Nani mkubwa kati ya Mkurugenzi wa TISS na IGP?

Facts mkuu
 
Beware, ChatGTP huwa inadanganya muda mwingine
 
Mkimaliza kubishana na mimi mnijulishe kati ya CIA na FBI nani mkubwa?
FBI - wanahusika na masuala ya usalama yanayohusu federal states za USA (ndani ya USA yote)
Wanaweza kukamata (arrest)

CIA - Ni kwa mambo ya intelijensia ya usalama ya nje ya Marekani.
Hawawezi kukamata kisheria.
 
FBI - wanahusika na masuala ya usalama yanayohusu federal states za USA (ndani ya USA yote)
Wanaweza kukamata (arrest)

CIA - Ni kwa mambo ya intelijensia ya usalama ya nje ya Marekani.
Hawawezi kukamata kisheria.
Hayo yote nayajuwa, bado hujasema mkubwa nani.
 
Hapa umechemka, Polisi, Magereza na uhamiaji ni majeshi yapo chini ya wizara ya mambo ya ndani.

Huko kote idara ya usalama wa Taifa inaweza kuingia kwa njia zake na kupelekea hata kumng'oa IGP, CGP au Kamishna General wa Uhamiaji.

Mabadiriko mengi nyeti unayoyaona ni kazi ya Tiss.

Ukitaka kujuwa Tiss ndio engene ya nchi hata matibabu ya viongozi inatumika hospitali yao Mzena ambayo imewezeshwa kila kitu na huduma zake ni bora sana.
 
Tiss ni kama maji…. Yapo kwenye kilq part ya mfumo ulio formal na informal

Kulinganisha tiss na jeshi ni kosa kubwa nsio maana militarization ya tiss is highly discouraged

Maybe next time wasiwe wanatambulisha kabisa
 
Wote wako sawa

Wote wanaongoza vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo kisheria na kikatiba hakuna ambacho kipo juu ya kingine.

Tofauti yao pekee TISS iko chini ya Ofisi ya Rais.
Hiyo tofauti uliyoitoa ndiyo ukubwa wenyewe
 
Nadhani wote wapo 18 and above thus wote ni wakubwa.
 

Nilichokuwa najaribu kumjibu ni kwamba idara ama taasisi fulani kuwa chini ya ofisi ya Rais haina maana kwamba ndiyo ipo so special kuliko zingine bali ni mgawanyo wa majukumu tu.

Jeshini kuna military intelligence, polisi kuna kitengo cha intelligence na majeshi mengine yote yana vitengo kama hivyo.

Majeshi mengine yote yameanzishwa kikatiba isipokuwa TISS ndiyo imeanzishwa na sheria ya kawaida na sio kikatiba.

Je, hufahamu kwamba kitu kilichoanzishwa kikatiba ni superior na kina nguvu kuliko kitu kilichoanzishwa kwa sheria za kawaida?
 
Usipende sana kutumia Chatgpt itakuja kukuumbua mbele ya watu wanaojua mambo kuliko hiyo Chatgpt alafu ukirudi kuiuliza itakuomba msamaha kwa kusema ilikosea kukupa taarifa, siyo muda wote inakua sahihi.
 
Polisi, Magereza na uhamiaji ni majeshi yapo chini ya wizara ya mambo ya ndani.
Je, hujui kwamba TISS nayo ipo chini ya wizara ya Utumishi na utawala bora?

Pia TISS sio jeshi kwa mujibu wa sheria bali inatambulika kama 'idara'.

Kuwa na silaha na uwezo wa kukamata pekee hakufanyi kuitwa jeshi maana hata PCCB wana silaha na wana power ya kukamata watuhumiwa wa makosa ya rushwa lakini huwezi kuiita ni jeshi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…