Nani ananunua gazeti siku hizi? Hakuna umuhimu tena

Nani ananunua gazeti siku hizi? Hakuna umuhimu tena

Elvis Legacy

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2017
Posts
3,984
Reaction score
5,820
Habari wakuu.Miaka ya nyuma kidogo tulisoma magazeti, tena kila habari kuanzia za siasa michezo hadi vibonzo bila kusahau matangazo.

Nakumbuka miaka ile, mzee alikuwa akija na magazeti ya Nipashe, Majira na Mwananchi kila alipotoka kwenye mihangaiko. Hii ilitujengea hamasa ya kupenda kusoma tukiwa nyumbani, maana, Magazeti ndio yalikuwa na mambo mapya tofauti na vitabu vya hadithi ambavyo tulivosoma na kuvirudia mpaka tukavichoka.

Siku hizi watoto wa familia nyingi hawana tena desturi ya kusoma magazeti maana wazazi hawana utamaduni wa kununua na kuyapeleka nyumbani, hata vijana wa leo wengi hatusomi magazeti wala hatuna source yoyote ya hard news ambazo tunasoma kila siku. Badala yake tumejikita zaidi na taarifa za kwenye social media ambazo hazijahaririwa wala hazina hata chanzo makini cha habari husika. Baada ya hapo tunapitia 'comments' na kujadili kila mtu kulingana na alivyoielewa au anavyotafsiri kama apendavyo.

Je hili jambo lina afya kwa kizazi kijacho? Sijaangazia kusikiliza taarifa ya habari ambapo zamani kulipewa umuhimu kwenye runinga za majumbani. Ndio kusema magazeti, redio na runinga zimepitwa na wakati. Cha kushangaza bado miswada ya sheria na matangazo muhimu ya serikali yanapatikana kwenye magazeti. Nini kifanyike?
gazeti.jpg
 
Kuna magazeti yanadoda mezani pa wauza magazeti mitaani, wanauza nakala chache sana na megine hayauziki kabisa. Zipo kampuni za magazeti zimekufa, zimeacha uzalishaji na zingine zinaishi kwa ruzuku tu huku zingine zikijikongoja. Automatically magazeti yamesukumwa mbali na mitandao ya kijamii inayoleta habari kwa haraka. Anyway makampuni mengine yameamua kula sahani moja na mitandao hayajakata tamaa yapo yako hoi
 
Magazeti bado kuna sehemu yanauzika sana tuu ila sio kama zamani...
Sehemu za maofisini hua wananunua magazeti, Maktaba kuu na za mikoa hununua na huweka kumbukumbu, pia kuna wakandarasi nao hununua ili kuangalia tender mbalimbali za Serikali
 
Kabla ya kuja kwa mitandao ya kijamii nilikuwa najaza kilo tatu za magazeti kwa mwezi kwa ajili ya kujisomea tu, kisha nayauza madukani kufungia bidhaa. Mpaka sasa nina salfeti limejaa magazeti yaliyotoka miaka kumi iliyopita, nimeyaweka kwenye library yangu ndogo kama kumbukumbu, pamoja na kuwepo mitandao huwa nanunua magazeti mara moja moja sana lakini si kama zamani naweza kunununua magazeti ya shilingi elfu tatu kwa bei ya shilingi mia tano kwa nakala moja. Bado kuna magazeti yanauzwa shilingi mia tano lakini sina munkari wa kununua nakala zisizozidi mbili. Bajeti ya kununua magazeti imehamia kwenye kununua bando la intaneti
 
Hali ni mbaya sana.. tatizo hakuna hamasa ya siasa! Siasa ndiyo ilikuwa inahamasisha usonaji wa magazeti. Makao Makuu ya Mkoa wa Manyara BABATI...kijiwe cha Magazeti ni kimoja tu! Muuzaji aliniambia hauzi nakala zaidi ya 100 Kwa siku!
Sasa kama Babati hali ndiyo hiyo huko Mbulu itakuwaje!
 
Kila kitu uja na faida na hasara teknolojia ina faida na hasara kwa sasa mitandao ya kijamii ndio uleta habari kwa haraka mchawi ni bando lako tu

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
 
Napita kila siku kuangalia vichwa vya habari tuu, simu imebeba zaidi ya gazeti
 
Magazeti walijisahau sana. uwepo wa mitandao umetuokoa wengi.
Ilifikia kipindi Dr Mwakyembe akiwa Waziri alipiga marufuku vituo vya redio kusoma taarifa za magazeti kwa urefu. Lengo ni msikilizaji akanunue gazeti. Marufuku hii haikuleta tija ktk soko la magazeti. Hali mbaya.
 
Kizazi çha sasa hakina utamaduni wa kusoma.

Nakumbuka kipindi kile magazeti ka Mzalendo ,Mfanyakazi ,Sunday News nk ilikuwa ni kawaida kuyakuta home.
 
Kizazi çha sasa hakina utamaduni wa kusoma.

Nakumbuka kipindi kile magazeti ka Mzalendo ,Mfanyakazi ,Sunday News nk ilikuwa ni kawaida kuyakuta home.
Hata mbinyo wa Jiwe Kwa vyombo vya habari ulichangia ...Kila gazeti lilikuwa linaandika kusifu na kutukutuza watu eakaona upuuzi kununua magazeti
 
Kuna magazeti yanadoda mezani pa wauza magazeti mitaani, wanauza nakala chache sana na megine hayauziki kabisa. Zipo kampuni za magazeti zimekufa, zimeacha uzalishaji na zingine zinaishi kwa ruzuku tu huku zingine zikijikongoja. Automatically magazeti yamesukumwa mbali na mitandao ya kijamii inayoleta habari kwa haraka. Anyway makampuni mengine yameamua kula sahani moja na mitandao hayajakata tamaa yapo yako hoi
Upo sahihi mkuu ila taarifa za mitandaoni mara nyingi huwa hazijitoshelezi, ukiingia YouTube kila mtu ni mwandishi na wanalenga zaidi kupata followers na likes kuliko hifikisha taarifa sahihi kwenye jamii.

Ni bora magazeti ambayo yamehamia kidigitali unaweza ukapata taarifa kwa kina. Japo usomaji wa kwenye simu ni tofauti na hard copy.
 
Kizazi çha sasa hakina utamaduni wa kusoma.

Nakumbuka kipindi kile magazeti ka Mzalendo ,Mfanyakazi ,Sunday News nk ilikuwa ni kawaida kuyakuta home.
Hapo umegusa penyewe mkuu. Siku hizi watu wanapenda kusikia zaidi kuliko kusoma.
Maarifa mengi yamefichwa kwenye maandishi lakini wengi hatupendi kusoma.
 
Zamani mzee alikuwa akishamaliza kusoma mambo yake mi nilikuwa nayanyakua kwaajili ya kusoma katuni, hakika zilikuwa zinafurahisha sana.
Nakumbuka tukiwa boarding school tulikuwa tunachanga hela kununua gazeti la sani ili kusoma vibonzo vya kina madenge, baba ubaya, sokomoko, ndumilakuwili n.k
 
Hapo umegusa penyewe mkuu. Siku hizi watu wanapenda kusikia zaidi kuliko kusoma.
Maarifa mengi yamefichwa kwenye maandishi lakini wengi hatupendi kusoma.
Sasa utaingia JF ili usikie nini wakati huku tunasoma?

Hard copy zimeshapitwa na wakati, Mimi gazeti la Mwana nchi nalisoma kila siku kwenye soft copy.
 
Shigongo alijua kuvuna pesa zetu na hadithi zake za uongo na kweli, kipindi kile magazeti ya udaku sh 100.

Jumatatu - champion
Jumanne - Uwazi
Jumatano nimesahau jina
Alhamisi - amani
Ijumaa - Ijumaa na Kiu
 
Back
Top Bottom