Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 59,045
- 94,974
LAZIMA Wana Kadi za CCM
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
LabdaVisinge kuwepo madukania itakuwa ulishindwa kunyoosha mkono , TBS wao ukinyoosha mkono vizuri huwa hawajali
Na maafisa watenda wa vijiji na kata,niliskitika sana kumkuta afisa mtendaji kijiji kauziwa subwoofer ya mchina spika mbili ndefu kwa shilingi 550,000 ,sub ambayo bei yake ni around 200,000-250,000Walimu ni wahanga wakubwa wa hawa watu
Mtazamo wako unaweza hisi uko sahihi kama utakuwa umefikiria ndani ya box. Lazima ukubali kutoa mawazo yako nje ya box na kuwaza kwa mapana kwa kuliangalia TaifaHivyo vitu fake vipi kwao Waturuki tu mkuu au una lingine mkuu? Au ni hisia kwamba wanachukua ajira za Watanzania yaani mpaka umachinga wanafanya wao?
Kama issue ya bidhaa fake, je ukienda kwenye maduka mengine mbali na Waturuki hakuna bidhaa fake?
Kama ni issue ya umachinga wao, je kabla ya kuja wao kuanza na huu ubunifu wa kuuza vyombo Kwa mkopo, je Kuna Mtanzania yoyote alikuwa anaifanya hii kazi ya kukopesha vyombo kiasi kwamba anaingilia maslahi ya Watanzania?. Ukiangalia Kwa makini utagundua huo ni ubunifu wao na unarahisisha upatikanaji wa vyombo vya kielektroniki Kwa urahisi japo gharama inakuwa juu Kwa kuwa ni mkopo.
Suruhisho si kuwalaumu bali na wewe ingia road Kwa style/ubunifu mwingine ambao utauza Kwa wananchi maana Watz wengi hawakuwa wanafanya biashara ya mtindo huu wa mkopo ambapo mtu anachukua vyombo ANATUMIA huku ANALIPA KIDOGO KIDOGO bali ilikuwa mtu ANABANDIKA yaani UNALIPA KIDOGO KIDOGO ukimaliza ndo unachukua bidhaa.
Mie nachukulia kama UBUNIFU hivyo na nyie muige
Hawawezi kumshitaki kwasababu hakuna mamlaka inayo watambua na wakifanya hivyo watakuwa wanajishitaki wenyewe.Ofisini kwetu kuna Jamaa anadaiwa na Waturuki, anawakwepa huu mwaka wa 3, sa sijui wanashindwa nn kumshtaki
Yaani Tz imekuwa Shamba la Bibi , Kodi nyingi Sana wawekezaji wa nje wanakwepa na chanzo cha upungufu wa US dollarsWana JF.
Si kwa nia mbaya maana waturuki wametoa ajira lakini kuna haya.
Waturuki wamekuwa wakizunguka mitaani na bajaji wakikopesha vyombo mbali mbali. Msala wangu kwao ni kwamba, nani ametoa kibali cha ukaguzi wa vyombo vyao vya umeme?
Kama kuna mtu wa TBS na FCC inabidi kwa pamoja kuchunguza vifaa vinavyosambazwa na waturuki wanaofanya kazi zao kama wamachinga. Waturuki wana bajaji nyingi zinazunguka mjini nyumba kwa nyumba wakikopesha vifaa mbali mbali vya umeme.
Hasa Rice Cooker na Multicooker. Vifaa vingi vinavyotumia moto, hasa wakati wa kupika vimekuwa nyaya za machine zinapata moto kiasi cha kuyeyuka na kusababisha hatari ya kuunguza nyumba. Ni kweli Tanzania ni dampo kuu la vifaa vilivyoigiziwa na kufanywa original , lakini vingi vinaingizwa kwa njia ya panya.
Hipo haja ya kupita nyumba kwa nyumba na kukagua vifaa vya umeme vya majumbani. Hapa tutaepusha nyumba kuwa zinaungua hovyo na kusababisha uharibifu mkubwa wa vitu. Kama FCC na TBS wasipochunguza vifaa vya umeme vinavyoingizwa nchini. Basi tutegemee nyumba nyingi kuungua.
Hii ndo maana halisi ya kutofautiana hoja, nimetoa maoni yangu na wewe ukatoa yako based on maoni yangu, mwisho wa siku umekuja na point ya msingi paragraph ya mwisho though siwatetei ila nilikuwa naangalia Kwa jicho lingine nikikumbukia fujo za South Africa kuwafukuza wageni huku hizo kazi wao kama wazawa hawazifanyi.Mtazamo wako unaweza hisi uko sahihi kama utakuwa umefikiria ndani ya box. Lazima ukubali kutoa mawazo yako nje ya box na kuwaza kwa mapana kwa kuliangalia Taifa
Yes ni ubunifu wao, lakini nchi inanufaikaje? Hawa ni wageni wanabanwa na sheria za wageni kufanya kazi yoyote ndani ya nchi husika. Kuruhusu kila mgeni kufanya biashara yoyote kwasababu ya ubunifu ni uzwazwa kwasababu kwanza kabisa haujui background yao hivyo kuwaruhusu kuzurula mtaani nyumba kwa nyumba ofisi kwa ofisi ni kuhatarisha usalama wa nchi yetu
Kwa kutumia mwanya huo, wakijipenyeza mashushu unajua ni yaarifa ngapi watazikusanya?
Kwa mwanya huo wakijipenyeza magaidi unajua ni taarifa ngapi watazikusanya?
Sheria ziko wazi, kuna kazi ambazo wageni wanaruhusiwa kufanya na ambazo hawaruhusiwi. Walioweka huo utaratibu sio wajinga
Tukubali kama Taifa tumefeli kuweka mifumo ya kujilinda na kuwalinda wananchi kwasababu hao waturuki na watu wa mataifa mengine (kwasababu sio waturuki tu wanaofanya hizi biashara) hata kwa kuwahoji maswali ya kawaida tu utagundua kuwa wengi kama sio wote hawana vibali vya kufanya kazi nchini. Hapa maana yake hata ukipata nao shida hakuna mamlaka itakayokusaidia
Tusiwatetee eti kwasababu ni wabunifu, bali tuyaseme ili tuionyeshe serikali namna mifumo yao ilivyo loose
Kikuu sijawahi kuielewa..vitu vya umeme usiagize mitandaoni ni hatariNi hatari Kuna watu wanaitwa Kikuu , niliwahinkuagiza saa ikawa, poa , nikamwagizia wife nywele za singa' zikawapoa akapiga Bei mara Nne ya Bei , nikaanza kunogewa . Mara nikaona shaving machine .. Wahl Brand heavy Duty😴 Bei poa , ikaagiza!
Ndani ya wiki mbili ikatua Dodoma! Majanga yalianza Sasa niijaribu! Ile kuichomeka tu wire wake ukaanza kuungua kama Uzi wa nlyon unavoungua moto! Ndani cart moja niliagiza na kettle... Hii haikuungua .. ila ilikuwa inakula umeme unit 1+ kuchemsha maji Lita moja!
Nami nilijiuloza nani anadhibiti vifaa Kwa wasambazaji Hawa wa Online kama Kikuu?!
Nami nimekutana nao sehemu kadhaa wakiwa wanakopesha bishaa zao.Ni sahihi mleta uzi.Hawa machinga wa kutoka Uturuki na nchi zingine wachunguzwe.Hata umachinga wananchi wa asili ya Tanzania wameshindwa kufanya?Kwa nini?Kifanyike nini?Na hao wanaofanya umachinga ambao si raia wa Tanzania wanakidhi vigezo?