Nani atufumbue kuhusu hawa wahindi na waarabu juu ya wanachokifanya huku mitaani

ukiwa maskini kuna sadaka huwez kuzijua jitahidi uwe na hela ujue kujitoa kwa wenye uhitaji upo mtaa wanagawa mpka hela ww kulishwa ndo unashangaa
 
SI mtaani kwetu kondoo 200 walichinjwa.kuna jamaa mlevi anaaitwa j akachukua nyama ili aende kuuza ghafla akagongwa na Noah akafa hapohapo
 
Miaka kumi iliyopita hao watu wiokuwa wakikarimu watu Moshi, Bomang'ombe na Arusha walikamatwa kwa ugaidi na kwa ufahamu wangu na maneno ya Sheikh Ponda kuwa mpaka leo hawaja achiwa na hawajawahi kufikishwa mahakamani
 
Mtaa gani huo nipite kesho?
 
Nilitoka Morogoro mwaka huu mwanzoni mwezi wa 4 Kuja Moshi mjini kutokana na masuala ya kifamilia,

Nifupishe mada kilichonistajabisha ni kwamba kila ipokua inafika jioni majira ya saa kumi na nusu muda wa Azana, niliona kundi kubwa la watoto na watu wazima wachache wakiongozana kuelekea katika jumba moja ambamo walidai walikua wakipikiwa chakula Aina ya wali, pilau kwa maharagwe na kila siku mbili katika week walichichinjwa mbuzi, hivyo kila week mbuzi 2.

Na kwa makadirio mchele ulikua sio chini ya kg50 kila siku na nilipojaribu kuwauliza zoezi hili limeanza lini na linaisha lini? walidai limeanza baada ya mfungo kwisha na litaishia mwezi wa kumi na mbili du! Nilibaki mdomo wazi, kwakua ni kitu ambacho sijawaiona wala kusikia sadaka ya kulisha watu kwa miezi yote hii na nikiwa Moshi niliuza watu kadha hawakuweza nipa majibu sahihi na hata nilipokwenda Many Ara na Arusha pia sikupata majibu husika, mwenye kujua hii kitu kiundani atufungue tafadhali.

Maswali yangu ni kama haya;
1. Lengo la kupika na kuchinja na kulisha watu kila siku isipokua juma pili ni nini?
2. Je Kuna madhara yoyote kwa wanaokwenda kushiriki kula chakula icho?
3. Ni upi salama wa chakula, mamlaka za serikali zinashiriki kupima ubora wa chakula?
4. Je hii umeshawai kuishuhudia mtaani kwenu?
5. Je hamna Imani za kishirikina zinazoambatana na zoezi hilo hasa kwenye kuchinja mnyama?
wahindi ns waarabu wameiningaje hapo?
 
Miaka kumi iliyopita hao watu wiokuwa wakikarimu watu Moshi, Bomang'ombe na Arusha walikamatwa kwa ugaidi na kwa ufahamu wangu na maneno ya Sheikh Ponda kuwa mpaka leo hawaja achiwa na hawajawahi kufikishwa mahakamani

Aisee, mama afanye kila namna awatoe hawa ndugu zetu.
 
Naunga mkono ya Kalunya!
Kama matajiri wangetimiza wajibu wao wa Kuwalisha Masikini kama walivyo elekezwa kwenye Quran; hakungekuwa na masikini wa kulala njaa. Dunia ya sasa imejaa Ubinafsi na unafiki; wengine wanakula na kusaza huku jirani yake anakufa kwa njaa/hawezi hata kusomesha mtoto shule ya kata. Anza kuangalia ndugu zako au hapo mtaani kwako, ni wangapi hawana hata uhakika wa kupata mlo wa siku? na wewe unajiita muumini unayesubiri siku ya mwisho/hukumu; Kumbuka Pepo hutafutwa huku duniani, huko mbinguni ni hesabu tu
Mimi natamani ningeweza, kutengeneza sehemu kama hiyo nijenge na Shule/Veta wapate Elimu Bure kabisa!!!
Huku JF sometimes you may find mtu kapata like hata 50 kwa point ya kijinga tu isiyokuwa na maana au thread ya kipumbavu tu lakini subscribers hao lakini point ya msingi kama hii au thread yenye umaana mkubwa ni very reverse
 
SI mtaani kwetu kondoo 200 walichinjwa.kuna jamaa mlevi anaaitwa j akachukua nyama ili aende kuuza ghafla akagongwa na Noah akafa hapohapo
Hapo mkuu kuna nadharia 2, ila zote ni sawa , ya 1 hyo ni ajari kama ajari zingine na ahadi yake isha fika , ya 2 na kubwa ni kuwa ALLAH alichukia kitendo cha yeye kudhurumu, na hii ni ahadi ya ALLAH kuwa hujibu kwa haraka dua za yatima na anaye dhurumiwa , sasa hyo mwamba alimjaribu mungu, hv unajisikiache kudhurumu chakula cha maskini ?, sasa mtu 1 tena kaacha kununua chakula eti kaenda kuelewea kisha anakuja kuchukua chakula cha wasio jiweza , huo sio uchawi , hyo ni ALLAH
 
Ni sadaka kama sadaka zingine japokuwa wapo wanaofanya na mambo yao ya ajabu.
Ila sie kila baada ya miezi 3, sikukuu au mwezi mtukufu huwa tunachinja ng'ombe 3 hadi 6 kwa ajili ya sadaka. Pamoja na kutoa mchele, maharagwe, unga wa ngano pamoja na sukari.
 
Nilitoka Morogoro mwaka huu mwanzoni mwezi wa 4 Kuja Moshi mjini kutokana na masuala ya kifamilia,

Nifupishe mada kilichonistajabisha ni kwamba kila ipokua inafika jioni majira ya saa kumi na nusu muda wa Azana, niliona kundi kubwa la watoto na watu wazima wachache wakiongozana kuelekea katika jumba moja ambamo walidai walikua wakipikiwa chakula Aina ya wali, pilau kwa maharagwe na kila siku mbili katika week walichichinjwa mbuzi, hivyo kila week mbuzi 2.

Na kwa makadirio mchele ulikua sio chini ya kg50 kila siku na nilipojaribu kuwauliza zoezi hili limeanza lini na linaisha lini? walidai limeanza baada ya mfungo kwisha na litaishia mwezi wa kumi na mbili du! Nilibaki mdomo wazi, kwakua ni kitu ambacho sijawaiona wala kusikia sadaka ya kulisha watu kwa miezi yote hii na nikiwa Moshi niliuza watu kadha hawakuweza nipa majibu sahihi na hata nilipokwenda Many Ara na Arusha pia sikupata majibu husika, mwenye kujua hii kitu kiundani atufungue tafadhali.

Maswali yangu ni kama haya;
1. Lengo la kupika na kuchinja na kulisha watu kila siku isipokua juma pili ni nini?
2. Je Kuna madhara yoyote kwa wanaokwenda kushiriki kula chakula icho?
3. Ni upi salama wa chakula, mamlaka za serikali zinashiriki kupima ubora wa chakula?
4. Je hii umeshawai kuishuhudia mtaani kwenu?
5. Je hamna Imani za kishirikina zinazoambatana na zoezi hilo hasa kwenye kuchinja mnyama?
Lengo ni mchele uliwe, madhara ukila kwa pupa utavimbiwa, usalama ni kuwa makini na mifupa midogomidogo kwani ikikukwama utakufa, nimeshuhudia kwdnye misiba, kuchinja mnyama kunahitaji kisu kikali na mchinjaji atazame kaskazini(Maka).
Mwisho nakushauri acha uroho na kuchungulia majumba yasiyo kuhusu.
 
Mtu ukiwa huna asili ya wema basi ukiona mwenzako anatoa sadaka wewe lazima uwe na mashaka na huyo mtu. Wakati wewe unatumia faida yako yote ya mapato kwenye Bar wenzako wanatoa fungu kusaidia masikni.

Warabu na wahindi ndio wanaongoza kwa kutoa misaada kwa maskini tanzania lakini kama alivyo sema member mmoja humu "waswahili hawana kheri"
 
Hili si kweli. warabu na wahindi ni wakaoloni na wana mashirikiano na unasaba na mzungu kumkandamiza mtu mweusi. na hawana maadili yoyote ya maana kumshinda mtu mweusi.
 
Back
Top Bottom