Naogopa kuwa mama

Kuna kitu hujakitaja! Baba yako yupo au ni single mother? Kwa maangaiko haya hawezi kujiweka nadhifu kumvutia mumewe, hilo mosi! Pili, kwa umri ulionao huwezi msaidia mama yako inaonyesha jinsi gani kazaa kizazi zembe kitakachokuwa mzigo kwake mwenyewe nguvu zikiisha! Ndo maana hata wewe unaogopa kuolewa jinsi unavyomuona mama yako! Hopeless mama! Angetakiwa awe anawaamsha usiku saa10 mfanyekazi na kujiandalia mambo yao wenyewe na kuweka mambo ya nyumbani yaliyondani ya uwezo wao
 
Binadamu ameumbwa kufanya adaptation to current environment.
The day umebeba mwanao kuba hali flani itakuvaa ambayo itakufanya uweze kufanya kila kitu kwa ajili ya mtoto wako hata wawe kumi bila kuchoka.
Subiri nkupe ushuhuda, kipindi tuna date na wife, alikua mtu wa kulala vbaya mno. Yaan kwa mfano akiingia ndani ijumaa anaweza kutoka j3. Muda woote akimaliza tu kazi zake ni kitanda. Wakati mimi ndo kwanza siku inaanza. Tunaeza kula lets say saa moja usiku, yeye akimaliza tu anaenda kuzima. Mimi nasepa zangu narudi hata saa tano huko ndo nalala.
Lakn tulivopata tu mtoto, alibadilika ghafla. Yaani anaweza kuamka hata mara 9 kwa usiku mmoja. Atanyonyesha, mara kubadilisha diaper, mara kucheza na mtoto n.k.
Na asubuhi mapeema yuko live , mara apike chakula, sijui afue manguo, anijali na mimi na mavitu yote. No complains or anythng. Mtofo muda wote msafi, ana afya kubwa, nyumba iko standard n.k, vitu vyangu ameorganize, chakula on time na mashughuli yote.
So, hata kwako itakua hvyo. The joy of life inatokana na kuona uzao wako.
Kamwe usiogope, tena kama unaweza pata watoto mapema ili ufurahie kuona wakiwa wanakua.
Usitamani kua mwanaume, kuna vitu ambavyo tunapitia, ungeambiwa ungekimbia spidi ya fumanizi.
Kila la kheri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…