Nani anaweza kutupa historia ya pesa?

Wakuu topic bado inaendelea karibuni
 
Karibuni wakuu ngoma inaendelea
 
Karibuni kaeibuni. Mwenye wazo jipya aliweke mezani. Wote tunataka kujifunza
 
Pesa ni makaratasi hasara roho...

Japo maisha siyo kutesa kila siku, ila pesa ndiyo kila kitu...
 
Nielewavyo mimi

Hapo mwanzo watu walibadilishana bidhaa kwa bidhaa yaani Maharagwe kwa Mchele ama ngano kwa Chumvi au vyovyote vile walivyoona ni mabadilishano ya haki.

Hali hii ilikwenda mpaka pale likawajia wazo la kuwa na kipimo cha ubadilishaji huo wa bidhaa, Wakaja na Dhahabu ikiwa ni kitu cha thamani miongoni mwa jamii zote.
Hivyo ikawa kama unahitaji bidhaa ni lazima uwe na dhahabu ili kuipata bidhaa unayoihitaji. Mfano: Dhahabu kwa Mchele, na Dhahabu kwa Chumvi.

Hii pia ikaenda mpaka walipokuja watu wa Benki (Bankers), hawa walikua ni wafanyabiashara ambao walikua na mitaji mikubwa ambapo walikua wakiwakopesha wafanyabiashara wengine na walilipwa kwa Riba.
Hawa walikua na hifadhi kubwa ya dhahabu, likaja wazo la kuliko watu kutembea na midhahabu kila pahala ni vyema waweke dhahabu sehemu fulani (kwa Bankers) kisha wataipata muda wowote watakapoihitaji.
Ili kuhakikisha kila muwekaji dhahabu anatambulika na kupewa kiasi sahihi alichoweka watu wa Benki wakawa wanatoa 'kikaratasi' (Bank Note) kwa kila mwenye dhahabu yake. Hivyo ikiwa unahitaji bidhaa fulani wewe unatembea na 'kikaratasi' (ambacho kinawakilisha kiasi fulani cha dhahabu) mpaka kwa muuzaji na kumkabidhi, nae atakukabidhi bidhaa inayoendana na kiasi cha dhahabu inayowakilishwa kwenye 'kikaratasi' Ikawa 'kikaratasi' kwa Mchele na 'kikaratasi' kwa Chumvi.

Wauzaji bidhaa walipokea 'kikaratasi' na kwenda Benki kuchukua dhahabu yenye thamani sawa na iliyowakilishwa kwenye 'kikaratasi'. Hapa Benki ndizo zikawa na Pesa Halisi yaani Dhahabu na madini ya fedha na wengine wakiwa na 'kikaratasi' tu.
Mfumo wa 'kikaratasi' ulikumbwa na matatizo mengi ikiwemo kughushi, lakini utatuzi ulipatikana kwa kuboresha utengenezaji wake.

Miaka ya hivi karibuni zikazuka pesa za mitandaoni yaani Bitcoin na Cryptocurrencies nyingine.
Mtindo ni uleule yaani kunakuwa na kiwango fulani kwenye mzunguko ambacho kinatumika kwa mabadilishano ya bidhaa au huduma baina ya watu.

Naamini utakuwa umepata Mwangaza...

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Unaweza kutuambia udanganyifu unaoweza kufanyika kwenye huu mfumo. Na nani anafaidika kwenye huo mfumo wa kidunia wafedha. Na kama anafaidika je, ni kwa njia ya haki au sio. Na kama anafaidika kwa njia ya utapeli nani wa kimsimamia. Je kuna taasisi zinazosimamia haki kwenye fraud zozote. Na kama zipo nani anaezisimamia kama zimesimamia vizuri. Je ni swala ambalo liko kiimani zaidi kwamba tuamini tu mfumo upo safe na hamna udanganyifu au limekaa ki fact. Kwamba kama udanganyifu ukitokea basi automatically mtu anakamatwa.
Pia unaweza elezea kwann italy ilikua na covid 19 kali kabisa kuliko nchi zote na bado thamani yao ya hela ikaendelea kua ile ile? Tulitegemea thamani ya hela ipungue kwa sababu uzalishaji wao ulishuka..( nanukuu kutoka kwenye principle za currency inavopaswa kufanya kazi).
Ukiweza kunijibu hayo maswali then utakua umetoa watu wengi sana kwenye kiza. Lakini nilipenda uwe honest kwenye majibu yako
 
Nitajibu kadri nilivyojaaliwa uelewa juu ya hili suala..
Tukianza na Udanganyifu unaoweza kufanyika katika mfumo huu wa fedha,
Ndio, kuna mapengo mengi sana yanayotoa fursa kwa watu wenye nia Ovu kufanya udanganyifu na kujiingizia kipato kwa njia zisizo za halali.
Mathalani, Katika ngazi za kibenki watu wanaweza kughushi cheki na sahihi za wamiliki wa akaunti, au kwa kuongeza idadi ya sifuri zilizoandikwa kwenye cheki husika.

Katika ngazi ya benki pia Kampuni inaweza kughushi nyaraka zake za mapato na matumizi kuonyesha kuwa kampuni inatengeneza faida kubwa hali ya kuwa ni kinyume chake, Kughushi huku kunatumika kupata Imani ya Benki ya kukopeshwa kiasi kikubwa cha fedha.

Kimsingi katika Udanganyifu njia zinazotumika ziko nyingi sana, Si rahisi kuziandika zote hapa.


Kuhusu nani anafaidika;
Kwa maono yangu afaidikae na mfumo huu ni Marekani, Pesa yake yaani Dola ndiyo inayotumika na kuaminika zaidi katika miamala mingi ya kibiashara Ulimwenguni. Inakadiriwa asilimia 70 za miamala ya kifedha ifanyikayo Duniani huhusisha Dola ya Marekani kama fedha ya mabadilishano.

Hali hii huifanya Dola ya Marekani kuwa na Uhitaji Mkubwa sana hivyo Marekani inachapisha Dola nyingi sana kwaajili ya kutimiza mahitaji yake ya ndani na ya kidunia.

Marekani anafaidika kwa kuwa Wananchi wake wananunua bidhaa toka nje kwa bei rahisi sana kuliko watu wengine duniani, hii ni kwa sababu Wamarekani hawahitaji kuibadilisha Dola yao ili kufanya miamala baki wao wanaitumia kama ilivyo na kununua bidhaa nje kwa wingi huku wakilipa kidogo.

Kwa kuongezea Marekani inalipwa na Mataifa mengine ili kuwauzia Dola, yaani Mfano, Kuwait inahitaji Dola 8000 za Kimarekani hawana namna nyingine ya kuzipata ila kwa kwenda Marekani na kulipa (aidha kwa dhahabu au mafuta, au kwa kingine chochote watakachoelewana) na kupewa hizo Dola 8000 ambazo wao watatumia kufanya Miamala ya kibiashara na Nchi nyingine.

Uhalali au Uharamu wa Marekani kufaidika na mfumo huu inategemea na Mtazamo, hivyo nisingependa kulijadili hili.

Kuhusu Chombo kinachosimamia Ubadhilifu katika mfumo wa fedha:
Hakuna chombo kimoja cha kimataifa kinachoshughulika na hili, bali kila nchi ina sheria zake zinazojaribu kuziba mianya ya kufanya aina yoyote ya Ubadhilifu kwa kuifanya kuwa kinyume cha Sheria. Mfano Tanzania tuna TAKUKURU na POLISI ambavyo vinashughulika na kesi zote zinazojihusisha na Uhujumu wa Mfumo huu wa Fedha kama Utapeli Benki uloelezewa hapo juu.
Lakini pia kuna INTERPOL ambayo inajitahidi kushughulikia baadhi ya kesi zinazohusishwa na Ubadhilifu wa Fedha.

Kesi ya Italia;
Italia Iliathiriwa sana na janga la Corona, ilitarajiwa kuona Sarafu yake inashuka thamani, Ni kweli.
Kupanda na kushuka kwa thamani ya Sarafu ya nchi fulani hutegemea sana na Uhitaji wa Sarafu hiyo katika Miamala ya Kifedha.
Uhitaji huo huenda sambamba na masuala ya Uwekezaji na Biashara na nchi za kigeni. Vyote hivi vilishuka wakati wa janga la Korona nchini Italia.

Ni Muhimu kuzingatia ya kuwa Italia ni moja ya nchi ya Ulaya iliyogubikwa na madeni makubwa sana ikiwa pamoja na Ugiriki, ni sawa na kusema ina Uchumi goigoi ukilinganisha na nchi nyingine za Ulaya Magharibi.

Ifahamike kuwa Italia ilikuwa ikitumia Sarafu yake ya Lira lakini iliacha mwaka 1999 na kuanza kutumia Euro, hivyo hapa tunaizungumzia Athari zilizoikumba Euro wakati wa Korona.


Kwanini thamani yake haikutetereka sana?
Korona iliiathiri sana Italia na kupelekea kushuka kwa Uwekezaji nchini humo, kufungwa kwa Biashara na kushuka kwa Uzalishaji ambao ungepelekea Ongezeko la Biashara za kigeni yaani Exports.

Uimara wa Sarafu ya Euro hautegemei Uchumi wa Italia pekee yake, kwakuwa Euro inatumika na nchi nyingi za Ulaya hivyo mambo yanayochanganua Kupanda na kushuka kwa thamani yake hutegemea na nchi zote zinazotumia Euro.

Nchi kama Ujerumani ambayo haikuathiriwa sana ukilinganisha na Italia na Uhispania ndio zilizoiokoa Euro kutoshuka thamani, kwakuwa Vitega Uchumi vya nchi zingine za Ulaya havikuathiriwa sana kupelekea kushuka kwa thamani ya Euro.





Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Kwa maelezo yako in summary

1. Kuna nchi wanaweza chapisha hela bila kuulizwa. na wananchi wake wanaishi kama maboss wa dunia sababu hela yao haipatikani kwa jasho. Ina printiwa tu

2. Italia hata kama corona ingepiga milele na wananchi wakakaa bila kufanya kazi. Euro isingeshuka wala lira kwa sababu ile ile, wanauwezo wa kucheza na thamani ya pesa kwenye computer(exchange rate). Ila afrika kwa sababu hatumiliki wala hatutumii hiyo michezo ya computer. sisi hela yetu inashuka thamani
 

Hapana, hayo siyo nlomaanisha Mkuu.

Hakuna nchi wanaprint tu pesa bila kuwa na mnyororo wa ufanyaji kazi, ikitokea wakafanya hivyo watakumbwa na tatizo liitwalo 'Inflation' ambapo thamani ya sarafu hushuka mara dufu dhidi ya sarafu yoyote ya kigeni, Mfano Zimbabwe wakati wa Mugabe walifanya hivyo kujikwamua toka kwenye vikwazo.

Kama Italia wangelikua wanatumia Lira wakati wa korona si ajabu tungeona Lira ikiporomoka.
Mfano Uchina ni Taifa la kwanza kuathiriwa na Korona na kwa miezi ya awali thamani ya sarafu yake ya Yen ilishuka sana lakini baadae ikapanda kutokana na kwamba waliweza kuuudhibiti ugonjwa na kurudisha imani kwa Wafanyabiashara na Wawekezaji.

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
We unaongelea country economy. On country level ndo huwa kuna inflation. Lakini on global level futa hicho kitu. Ni ngumu sana kugundua inflation on global level sababu nchi tofauti na marekani zinatumia currency nyingine. Lakini zote ziko backed up by dollar.
We mwenyewe kwenye maelezo yako ya kwanza umekubali kua fraud inaweza tokea kwenye kuprint na mtu asijue.
Afu kumbuka unapoongelea global economy usichanganye na state economy. Dollar is global. But tsh is country wise.
Unachanganya sana mkuu. Sikulaumu kwa sababu elimu yetu ya kibongo ndo imetulazimisha tukariri hivo.
Ina maana kwa maelezo yako unataka kusema mfumo uko safe. Hata gadafi alikosea kuja na currency ya africa? Mmh. Kua honest mkuu acha kuji contradict.
 
Alafu issue ya zimbabwe sio ya kutolea mfano. Ingekua ni taifa kubwa example "us" limefanya kitu alichokolifanya mugabe wala usingesikia hiyo kesi. Hakuna nchi inayodiriki kulikagua linchi kama marekaji hata kama lime cheat.
So mfano wa zimbabwe ungeuacha tu
 
Alafu unaweza kuniambia nani alikua anamonitor thamani ya pesa ya china. Kushusha hadi kupanda tena. Dont tell mi kwamba ni automatic process inatokea mbinguni.
As long as binadamu yupo in control bado mfumo hauko safe. Believe mi or not
 
Mkuu leo hii hata nchi kama Ujerumani (ingelikua inatumia sarafu yake peke yake mbali na Euro) ikizalisha fedha nyingi na kuziingiza kwenye mzunguko kesi itakuwa ileile sawa na ya Zimbabwe (Inflation).
Kwa Marekani ni exception kwakuwa Fedha yake inatumika ulimwenguni kote, lakini pamoja na hilo wanaizalisha kwa kuzingatia uhitaji endapo wakizidisha kuliko uhitaji hatma yake itakua kama ile ya Zimbabwe tu, hii kitu iko fixed.
Kesi kama hiyo iliikuta Hungary miaka ya 1940 na iliyokua Yugoslavia miaka ya 90s.

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Alafu unaweza kuniambia nani alikua anamonitor thamani ya pesa ya china. Kushusha hadi kupanda tena. Dont tell mi kwamba ni automatic process inatokea mbinguni.
As long as binadamu yupo in control bado mfumo hauko safe. Believe mi or not
Kikanuni, thamani ya Sarafu ya nchi fulani hutegemea uhitaji wa sarafu hiyo, ambapo huenda sambamba na ufanyaji biashara na uwekezaji.

Miezi ya mwanzo ilipozuka korona Safaru ya Uchina ilitetereka kutokana na kwamba Biashara ilipungua (uzalishaji ulishuka) huku uwekezaji ukidorora hivyo AUTOMATICALLY Sarafu ilishuka thamani.

Lakini wao waliweza kuudhibiti mapema ugonjwa wa Korona hivyo kurudisha imani kwa Wawekezaji, Wazalishaji na Wafanyabiashara jambo ambalo lilisisimua ongezeko la uhitaji wa sarafu ya Uchina, hivyo AUTOMATICALLY ikapanda tena thamani.

Au waweza tueleza ni nani ana udhibiti wa kupanda na kushuka thamani kwa sarafu ya Uchina?

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
mkuu unaongelea state economy, mi naongelea global economy, don't sleep on germany, germany haiwezi kua na inflation, sio nchi ya afrika hiyo, hiyo ni nchi ya ulaya ambayo wana Umoja mkali sana, alafu tambua nchi ya ulaya haiwezi kupata inflation kwa sababu pesa yao ina rotate kama dollar dunia nzima, so its their fiat money against the world( ni kama una print pesa na kuiweka kwenye uchumi wa dunia, hii ni tofauti na kuprint hela na kuiweka kwenye uchumi wa nchi yako), lakini issue ya Mugabe ilikua ni kwamba pesa aliyoprint aliwekewa sunction na restriction kufanya biashara pia ikashushwa thamani kwa reference ya dollar. so alishindwa kufanya biashara hata na nchi zake za afrika, ila afrika ingekua na Umoja sanction isingekua inamadhara yoyote, ila kwa sababu nchi za ulaya zina Umoja, ndo maana hakuna kitu kwao kina itwa sunction kwa sababu wakifanya hivo wanakua wanajipiga pini wenyewe
 
Kama sijakosea...
Umemaanisha Umoja wa Ulaya hata wakichapisha pesa nyingi kushinda Uhitaji hawawez pata Hyperinflation?

Na Marekani vivyo hivyo?

Nijuze kama nimekosea kukuelewa

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…