Nani Karuhusu Waturuki kufanya umachinga wa kukopesha vyombo vya umeme mitaani? TBS na FCC mnayajua haya?

Mtazamo wako unaweza hisi uko sahihi kama utakuwa umefikiria ndani ya box. Lazima ukubali kutoa mawazo yako nje ya box na kuwaza kwa mapana kwa kuliangalia Taifa

Yes ni ubunifu wao, lakini nchi inanufaikaje? Hawa ni wageni wanabanwa na sheria za wageni kufanya kazi yoyote ndani ya nchi husika. Kuruhusu kila mgeni kufanya biashara yoyote kwasababu ya ubunifu ni uzwazwa kwasababu kwanza kabisa haujui background yao hivyo kuwaruhusu kuzurula mtaani nyumba kwa nyumba ofisi kwa ofisi ni kuhatarisha usalama wa nchi yetu

Kwa kutumia mwanya huo, wakijipenyeza mashushu unajua ni yaarifa ngapi watazikusanya?

Kwa mwanya huo wakijipenyeza magaidi unajua ni taarifa ngapi watazikusanya?

Sheria ziko wazi, kuna kazi ambazo wageni wanaruhusiwa kufanya na ambazo hawaruhusiwi. Walioweka huo utaratibu sio wajinga

Tukubali kama Taifa tumefeli kuweka mifumo ya kujilinda na kuwalinda wananchi kwasababu hao waturuki na watu wa mataifa mengine (kwasababu sio waturuki tu wanaofanya hizi biashara) hata kwa kuwahoji maswali ya kawaida tu utagundua kuwa wengi kama sio wote hawana vibali vya kufanya kazi nchini. Hapa maana yake hata ukipata nao shida hakuna mamlaka itakayokusaidia

Tusiwatetee eti kwasababu ni wabunifu, bali tuyaseme ili tuionyeshe serikali namna mifumo yao ilivyo loose
 
Ofisini kwetu kuna Jamaa anadaiwa na Waturuki, anawakwepa huu mwaka wa 3, sa sijui wanashindwa nn kumshtaki
Hawawezi kumshitaki kwasababu hakuna mamlaka inayo watambua na wakifanya hivyo watakuwa wanajishitaki wenyewe.

Ubaya ni kwamba siku wakikutana nae hata kwa bahati mbaya watamfanyia kitu kibaya sana. Ndivyo walivyo nimewashuhudia mara kadhaa. Kuna baadhi ya ofisi walishapigwa marufuku kukanyaga kwasababu ya tabia zao hizo za vurugu
 
Yaani Tz imekuwa Shamba la Bibi , Kodi nyingi Sana wawekezaji wa nje wanakwepa na chanzo cha upungufu wa US dollars
 
Hii ndo maana halisi ya kutofautiana hoja, nimetoa maoni yangu na wewe ukatoa yako based on maoni yangu, mwisho wa siku umekuja na point ya msingi paragraph ya mwisho though siwatetei ila nilikuwa naangalia Kwa jicho lingine nikikumbukia fujo za South Africa kuwafukuza wageni huku hizo kazi wao kama wazawa hawazifanyi.

Btw maoni yako mazuri
 
Kikuu sijawahi kuielewa..vitu vya umeme usiagize mitandaoni ni hatari
 
Ni sahihi mleta uzi.Hawa machinga wa kutoka Uturuki na nchi zingine wachunguzwe.Hata umachinga wananchi wa asili ya Tanzania wameshindwa kufanya?Kwa nini?Kifanyike nini?Na hao wanaofanya umachinga ambao si raia wa Tanzania wanakidhi vigezo?
Nami nimekutana nao sehemu kadhaa wakiwa wanakopesha bishaa zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…