Nani yuko nyuma ya hujuma dhidi ya Bomba la Mafuta la Kigamboni?

Nani yuko nyuma ya hujuma dhidi ya Bomba la Mafuta la Kigamboni?

RWANDES

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
1,788
Reaction score
4,401
Kutokana hali iliyopo sasa, ikumbukwe kwamba mkuu wa mkoa Dar es Salaam, Amos Makalla juzi alikuta bomba la mafuta wilaya ya Kigamboni watu ambao hakuwagaja wamejiunganishia mafuta cha ajabu yeye alikamata watu mbalimbali na kusema kwamba ataunda kamati juu ya suala hilo. Tangu azungumzie swala hilo tayari kuna ukimya wa sintofahahamu hata mkuu wa TAKUKURU hajafuatilia suala hilo.

Tunachoona mitandaoni ni kuripoti taarifa za Sabaya tu hujuma ya bomba la mafuta pamoja na tani moja ya madawa ya kulevya yaliyolipotiwa mwezi uliyopita mambo hayo huwezi sikia yakiongelewa zaidi ya kusikia kesi ya Sabaya siku ya kuripoti mahakamani.

Je, kosa ni la wanandishi wa habari au kuna mtu yupo nyuma ya saga hiyo! Kwanini mkuu Takukuru hazungumzii kuhusu saga ya bomba la mafuta!

Naona kuna mahala hapapo sawa, Watanzania tuna kazi kubwa kupaza sauti sehemu tunapoona mambo hayaendi sawa tusikae kusifia tu hata tukiona mabaya tuyaseme bila kupepesa macho! Waandishi wa habari mna kila sababu ya kuhoji juu ya bomba la mafuta iwe kupitia kwa mkuu wa Takukuru au mkuu wa mkoa kujua ukweli wa jambo hilo.
 
Tulia, utapotezwa wewe, Sara Msafiri aliyekuwa mkuu wa wilaya ya kigamboni ndiye aliyevujisha hiyo project ya wakubwa, yupo Kibaha huko hutamuona tena akiongelea.

Kaa kimya kabisa, ushaona hata gazeti la Uhuru au Habari Leo au magazeti yana ripoti hiyo saga!issue ya malori kupanga foleni, bunge Lili simama hadi Pm akaenda kutatua, hii ngoma ngumu. Utasikia polisi wakisema tunawashikiria watu wahusika, haiwataj wala hatuwaoni.
 
Sitaki ushaidi mm,mada kama hizi nashauri zifungwe hapa JF.

Maana ukiongea ongea unaweza ukajikuta umetupwa katika daraja la Kigamboni bila nguo watu washafanya yao.
 
Modulator naomba uzi huu usiufute
 
Whistleblowers, zile NGO za kutetea ukandamizaji wa mashoga, nk wapo kimya tu.
 
Pengine ni halali labda hatujui utaratibu, labda wanalipa na kodi utajuaje?..biashara ya mafuta na unga zinafanana..tofauti ni moja imehalalishwa kwa muda
 
Kamati ya bunge inayohusika na nishati wanasemaje,hawajaomba mwongozo walijadili kwa dharula
 
Kamati ya bunge inayohusika na nishati wanasemaje,hawajaomba mwongozo walijadili kwa dharula
Hapo hata waziri mkuu hasemi kamwachia mkuu wa mkoa kule hakugusiki na hakuna anayeinua mdomo kupasemea hapo
 
Baadhi ya watanzania ni watu waajabu sana. Badala kulalamikia vitu muhimu kama vyakula na bidhaa mbali mbali kupanda bei, mafuta/petrol/diesel, ushuru wa magari, vifaa vya ujenzi, tiketi za ndege, kodi n.k. nyie mnakimbilia bandari na vifurushi vya data/kupiga simu. Yoye chuki na wivu kwa wawekezaji.. huu ujinga sijui utaisha lini!
 
Back
Top Bottom