Nani kasema Nguruwe halali? Sio Ukristo au Uislamu kote wamemkana.

Nani kasema Nguruwe halali? Sio Ukristo au Uislamu kote wamemkana.

Katika Agano JIPYA Nguruwe ni ruksa kuliwa! Baada ya Kristo kuja vyakula vyote vilivyohesabika ni najisi katika Torati(Agano la KALE)-Walawi 11:4-43),alivitakasa kwa Neno la Mungu,(Marko7:16-19)-Yesu akasema,Kimuingiacho mtu hakimtii mtu unajisi,bali kimtokacho.Kwa kusema hivyo alivitakasa vyakula VYOTE.Na tena Neno la Mungu linasema,vilivyotakaswa na Mungu wewe usiviite Najisi,(Matendo9:11-16)
Vimtokavyo mtu ambavyo vyaweza kumtia mtu unajisi ni vile vitokavyo moyoni,yaani maovu au dhambi,(Marko7:21-23)
Kwa hiyo kama mtu hali nguruwe lakini anafanya maovu mf.uzinzi,ulawiti,ufiraji,uuaji,wizi,kinyongo,matusi,Uongo,nk mbele za Mungu huyo ni Najisi.Na walio najisi wote mahali pao ni katika lile ziwa la moto liwakalo kiberiti,(Ufunuo21:8)
Soma,(Warumi14:14).Kwa hiyo ni ruksa kula Kitimoto bila wasiwasi! Na usisikilize roho za majini zisemazo usile hiyo kitu,unachotakiwa ni kushukuru tu then unaendelea kula,(1Timotheo4:1-5)
Aya kulaga
 
Huo ni ushetani kupingana na mungu
Huyo hawezi kuwa mungu wa kweli yan akukataze kula ngurue akuruhusu kula ng'ombe ngamia lazima kunakitu hakijaeleweka kunaaina nyingi za makatazo sio kila katazo ni kwa kila mtu pia yapo makatazo ambayo ni kwa kipindi maalumu sasa muwemnasima vizuri msifuate mikumbo na kasumba za tamaduni na mila za watu mkamsingizia mungu
 
Kwenye Ukristo mambo ni tofauti siyo kama huko kwenu ambako sijui wokovu unapatikanaje.

Huku kwetu wokovu unategemea Neema ya Mungu kupitia kwa damu ya Mwana wake Yesu Kristo na siyo haya maelfu ya sheria za Musa.

Siwezi kwenda motoni kisa nilikula bata, kambale au kitimoto!
Hata nasi pia.

Lkn angalau uwe na 'twaa' ya kuweza kujizuia kutenda dhambi ndogo ndogo kama kuacha dhambi kubwa imeshindikana.

Lkn point yangu ipo palepale...Mungu Anatupenda, kuamrishwa kuacha kula nguruwe lazima atakuwa Ana madhara...haiwezekani Atuamrishe tusile tu burebure
 
Huyo hawezi kuwa mungu wa kweli yan akukataze kula ngurue akuruhusu kula ng'ombe ngamia lazima kunakitu hakijaeleweka kunaaina nyingi za makatazo sio kila katazo ni kwa kila mtu pia yapo makatazo ambayo ni kwa kipindi maalumu sasa muwemnasima vizuri msifuate mikumbo na kasumba za tamaduni na mila za watu mkamsingizia mungu
Unapingana na maandiko? Aya kulaga kika mtu na msalaba wake
 
Katika dini ya Ukristo, maandiko matakatifu ya Biblia yanapinga ulaji wa nguruwe kwa sababu inachukuliwa kuwa ni mnyama najisi.

Hii inapatikana katika kitabu cha Mambo ya Walawi 11:7-8 ambapo inasema " Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu huyo ni najisi. .Hamtakula nyama yao, wala hamgusi mizoga yao. Hao ni najisi kwenu."

Pia, kuna vifungu vingine vinavyopinga ulaji wa nguruwe kama vile Kitabu cha Kumbukumbu la Torati 14:8 ambacho kinapinga ulaji wa nguruwe, na Matendo ya Mitume 15:28-29 ambayo yanahimiza waumini kuepuka kula nyama iliyotolewa kwa sanamu na damu.

Kwa upande wa Uislamu, Quran inapinga ulaji wa nguruwe na inachukuliwa kuwa ni haramu kwa Waislamu. Kifungu cha Quran Surat al-Baqarah 2:173 kinakataza ulaji wa nguruwe pamoja na nyama ya wanyama waliochinjwa kwa njia ya kuchinjwa bila kumtaja Mungu, damu, nyama ya wanyama wanaouliwa kwa sababu ya miungu, na wanyama waliofariki kwa kifo cha asili. Kwa hivyo, Waislamu wanachukulia ulaji wa nguruwe kama jambo la kinyume na mafundisho ya dini yao.


NB: TUJADILI KWA AYA NA VIFUNGO MBALIMBALI ZA VITABU MBALIMBALI VYA DINI NGOJERA HAZITAKIWI.

View attachment 2613342
ajabu ni kwamba, baada ya mfungo kuisha, ukichelewa kuagiza unakuta imeisha. acheni unafiki.
 
Tutamla hata iweje. Awe haram asiwe haram tunaendelea kumla
 
Unapingana na maandiko? Aya kulaga kika mtu na msalaba wake
Unasoma andiko moja tu unabeba kasumba bila kuangalia nyakati na makusidio ya kila andiko mungu wa kweli hawezi muhukumu mja kisa kula mnyama fulani ambae akimla anaenda tumboni then chooni
 
Katika dini ya Ukristo, maandiko matakatifu ya Biblia yanapinga ulaji wa nguruwe kwa sababu inachukuliwa kuwa ni mnyama najisi.

Hii inapatikana katika kitabu cha Mambo ya Walawi 11:7-8 ambapo inasema " Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu huyo ni najisi. .Hamtakula nyama yao, wala hamgusi mizoga yao. Hao ni najisi kwenu."

Pia, kuna vifungu vingine vinavyopinga ulaji wa nguruwe kama vile Kitabu cha Kumbukumbu la Torati 14:8 ambacho kinapinga ulaji wa nguruwe, na Matendo ya Mitume 15:28-29 ambayo yanahimiza waumini kuepuka kula nyama iliyotolewa kwa sanamu na damu.

Kwa upande wa Uislamu, Quran inapinga ulaji wa nguruwe na inachukuliwa kuwa ni haramu kwa Waislamu. Kifungu cha Quran Surat al-Baqarah 2:173 kinakataza ulaji wa nguruwe pamoja na nyama ya wanyama waliochinjwa kwa njia ya kuchinjwa bila kumtaja Mungu, damu, nyama ya wanyama wanaouliwa kwa sababu ya miungu, na wanyama waliofariki kwa kifo cha asili. Kwa hivyo, Waislamu wanachukulia ulaji wa nguruwe kama jambo la kinyume na mafundisho ya dini yao.


NB: TUJADILI KWA AYA NA VIFUNGO MBALIMBALI ZA VITABU MBALIMBALI VYA DINI NGOJERA HAZITAKIWI.

View attachment 2613342
hiyo ilikuwa kwa ajili wa walawi. Yesu kristo alikuja kutakasa hayo yote ndiyo maana ya ujio wake. Najis ni kile kimtokacho mtu mdomoni mwake maana hicho chatoka moyoni mwake. Ila kiingiacho kinapitia tumboni mwishoni kinaenda chooni.
 
hiyo ilikuwa kwa ajili wa walawi. Yesu kristo alikuja kutakasa hayo yote ndiyo maana ya ujio wake. Najis ni kile kimtokacho mtu mdomoni mwake maana hicho chatoka moyoni mwake. Ila kiingiacho kinapitia tumboni mwishoni kinaenda chooni.
Aya kulaga tu, wewe sio walawi
 
Chaumbile Imulungu ni chakumemena..[emoji123][emoji106]
Chaumbile Imulungu ni chakumemena!
[emoji1427][emoji1427]
قُلْ هَلُمَّ شُهَدَاءَكُمُ الَّذِينَ يَشْهَدُونَ أَنَّ اللَّهَ حَرَّمَ هَـٰذَا ۖ فَإِن شَهِدُوا فَلَا تَشْهَدْ مَعَهُمْ ۚ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَالَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ وَهُم بِرَبِّهِمْ يَعْدِلُونَ

[ AL - AN-A'AM - 150 ]
Sema: Leteni mashahidi wenu watao shuhudia kuwa Mwenyezi Mungu ameharimisha hawa. Basi wakishuhudia, wewe usishuhudie pamoja nao. Wala usifuate matamanio ya walio zikanusha Ishara zetu, wala hawaiamini Akhera, na ambao wanamlinganisha Mola Mlezi wao na wengine.

الْيَوْمَ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۖ وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَّكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَّهُمْ ۖ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ مُحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ وَلَا مُتَّخِذِي أَخْدَانٍ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِالْإِيمَانِ فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ

[ AL - MAIDA - 5 ]
Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. Na chakula cha walio pewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao. Na pia wanawake wema miongoni mwa Waumini, na wanawake wema miongoni mwa walio pewa Kitabu kabla yenu, mtakapo wapa mahari yao, mkafunga nao ndoa, bila ya kufanya uhasharati wala kuwaweka kinyumba. Na anaye kataa kuamini bila shaka a'mali yake imepotea, naye katika Akhera atakuwa miongoni mwa wenye khasara.

Biblia Takatifu Mungu Anawaagiza Musa na Haruni Wawaambie wana Israeli nini Wale na nini Wasile!
[emoji1427][emoji1427]
Bible. Leviticus 11:1-2
[1]And the LORD spake unto Moses and to Aaron, saying unto them,
BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,
[2]Speak unto the children of Israel, saying, These are the beasts which ye shall eat among all the beasts that are on the earth.
Neneni na wana wa Israeli, mkiwaambia, Wanyama hawa ndio wanyama wenye uhai mtakaowala, katika hayawani wote walio juu ya nchi.

soma mpaka mstari wa.24
ww Mndenge unaesema haramu tuwekee Ushahidi wa Ayat toka Biblia Takatifu ima Quran.[emoji101][emoji101]
 
We utajua mwenyewe mzee,sio kila mtu anayaamini hayo maandiko yako,we tuliochagua kuyaish maisha fully,nguruwe ni mpendwa wetu
 
Hata nasi pia.

Lkn angalau uwe na 'twaa' ya kuweza kujizuia kutenda dhambi ndogo ndogo kama kuacha dhambi kubwa imeshindikana.

Lkn point yangu ipo palepale...Mungu Anatupenda, kuamrishwa kuacha kula nguruwe lazima atakuwa Ana madhara...haiwezekani Atuamrishe tusile tu burebure

Soma hapa chini uridhike. Na adhabu ya kugusa au kula wanyama hawa najisi ilikuwa ni kusubiri mpaka jioni unafua nguo na au kuoga basi kazi kwisha. Nasikia nyinyi huko mnakula ngamia japo humu naona katajwa kuwa hafai....masheria haya Musa kwetu wakristo hayana nafasi katika wokovu wetu. Nitaelewa kama kuna sababu zingine za kiafya......

MAMBO YA WALAWI 11

1 Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,
Mambo ya Walawi 11:1

2 Neneni na wana wa Israeli, mkiwaambia, Wanyama hawa ndio wanyama wenye uhai mtakaowala, katika hayawani wote walio juu ya nchi.
Mambo ya Walawi 11:2

3 Kila mnyama mwenye kwato katika miguu yake, mwenye miguu ya kupasuka kati, mwenye kucheua, katika hayawani, hao ndio mtakaowala.
Mambo ya Walawi 11:3

4 Pamoja na hayo, wanyama hawa hamtawala katika wale wenye kucheua, na katika wale walio na kwato; ngamia, kwa sababu yuacheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.
Mambo ya Walawi 11:4

5 Na wibari, kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.
Mambo ya Walawi 11:5

6 Na sungura, kwa sababu hucheua, lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.
Mambo ya Walawi 11:6

7 Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.
Mambo ya Walawi 11:7

8 Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu.
Mambo ya Walawi 11:8

9 Katika hao wote walio ndani ya maji mtakula hawa; kila aliye na mapezi na magamba, ndani ya hayo maji, na ndani ya bahari, na ndani ya mito, mtakula hao.
Mambo ya Walawi 11:9

10 Na hao wote wasio na mapezi na magamba, ndani ya bahari, na ndani ya mito, katika hao waendao majini, na katika wote wenye uhai, waliomo majini, hao ni machukizo kwenu,
Mambo ya Walawi 11:10

11 watakuwa machukizo kwenu; msiile nyama yao, na mizoga yao itakuwa machukizo kwenu.
Mambo ya Walawi 11:11

12 Kila asiye na mapezi wala magamba aliye ndani ya maji ni machukizo kwenu.
Mambo ya Walawi 11:12

13 Kisha katika ndege hawa watakuwa ni machukizo kwenu; hawataliwa, ndio machukizo; tai, na furukombe, na kipungu;
Mambo ya Walawi 11:13

14 na mwewe, na kozi kwa aina zake,
Mambo ya Walawi 11:14

15 na kila kunguru kwa aina zake;
Mambo ya Walawi 11:15

16 na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake;
Mambo ya Walawi 11:16

17 na bundi, na mnandi, na bundi mkubwa;
Mambo ya Walawi 11:17

18 na mumbi, na mwari, na mderi;
Mambo ya Walawi 11:18

19 na korongo, na koikoi kwa aina zake, na hudihudi, na popo.
Mambo ya Walawi 11:19

20 Tena vyote vitambaavyo vyenye mabawa viendavyo kwa miguu minne, hivi ni machukizo kwenu.
Mambo ya Walawi 11:20

21 Pamoja na hayo, hivi vitambaavyo vyenye mabawa viendavyo kwa miguu minne ni halali kula, hao walio na miguu mirefu, ya kurukia juu ya nchi;
Mambo ya Walawi 11:21

22 katika hao mna ruhusa kuwala; nzige kwa aina zake, na nzige kuu kwa aina zake, na panzi kwa aina zake, na parare kwa aina zake.
Mambo ya Walawi 11:22

23 Lakini vyote vitambaavyo vyenye mabawa, vilivyo na miguu minne, ni machukizo kwenu.
Mambo ya Walawi 11:23

24 Nanyi mtakuwa najisi kwa wanyama hao; kila atakayegusa mzoga wao atakuwa ni najisi hata jioni;
Mambo ya Walawi 11:24

25 na mtu awaye yote atakayechukua cho chote cha mizoga yao atafua nguo zake, naye atakuwa najisi hata jioni.
Mambo ya Walawi 11:25

26 Kila mnyama aliyepasuliwa ukwato, naye hana kwato mbili, wala hacheui, huyo ni najisi kwenu; kila agusaye wanyama hao atakuwa ni najisi.
Mambo ya Walawi 11:26

27 Tena kila mnyama aendaye kwa vitanga vyake, katika hao wanyama wote waendao kwa miguu minne, hao ni najisi kwenu; awaye yote atakayegusa mizoga yao, atakuwa ni najisi hata jioni.
Mambo ya Walawi 11:27

28 Na huyo atakayechukua mzoga wa wanyama hao atafua nguo zake, naye atakuwa ni najisi hata jioni; hao ni najisi kwenu
Mambo ya Walawi 11:28

29 Tena katika vitu vile vitambaavyo, vitambaavyo juu ya nchi, hivi ni najisi kwenu; kicheche, na panya, na mjombakaka, kwa aina zake,
Mambo ya Walawi 11:29

30 na guruguru na kenge, na mjusi na goromoe, na lumbwi.
Mambo ya Walawi 11:30

31 Wanyama hao ndio walio najisi kwenu katika hao watambaao; awaye yote atakayewagusa, wakiisha kufa, atakuwa ni najisi hata jioni.
Mambo ya Walawi 11:31

32 Tena kitu cho chote, wanyama hao mmojawapo atakachokiangukia, wakiisha kufa, kitakuwa ni najisi; kwamba ni chombo cha mti, au nguo, au ngozi, au gunia, chombo cho chote kitakachoangukiwa, ambacho ni chombo cha kufanyia kazi yo yote, lazima kitiwe ndani ya maji, nacho kitakuwa ni najisi hata jioni; ndipo kitakapokuwa ni safi.
Mambo ya Walawi 11:32

33 Na kila chombo cha udongo, wanyama hao mmojawapo atakachokiangukia, kila kilichomo ndani yake kitakuwa ni najisi, na hicho chombo kitavunjwa.
Mambo ya Walawi 11:33

34 Kila chakula kilichomo, ambacho ni kuliwa, hicho ambacho maji hutumiwa juu yake, kitakuwa ni najisi; na kila kinyweo ambacho ni cha kunywewa, kilichomo katika chombo kama hicho, kitakuwa ni najisi.
Mambo ya Walawi 11:34

35 Na kila kitu kitakachoangukiwa na kipande cho chote cha mizoga yao kitakuwa najisi; kwamba ni tanuru, au meko ya vyungu, kitavunjwa vipande vipande; ni najisi vitu hivyo, navyo vitakuwa najisi kwenu.
Mambo ya Walawi 11:35

36 Pamoja na hayo, chemchemi, au shimo, ambamo maji yakusanyika, vitakuwa ni safi; lakini hicho kitakachogusa mizoga yao kitakuwa ni najisi.
Mambo ya Walawi 11:36

37 Na kipande cho chote cha mzoga kikiwa kimeangukia mbegu za kupandwa zitakazopandwa, zitakuwa safi.
Mambo ya Walawi 11:37

38 Lakini kwamba hizo mbegu zilitiwa maji na cho chote cha mizoga yao kuziangukia, ni najisi kwenu.
Mambo ya Walawi 11:38

39 Kama akifa mnyama awaye yote, ambaye mna ruhusa kumla, yeye anayeugusa mzoga wake atakuwa najisi hata jioni.
Mambo ya Walawi 11:39

40 Na yeye atakayekula nyama ya mzoga wake atafua nguo zake, naye atakuwa najisi hata jioni; yeye atakayeuchukua mzoga wake atafua nguo zake, naye atakuwa ni najisi hata jioni.
Mambo ya Walawi 11:40

41 Na kila kitu kitambaacho juu ya nchi ni machukizo; hakitaliwa.
Mambo ya Walawi 11:41

42 Kila aendaye kwa tumbo lake, na kila aendaye kwa miguu minne, na kila aendaye kwa miguu mingi, maana, ni vyote vyenye kutambaa vitambaavyo juu ya nchi, hamtavila, kwa kuwa ni machukizo.
Mambo ya Walawi 11:42

43 Msifanye nafsi zenu kuwa ni chukizo kwa kitu cho chote chenye kutambaa, kitambaacho, wala msifanye nafsi zenu kuwa ni najisi kwa vitu hivyo, mkajipatia uchafu kwa hivyo.
Mambo ya Walawi 11:43

44 Kwa kuwa mimi ni Bwana, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yo yote, kiendacho juu ya nchi.
Mambo ya Walawi 11:44

45 Kwa kuwa mimi ni Bwana niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu; basi mtakuwa watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu.
Mambo ya Walawi 11:45

46 Hii ndiyo sheria katika hao wanyama, na ndege, na kila kiumbe kilicho hai, kiendacho ndani ya maji, na kila kiumbe kitambaacho juu ya nchi;
Mambo ya Walawi 11:46

47 ili kupambanua kati ya hao walio najisi na hao walio safi, na kati ya kiumbe kilicho hai ambacho chaliwa, na hicho kilicho hai ambacho hakiliwi.
Mambo ya Walawi 11:47
 
Back
Top Bottom