ubarinolutu
JF-Expert Member
- Oct 22, 2012
- 2,424
- 4,954
S2Kizzy
Mika Mwamba
Leo kumekuwa na ubishani mkali, je ni nani Producer Bora wa mziki , kati ya Producer namba moja wa muda wote wa Tanzania ajulikanae kama s2kizzy, na engineer wa mziki aliewahi kuwa producer wa nyimbo za bongo fleva Kwa Jina Milka Mwamba.
Sasa s2kizzy ambaye Kwa Sasa ni namba moja nchini ametengeneza nyimbo kama Tetema, far away diamond, enjoy, na Mila Mwamba ametengeneza nyimbo kama Twenzetu ya chege, na Mabinti wa kitanga Bwana misosi.
Wanajamvini ambao sio watoto wa 2000, Nina matumaini wanawajua maproducer wote Hawa wawili, Sasa nani mkali kati ya mzungu mika Mwamba na mbongo S2kizzy