Nani kati ya Samia na mfumo mfu anayetawala Tanzania?

Father of All

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2026
Posts
458
Reaction score
843
1783790796868.png

Alipoapishwa kuwa rais kutokana na ajali ya kufiwa mtangulizi wake, rais Samia aliahidi mambo mengi mazuri. Alimuita Tundu Lissu na kuongea naye mambo mazuri. Alianza kujitenganisha na utawala wake na Magufuli. Alianza kutofautiana na mfumo.

Muda haukupita, mara Samia wa matumaini akaanza kuwa Samia wa maangamizi na kukatisha tamaa. Kwa wajuzi wa mambo, mfiumo wetu hatari na uliochakaa ulianza kumvuta sikio. Bila kujua la kufanya, sasa Samia tuliye naye ni tofauti kabisa na yule aliyeingia kwa matumaini na mbwembwe.

Ghafla bin vu, upotezaji, utekaji, na mauaji ya wanaharakati na waandamanaji vikaanza kuwa zana zake za maangamizi. Bila hili wala lile, uchawa na ufisadi vikarejea na kuanza kuitafuna nchi. Taratibu, mengi yja maovu aliyoahidi kutokomeza yakaanza kuwa alama zake kiuongozi na utendaji. Waliokuwa wamewekwa kando kama vile Dk. Bashiru Ali Kakurwa na wengine wakaanza kuibuka kwenye uteuzi wake usio na kichwa wala miguu. Mizengwe na ubabaishaji ndo vikaanza kushamiri kuliko hata wakati wa Magu!

Je, kati ya Samia na mfumo, nani anatawala Tanzania kwa sasa? Kwa balaa na hali hii, nini kifanyike kuikomboa nchi yetu toka kwenye mikono michafu ya machawa wanaokula kwa mikono na miguu bila kunawa huku wakinonihino kwenye chombo waliamo---Tanzania?
 
Tatizo kubwa ni team Kikwete na machawa wake!
Mtu mbaya zaidi kwa ustawi wa Tanganyika.
 
Hakuna cha mfumo wala nini. Wahuni ndiyo wamemuweka mtu kati. Kila anachofanya, anafanya kwa matakwa yao. Wananchi hawana mtetezi. Mafuta bei juu, cement bei juu, maisha yamepanda mpaka basi! Pesa haina thamani! Na wala hajali.
 
Back
Top Bottom