Ambition plus
JF-Expert Member
- Feb 23, 2018
- 6,101
- 11,381
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Polepole hakukosea kuwafananisha!
Nimekuelewa!Ugonjwa Umetikisa Dunia na Umeua Watu Wengi Umeyumbisha Uchumi wa Mataifa makubwa Baadhi Wamefunga Mipaka yao..
Anatokea Mwana FA na kimwanya Chake anatoa maneno ya Kudharau Huu ugonjwa anasema eti haka KAUGONJWA HATA KASIWATISHE na hapo ana siku kadhaa hata hajawa Clear, Pumbaf zake.
Juzi ya wapi bwashee?!
Logic ya wengi wanaotilia shaka yako hapo. Mtu anasema ana Covid-19 lakini anarekodiwa akionesha dharau as if ugonjwa anaoongelea ni sawa na kidonda cha kujikata na wembe?Nimekuelewa!
Muache ajipambanue na mwanya wake kama mlango wa noah. Siku akiukwaa kisawasawa ndo atajua Mungu haimbi hip-hop wala bongo flaver. Watu wako serious na dunia imesimama kwasababu ya corona yeye anaibuka na kusema bora malaria. Wazungu wamekosa ALU au Paracetamol?
Umewakosea Mama zetuKila mtu ana uwezo wake wa kuchanganua jambo na kuamua kuliamini au kutoliamini..
Sasa unataka kila unaloliamini wewe ndio kila mtu aliamini..?
Wee Mama vipi wewe..!?
Sijaelewa kwanini watanzania wamekuwa wagumu kumuamini Mwana FA kwamba ana maambukizi ya Corona aliyoyapata Afrika kusini.
Mbona Aurlus Mabere hatunaye kwa sababu ya Corona?
Mbona Mano Dibango naye amepata maambukizi ya Corona!
Hata mimi awali sikuamini lakini baada ya kufuatilia mambo yanayoendelea Afrika kwa sasa ambapo kuna vifo zaidi ya 16 vya Corona sitabisha tena mtu akisema ana maambukizi maana watu wameanza " kuvuta" pamoja na joto lote mfano kule Misri!
Niishie hapo!
*MWANAMZIKI NGULI AURLUS MABELE AFARIKI DUNIA*
Aurlus mabere kafa kwa magonjwa mengine, na alikuwa anaumwa kabla corona haijaingia France.
Usimsingizie
Ndiyo maana tunasema recruitment ya idara hii nyeti ni mbovu, na haitakaa ifanye mapinduzi makubwa ya kijasusi na uchumi wa kidola kama walivyofanikiwa Mossad, MI6, CIA n.kMwanaFA ni kipepeo wa kitengo, msisahau hilo.
Na mm juzi nilikutana nae sea cliffKwa Salam nimeamini ila kwa Mwana F.A. nadhani anatumika.Kwa sababu kwenye show ya Harmonize alikuwepo sasa hiyo south kaenda lini?
Sent using Jamii Forums mobile app
Ahsante sana mkuu!*MWANAMZIKI NGULI AURLUS MABELE AFARIKI DUNIA*
Mwanamuziki wa miondoko ya Soukous Aurlus Mabele amefariki dunia nchini Ufaransa akiwa na miaka 67.
Kwa mujibu wa rafiki yake wa karibu Nyboma Mwandido amethibitisha Aurlus Mabele kufariki dunia, huku taarifa zikieleza kuwa nguli huyo wa miondoko ya Soukous alifariki usiku wa kuamkia Ijumaa Machi 20, 2020 baada ya kuugua ugonjwa wa kiharusi kwa muda mrefu na hivi karibunia alipata maambukizi ya virusi vya corona.
Taarifa zaidi zimeeleza kuwa mwanamuziki huyo pia alikuwa akisumbuliwa kwa ugonjwa wa saratani ya koo, kwa miaka mingi, kabla ya kupata maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa corona.
Ugonjwa huo ambao ulianzia Wuhan nchini China na kusambaa katika nchi mbalimbali duniani, umeua zaidi ya watu 371 nchini Ufaransa.
Aurlus Mabele Alizaliwa mnamo mwaka wa 1953 huko Kongo-Brazzaville katika wilaya ya Poto-Poto nchini Jamhuri ya Kongo alifariki tarehe 20 March 2020.
Jina lake halisi ni Aurélien Miatsonama. Alianzisha kundi liitwalo "Ndimbola Lokole".
Mabele alikuwa mmoja ya waanzilishi na lijendi aliyewahi kuanzisha kundi la Loketo akiwa na wanamuziki wenzake nguli kama Mav Cacharel na Diblo Dibala miaka ya 1980 japo baadae kundi lao lilivunjika.
Mabele akiwa na Mav Cacharel na Diblo Dibala walitengeneza muziki maarufu wa soukous ambapo baadaye akatajwa kama mfalme, na kupelekea msemo wa kuwa "Aurlus Mabele ndiye mfalme wa soukous".
Mabele alikuwa ni msanii pekee aliyeweka makazi yake jijini Paris Ufaransa na kutamba katika miaka ya 1980 akitumia santuri.
Mabele pia aliwahi kutamba na nyimbo zake maarufu kama Embargo, Liste Rouge.
Katika miaka 25 ya kazi zake ameuza zaidi ya nakala milioni 10 za albamu dunia nzima na alisaidia kwa kiasi kikubwa katika kuitambulisha na kuisukuma vilivyo muziki wa soukous nje ya mipaka ya bara la Afrika.
Alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kupooza kwa miaka mitano, lakini aliweza kujipanga ili kufanya matamasha na kundi zima la Loketo huko Ulaya kati ya mwezi Mei na Juni, 2009.
Kwa kushirikiana na wapiga magitaa maarufu na wenye vipaji, alitengeneza dansi ya Kiafrika yenye ladha yake ya kipekee ya soukous kwa kutunga nyimbo kama vile Mousso Africa, Ivorian woman, Embargo, Betty De Asta, Evelyne, Loketo na kadhalika.
Sent using Jamii Forums mobile app