?
2. Tunaambiwa watumiaji wa simu tuko zaidi milioni 29 na kila siku unanunua vocha, tunalipia miamala?
3. Wangapi wanatumia magari yote yanalipiwa kodi na mafuta ukinunua unalipa kodi?
4. Tunalipa kodi tukilioia visimbuzi kila uchawi hiyo sio kodi?
5. Tunaonunua bidhaa kwa lipa namba, tunasafirisha bidhaa kutoka eneo moja hadi lingine bado tunalipa kodi
6. Mishahara yote nchini inakatwa kodi PAE.
NI UKWELI KUWA VAT na PAE tunalipa kila siku na kila mara
USSR
Pia soma:Rais Samia: Tunachokusanya hakiendani na idadi ya watu na shughuli za uchumi zilizopo. Pesa inaenda kwenye mifuko ya watu
1. Je, ni Watanzania wangapi wanalipia LUKU ya umeme kuna kodi mle na kila siku tunalipa?
2. Tunaambiwa watumiaji wa simu tuko zaidi milioni 29 na kila siku unanunua vocha, tunalipia miamala?
3. Wangapi wanatumia magari yote yanalipiwa kodi na mafuta ukinunua unalipa kodi?
4. Tunalipa kodi tukilioia visimbuzi kila uchawi hiyo sio kodi?
5. Tunaonunua bidhaa kwa lipa namba, tunasafirisha bidhaa kutoka eneo moja hadi lingine bado tunalipa kodi
6. Mishahara yote nchini inakatwa kodi PAE.
NI UKWELI KUWA VAT na PAE tunalipa kila siku na kila mara
USSR
Pia soma:Rais Samia: Tunachokusanya hakiendani na idadi ya watu na shughuli za uchumi zilizopo. Pesa inaenda kwenye mifuko ya watu
Mkuu, hii kodi huwa inahamia kwenye bei mpaka mtumiaji wa mwisho anailipia akinunua bidhaa hata asipopewa risiti.Kwa hapo anaehesabika ni mlipakodi ni producer sio wewe maana yeye ndio anauza Kwa whole sellers.
Wholesaler naye si alinunua akalipa hiyo kodi? Alichofanya ni kutaka mteja wake airudishe kwake.Whole sellers anaweza kukuuzia wewe na ukanunua ukijua umelipa.kodi.kumbe hapana.Bila risiti hakuna Kodi umelipa Mzee labda zile ambazo unaona directly kama Huduma za simu,Mafuta nk..
Ukidai risiti unamsababisha mwenye biashara alipe kodi halali ya mapato sababu mauzo yake yanakuwa wazi na pia unamfanya na yeye anapoagiza mzigo aombe risiti ili VAT isimuumize utakapomdai risiti hivyo supplier wake naye anajikuta hafichi mauzo and so on and so on. Risiti haihusiani na indirect tax za manunuzi, zile unalipa tu hata usipopewa risiti mkuu.Dai risiti ndio umelipa Kodi , otherwise Kuna producers wengi tuu kwenye informal sector hawalipi Kodi.
Tax base ni pamoja na wanaolipa indirect tax?Ukweli ni kwamba tax base ya Tanzania, effectively, ni ndogo sana. This is a fact, independent of all politics.
Ni kweli, binadamu huwezi jua mambo yote, kuna mambo tutayaelewa kuna mengine kunakuwa na ugumu kidogo mpaka tueleweshane.Sio kila mtu anaweza kuelewa hivi.
Population kubwa ya Watanzania ni watu tegemezi wasiozalisha kabisa, wanaozalisha kidogo sana na masikini hoehae, utapataje kodi kwa kundi kubwa la watu wa aina hiyo??Hizi indirect tax zinakuwa kubwa sababu direct tax zinalipwa na wachache mno. Watu M2 ni wachache mno, lazima bei za vitu ziwe juu kupitia indirect tax.
Mawinga hawatataka kurasimishwa.Bodaboda, mama ntilie, mawinga, fundi gereji, seremala, wakulima, wavuvi na wamachinga waanze kulipa direct tax.
Duh, ni kweli mkuu, sijui labda tubane matumizi, tupunguze ufisadi au kuufuta, ajira rasmi ziongezwe, mikopo kwa vijana waliorasimishwa iongezwe huenda tukapunguza tatizo.Population kubwa ya Watanzania ni watu tegemezi wasiozalisha kabisa, wanaozalisha kidogo sana na masikini hoehae, utapataje kodi kwa kundi kubwa la watu wa aina hiyo??
Ondoa ujinga wako hapa,Kama huna TIN ya Mapato wewe sio mlipakodi haijalishi unanunua bidhaa/Huduma au laa
Hiyo indirect tax wanaolipa wengi wanatumia huduma zaidi ya wanavyolipa kodi, so on balance wanakuwa net takers.Tax base ni pamoja na wanaolipa indirect tax?
Hata hivyo tatizo kubwa zaidi la Tanzania sio Tax base ndogo bali ni matumizi mabaya ya kodi na watawala.
Kukusanya kodi kubwa kwa walalahoi ni kuzidisha kiwango cha umasikini tu, muhimu zaidi ni kuzingatia matumizi ya kodi zenyewe.
Wewe shule ndio ulienda kusomea ujinga, Tozo ni kodi.Wacha upoyoyo, kuna kodi na kuna tozo.
Anayoiongelea Rais mama Samia ni kodi, unayoiongele wewe ni tozo.
Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
Kura Moja 🐼
Mawinga na bodaboda walipe direct tax/kodi ya moja kwa moja.Mkuu, kodi anayoongelea raisi ni kodi ya moja kwa moja itokanayo na shughuli zinazozalisha mapato.
Umefanya kazi au biashara ukapata ujira au faida kisha ule ujira au faida ukakatwa kodi.