Nani anamtumia Mwana FA juu ya ugonjwa wa Corona?

Nani anamtumia Mwana FA juu ya ugonjwa wa Corona?

Huyo Mwinjuma, FA or something like that ni idiot. Nimecheck, ni kweli ameandika huo upuuzi,anatumiwa na anapotosha watu. Ni kweli, hatupendi watu wapanic, lakini ni vizuri watu wakawa waangalifu i.e vigilant.

Ugonjwa ambao WHO wame u-designate Pandemic, yeye anasema eti kaugonjwa, sijui Malaria blah blah! Ugonjwa unaoweza kuua watu zaidi ya 500 kwa siku kwenye nchi yenye healthcare system nzuri kama Italy ni hatari.

Banana republic katika ubora wake.
 
Unaweza kusema corona sio hatari na ukajiona uko sahihi, lakini tukumbuke wengi waliokufa kwa corona ni wazee, na wenye matatizo ya kiafya yaliyosababisha kinga zao kua chini, hili ni kundi kubwa la watu tukiudharau corona inaweza kuwaondoa hao wote, na watu hao ni miongoni mwa jamii zetu, anaweza kua ni baba, mama,bibi, ndugu au rafiki, SIO UGONJWA WA KUPUUZA HATA KIDOGO

Sent using Jamii Forums mobile app
Mpumbavu huyo jamaa. Ni kweli vijana na watoto wengi wanaweza kupona huo ugonjwa, lakini miili ya watu iko tofauti tofauti na wengine pamoja na ujana wao hawataweza kuhimili, watakufa.

Lakini pia tuna wajibu wa kuwa waangalifu ili kulinda wale vulnerable, wazee na wenye underlying medical conditions, mfano kinga zimeshuka au tayari wana magonjwa mengine.
 
Nimeona na video ya ilo jinga. Lina sound bishoo fulani hivi! Limbukeni kabisa yaani.
Tafadhali jamani, kuweni waangalifu, kujilinda wenyewe na wazee wetu.
Puuzeni hilo dimwit.
 
Anaemtumia ametoka sasa hivi kufanya ka press ka ki K...

Hawa waache waendelee kumdhihaki Mungu.

All this is fkn staged... Wapumbavu.
 
Alizaliwa na seli nundu uyo mwana FA ndomana kapata corona kirahisi ana seli nundu uyo.

121.
 
Corona ni ndugu wa Ebola na kipindupindu zaidi hayo maralia yaweke pembeni
Corona inaenea kwa kasi tu ila effect kwenye vifo ni ndogo sana, usiichukulie poa malaria mkuu, jaribu kutafuta taarifa zake kwenye makala mbalimbali utaona hiyo corona haijafika hata robo ya vifo vitokanavyo na malaria

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwana FA haumwi Corona kaamua kuigiza tu ni kiki ya kishamba kaikosea kaja na Kiki pasipo kutafakari kuwa watanzania wa sasa wapo makini wanajua uigizaji wote
Ndio,huyu sio mgonjwa wa Corona.
Hii issue ni staged.
 
Shime shime watanzania wote tuungane kumshambulia FA kwa kujaribu kututoa kwenye njia. More than 3000 chinese died, 3000+ Italian died afu achia mbali kwingine huko France, USA, Africa afu yeye analeta sanaa kwenye ishu critical kama hii. Who sent this biachi mofo?
Jinga kabisa. Yaani limenikera mno.
 
Maelezo ya polepole yanamajibu san a kuliko yetu hapa, nadhani umegundua na nimewahi andika mahali kuwa, nchi inapaswa kujali Ustawi WA watu kwa mujibu WA katiba hivyo kwa mlipuko WA huu ugonjwa Ustawi wetu sasa ni afya kuliko uchumi kwani afya ndiyo mtaji WA uchumi na uchumi unatafutwa ukiwa na afya njema.

Serikali yetu inajali watalii, kuongeza pato LA taifa, kodi za ndege na uwanja na umwamba Mbele ya dunia kuwa corona siyo big issue in Tz zaid ya uchumi wetu it aka by oath Irina na ndiyo maana elimu haina tija kwa uchumi kama biashara .
Corona si big issue kama walivyo wapinzani hivyo serikali itaendelea na shughuli zake na wakati rais kaenda kujificha Dodoma huko Dar anaogopa corona.

Tutaona mengi mpaka corona iishe.

We Mungu tubariki tusife na kujieneza na corona....
Amin

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NANI ANAMTUMIA MWANA FA?

Na Thadei Ole Mushi

Mwana FA yupo Karantini au yupo nyumbani?

Wagonjwa wanaojulikana positive si wanawekwa Karantini chini ya uangalizi?

Mbona hajavaa Mask? Wanaomletea Chai, Chakula nk si atawaambukiza wote?

Je ni Nani anahusika kuvitangaza hivi visa? Ni wagonjwa wenyewe au Waziri? Naona Mwana FA na Meneja wa Diamond kashajitangaza wenyewe hata hivyo idadi ya walioambukizwa haikuongezeka au Hawa sio watanzania? Mbona Waziri haongezi idadi ya wagonjwa?

Anadai ametoka S.A juzi na video kaitoa Jana kwa maana hiyo juzi Ni jumanne ndio alirudi ila Jumapili alikuwa nchini kwa kuwa kwenye Uzinduzi wa albam ya Harmonize alikuwepo au tuseme aliondoka Jumapili na kurudi jumanne inawezekana ila angelituambi S.A alienda lini tungemwamini zaidi.

Kwa alichokipost baada ya hii video Ni kuwa malaria Ni hatari zaidi ya Corona kwa kuwa kapona. Kwa maneno haya tahadhari zote ambazo watu walikuwa wanazichukua wataacha kwa kuwa Ni ka ugonjwa kadogo na utapona tu kama yeye. Si tunajua huyu Ni celebrity hivyo vijana wengi watamuamini na kuacha kufuata kanuni za afya.

Nani anamtumia Mwana FA kupotosha jamii? Wizara ya Afya haioni upotoshaji huu wa wazi? Kwa Nini hawamkamati? Wanaomtumia kupotosha kwa nn wasimtumie kuwapa watu Elimu zaidi?

Serikali mbona haitoi tamko? Msanii mkubwa Kama huyu anasikilizwa na watu wengi je tufuate anayoyasema? Maswali Ni mengi kuliko majibu ila swali kuu linabakia Nani Anayemgumia na Kumtuma Mwana FA?

Tunavyozungumza hivi makamu wa pili wa Rais Burkinafaso ameshafariki kutokana na Corona. Mwana FA anatuambia hii ni vimafua tu?

Tuneona Ummy Mwalimu akimtakia kila la Kheri Mwana FA kuwa utavishinda tu hivi virusi mdogo wangu mbona Hao wengine sita wa awali hajawatakia salamu hii na Kheri hii? Nani anamtuma Mwana FA na Kwa malengo gani?

Ole Mushi
0712702602View attachment 1393727

Sent using Jamii Forums mobile app
Habari za Mwana FA tumeshaweka sana humu , ila ni basi tu watu hamkumbuki .
 
Ni kweli , US wameamua kutumia chroloqune kutibu corona
Bado mbona uelewi,hzo habari tunazijua kitambo sana kabla hata ww haujasimuliwa na Mwanahamisi Mwijuma ,ila bado na sio Chloroquine hile tuliyokuwa tunameza cc ni Chloroquine iliyoboreshwa.Na sio tu Chloroquine mpk ARv ikiboreshwa inatibu Corona kama unakumbuka yule jamaa wa kwanza mweusi kupona Corona ilitumika mchangaiko wa ARv.
 
Hawa Watanzania bana Watu wanakufa nyie mnasema hautishi yaani nyie mnataka kutisha lazima mtu akonde kama ukimwi?Uiengereza walianza kubisha watu wameanza kufa leo Uingereza wamefunga kilka kitu
 
Back
Top Bottom