Nani mkubwa kati ya Mkurugenzi wa TISS na IGP?

Na intelejensia ya jeshi itakuwa inafanya kazi gani?
 
Uzi umeishia hapa.
 
Ingekuwa ni katika nchi ambazo Idara za usalama zinatenda kazi kwa weledi na kulinda maslahi ya nchi, na sio kujipendekeza kwa namna ya kisiasa, au yale mambo ya unanijua mimi nani? Yani chukulia Taasisi kama Mosad, M16, KGB, CIA, hiyo TISS ndiyo ilitakiwa iwe engine ya nchi katika nyanja zote, za kiuchumi, kisiasa diplomasia, technology and innovation, lakini kwa hapa Tz naona angalau jeshi la polisi kinajitahidi kuliko hao TISS, angalau polisi wanakamata hata majambazi , so IGP ni mkubwa kuliko huyo mkurugenzi wa TISS, ingawa katika nchi za wenzetu wakuu wa Intelligence Agencies ni wakuu kimantiki kuliko police force.
 
Kwa hiyo unataka kusema diwani baada yakuondlewa tiss Kama hajastaafu anaweza kurudi polisi kuwa cp we vp ule ulikuwa uteuzi maana yake kuwa dgtiss tayari anakuwa na lenki ya igp.igp nayo ni utezi
Akistaafu utumishi huko alikoteuliwa, anakuja kupigiwa parade ya kuagwa kijeshi akiwa amevaa cheo cha Commissioner of Polisi.
Na yeye hatakuwa wa kwanza rejea hata yule aliyeteuliwa kuwa CGP aliagwa kijeshi kwa cheo chake cha Mwisho alichokuwa nacho TPDF, pia CP Mussa aliyeteuliwa kuwa RAS aliagwa kwa cheo chake cha mwisho Jeshini yaani CP.
Bila kusahau Balozi Sirro na Balozi Kaniki wote waliagwa kwa vyeo vyao vya mwisho Jeshini na sio vyeo vya uteuzi.
 
Kitu unachopaswa kujua Majeshi yote Duniani yana vitengo vyao vya ndani vya intelijensia ya Kijeshi.
Kwahiyo taarifa kutoka TISS ni nyongeza na sio kama utendaji wao unategemea taarifa za TISS kivile.
Na intelijensia ya kijeshi iko too deep kuliko intelijensia ya kiraia kwasababu kama wakienda wote kwenye observation ya silaha za adui mtu wa ndani ya Jeshi anaweza kutoa more details za formations, aina ya silaha na uwezo wake kuliko huyo raia ambaye hayuko familiar na hizo silaha ukizingatia training yake yenyewe inahusisha light weapons how comes aweze kuwa too deep kwenye mizinga na vifaru
 
Hata magereza ki protocol wanatakiwa wawe juu ya TIS maana katiba hadi muda huu haitambui TIS kama jeshi majeshi ya ulinzi na usalama yanayotambuliwa kwenye katiba ni Jwtz, Polisi, Magereza na Jeshi la kujenga taifa, kwahiyo ni basi tu huwa wanavunja protocol ilitakiwa aanze 1.CDF , 2. IGP, 3.CGP 4. DGTIS .

Ila huwa namuona anakaa wa 3 pembeni ya IGP sijui huwa wanatumia protocol gani
 
IGP kiprokali ni superior. Jeshi la polisi ni taasisi iliyoanzishwa kikatiba kwa ibara maalum.

Hakuna mahali popote kwenye katiba imeanzishwa taasisi/idara inayoitwa TISS.

Taasisi iliyoanzishwa kikatiba ni superior kuliko iliyoanzishwa na sheria ya kawaida.
 
Kimamlaka, wako sawa kwani wote ni wateuliwa wa raisi.

Kicheo, wako tofauti kwani DG wa TISS aweza kuwa na backgound ya JWTZ kwenye vyeo vya juu hadi Brigedia Jenerali wakati backgound ya IGP ni inspector, kamishna msaidizi na kamishna, hivyo IGP kuwajibika kumpigia saluti DG wa TISS.

Kiutendaji, DG wa TISS kazi zake ni siri wakati IGP ni haiko hivyo kwani mara kwa mara hutakiwa kujitokeza kwa umma kuelezea matendo ya shughuli za polisi.

Kiprotokali, IGP ndie anaepewa kipaumbele kwani yeye ndie anaesimamia shughuli nyingi zinohusisha polisi kama uongozaji misafara barabarani, doria, na usalama wa raia kwa ujumla akiwemo DG wa TISS mwenyewe.

Hiyo hata utambulisho wowote nadhani wazingatia hilo.

Hivyo kiujumla DGIS ni mkubwa kuliko IGP kutokana na wigo wa majukumu yake na background pia.
 
Tumeshuhudia mara kadhaa kwenye nchi kadhaa wanajeshi wanatangaza hadharani kumuondoa Rais madarakani ndani ya saa 24 iwapo hatajiuzulu kwa hiyari.

Wamefanya mapinduzi hadharani mfano halisi Zimbabwe na Egypt wanajeshi walitangaza kufanya mapinduzi iwapo Rais hatoachia ngazi ndani ya muda waliopanga.

Hizo idara zao za usalama zilishindwa nini kumlinda na kuzuia mapinduzi yaliyotangazwa yasitokee?

Maana wenzetu kama Misri idara zao za kiusalama wa Taifa zipo imara sana lakini jeshi linapoamua hakuna wa kuzuia.
 
Wote wako sawa

Wote wanaongoza vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo kisheria na kikatiba hakuna ambacho kipo juu ya kingine.

Tofauti yao pekee TISS iko chini ya Ofisi ya Rais.
Sasa kwa kusema Kwako tu kuwa TISS iko chini ya Rais huoni kuwa logically tayari umeshatoa Jibu kuwa TISS na hasa DGIS yuko juu ya IGP? Yaani IGP awe juu ya DGIS?

Yaani jambo hili dogo tu mmeshindwa Kuling'amua? Sasa naanza Kuamini kuwa Elimu ya Tanzania iko ICU na huenda karibuni tu Ikafa na Kuzikwa kabisa.
 
Lakini ikumbukwe IGP anawakilisha taasisi kubwa kiutendaji tena iliyoanzishwa kwa mujibu wa katiba.

Wakati DGIS anaongoza idara ambayo imeanzishwa kisheria na sio kikatiba.

Ni jambo lililowazi kwamba kitu chochote kilichoanzishwa na katiba ya nchi kina nguvu mbele ya macho ya sheria kuliko kilichoanzishwa na sheria za kawaida.

Tafsiri yake ni kwamba mchakato wa kulibadilisha jeshi la polisi ni suala lenye mchakato mrefu kwasababu lazima uguse katiba inasemaje ili usije kwenda kinyume na katiba.

Lakini mchakato wa kuibadilisha idara ya usalama ni wa kawaida maana unapeleka tu mswada wa marekebisho ya sheria husika inafanyiwa amendment haihitaji kuhusisha katiba.
 
Hata wizara ya uwekezaji ipo chini ya ofisi ya Rais, ina maana wizara hiyo ni superior kuliko wizara zingine?

Jeshi la polisi lipo kikatiba ila idara ya usalama haipo kwenye katiba bali imeanzishwa na sheria za kawaida tu.

Ikumbukwe 'idara' ni sehemu ndogo ya taasisi fulani kubwa.

Polisi ni jeshi kamili lakini idara ya usalama sio jeshi kamili linalojitegemea.
 
Usipate shida kaka, angalia wanavyo kaa. Kulia kabisa anakaa mkuu wa majeshi halafu kushoto kabisa ana kaa mkuu wa magereza.
Highest to lowest.
Anayemfuata kamanda John ndio jibu lako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…