Nani mkubwa kati ya Mkurugenzi wa TISS na IGP?

Natamani ungejua kwanini mmoja anaitwa 'Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama' na mwingine anaitwa 'Mkurugenzi Mkuu' wa 'Idara' hapo ungekuwa na uwezo wa kung'amua mambo kiwepesi.
 
Ndio nashangaa maana Rso ndio katibu wa vikao vya kamati ya ulinzi na usalama mkoa
Usikariri bwashee mara nyingi katibu wa vikao huwa RPC , rejea sakata la yule RC wa shinyanga na RPC wa wakati ule , ikabidi jiwe aingilie kati

kwa leo inatosha😀😀
 

Ni kweli hata w'mwanzoni mwa utawala wa Nyerere usalama wa Taifa kilikua ni kitengo tu ndani ya polisi. Baadae kilihamishiwa chini ya ofisi ya Rais mpaka sasa. Kazi yao ni uchunguzi .

Polisi wanadaraulika na kutumiwa na wanasiasa kusafisha uchafu wa serikali kwa sababu wao hawajulikani kama wanaajiriwa kama watumishi wengine chini ya Utumishi wa umma au Jeshi chini ya amiri jeshi mkuu. Na kwa sababu wako chini hawapo chini ya ofisi ya Rais basi wanaonekana kuwa wanapokea maelekezo wote ya usalama ya taifa
 
Ili leta kizaizai sana , maana kule magereza walikuwepo ma CP waliojiandaa kuwa CGP ila sasa ndo maelekezo ya amiri jeshi Mkuu hakuna wa kupinga
Katika ndoto zao walisahau kuweka akiba ya uwezo wa mamlaka ya uteuzi katika kuamua kuwaletea mtu kutoka nje ya idara yao.
Maana aliwahi kuwatahadharisha wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa yale maghorofa yao pale ukonga kuwa anaweza kuwaletea CGP kutoka nje ya Magereza
 
We unaodhani jiwe alikuwa fair?, unadhani CGP kutoka JWTZ angepewa ushirikiano unaotakiwa?

kilichonifurahisha afande Mzee wakati anatoka jeshini alikuwa brigadier kule anaenda kuongoza jeshi zima hahaha
 
Kwa sababu katiba hiyo hiyo haijaizuia CIC kuunda majeshi mengine iwapo itaonekana inafaa na mahitaji ya kiulinzi na usalama.

Ndio maana likaongezwa Uhamiaji, Fire na hivi karibuni Tiss.

Ulielezwa Uhamiaji kujiita idara ni Camouflage, kwa sababu ni jeshi pekee pia linabeba diplomasia ya nchi.

Tiss mahitaji yameongezeka hivyo wanahitaji force waweze kuintervene wao wenyewe

Fire kwa sababu ya changamoto ya underfunding kutoka Halmashauri na uwezo wa nchi kukabiliana na majanga.

Katiba inatakiwa ifanyiwe marekebisho makubwa moja wapo, inaitambua jkt kama jeshi wakati ni kamandi ndani ya jw hivyo kuiweka kama jeshi huru si sahihi.

Kwa nini, kwa sababu service man wakimaliza Kuna kamandi ya Reserve wahesabike huko, na mgambo kamandi ya Militia ipo.

Hivyo tunahitaji marekebisho ya katiba Ili yawekwe rasmi majeshi tajwa na kuorodheshwa majukumu Yao kila moja.
 
Umesoma marekebisho ya Sheria Yao ya mwaka 2023?

Idara ya usalama Sasa ni jeshi kamili.
Tena la ulinzi na Usalama
Yaani wanapiga kote kote
 
Natamani ungejua kwanini mmoja anaitwa 'Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama' na mwingine anaitwa 'Mkurugenzi Mkuu' wa 'Idara' hapo ungekuwa na uwezo wa kung'amua mambo kiwepesi.
Hili neno nalo halipo sahihi
Chief of defence force maana yake ni mkuu wa jeshi la ulinzi tu.

Ni kama Sasa police wanavyolazimisha IGP aitwe mkuu wa jeshi la police na walitaka cheo chake kiitwe Chief of police force
 
Mkuu ni kweli usemayo lakini DG wa TISS nimeongelea hapo juu kiufundi yupo juu ya IGP kwani kwa mfano ana uwezo wa kumweka kizuizini IGP au pia kiongozi yoyote wa ngazi za juu.

Lakini kama ni yeye uamuzi ukipitishwa ni Deputy na mazee wa MI ndo watamweka DG wao kizuizini kama sio…

Huu ni mfano mojawapo wa kwanini DG wa TISS ni mkubwa kwa IGP.

Mfano mwingine ni kuhusu special operations kama kuwashugulikia magaidi au majasusi wa kitoka nje ambao ni TISS ambao huzisimamia na kutoa maagizo kwa IGP ( behind the scenes) ambae atatoa ushirikiano kwa logistics.

Operesheni kama ya kumkamata mtuhumiwa wa uhaini Mohamed Tamim iliongozwa na TiSS na MI, mzee Mabere Marando akiwemo na si Solomon Liani aliekuwa IGP wa wakati huo. Hivyo ukiona hawa TISS wako kazini fahamu Mkuu wa nchi amepewa brief na ameOK operation na IGP apigiwa simu aandae logistics.

Kwa sheria na katiba TISS yapaswa kugawanywa kwa kuwa na ya ndani (domestic kama FBI) inokuwa chini ya Mambo ya Ndani na TiSS foreign (Kama CIA) ambayo inakuwa chini ya wizara ya mambo ya Nje au hukohuko Utawala Bora au Ofisi ya Raisi.

TISS ni idara muhimu kwa nchi si ya kuichukulia poa na huko nyuma niliwahi kutoa mapendekezo ya muundo wake.

Hivyo ni kweli mabadiliko ya katiba na sheria ni muhimu ili kuhakikisha integrity inakuwepo kwenye Idara na vyombo vingine.
 
Tunaomba link ya muongozo uliotoa
 
Umesoma marekebisho ya Sheria Yao ya mwaka 2023?

Idara ya usalama Sasa ni jeshi kamili.
Tena la ulinzi na Usalama
Yaani wanapiga kote kote
Samahani mkuu. Kama hutojali naomba nipatie specific provision inayoitambua idara kama jeshi kamili.
 
Hili neno nalo halipo sahihi
Chief of defence force maana yake ni mkuu wa jeshi la ulinzi tu.

Ni kama Sasa police wanavyolazimisha IGP aitwe mkuu wa jeshi la police na walitaka cheo chake kiitwe Chief of police force
Ndiyo hivyo mkuu title ya CDF inasomeka mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama na sio mkuu wa jeshi.

Neno 'forces' lina maana zaidi ya jeshi mkuu na halipo pale kwa bahati mbaya bali kwa maksudi kabisa.
 
Hivi kuna mahali huyu mama yake Lucas Mwashambwa anasoma au yote yanatoka akilini naona anaflow tu bila kusoma

Au kameza hii hotuba?
​

Kuna kitu kinaitwa TELEPROMPTER, screen za vioo ziko mbili moja kushoto nyengine kulia zinapitisha maandishi anasoma. Sio yeye tu marais wengi hata trump anatumia hizo kusoma script.

Ukitaka uone uwezo wa kiongozi yeyote kwenye kukremisha na hoja basi muache aflow bila teleprompter/script.
 
Unazungumzia umilikishwaji wa siraha vita na umilikishwaji wa nyaraka za kijasusi! Ukumbuke kwamba Hao wote wanaripoti kwa amiri jeshi mkuu!
 
Umesoma marekebisho ya Sheria Yao ya mwaka 2023?

Idara ya usalama Sasa ni jeshi kamili.
Tena la ulinzi na Usalama
Yaani wanapiga kote kote
Narudia tena mkuu, TISS sio 'jeshi kamili' hakuna sehemu yoyote ya sheria inayoitambua TISS kama jeshi bali kama idara ama chombo kinachoshughulikia masuala ya usalama kwa kutumia intelijensia.

Mfano sheria ya Uhamiaji namba 54 ya ambayo imefanyiwa marejeo mwaka 2016 inaitambua idara ya uhamiaji kama jeshi kamili kifungu cha 4 (3).

Lakini ukisoma sheria yote ya TISS hakuna mahali inataja TISS kama jeshi kamili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…