Naogopa kuwa mama

Naogopa kuwa mama

Natumai wazima wote,.

Iko hivi, kila siku zinavyoenda ndivyo ambavyo naogopa kuja kuitwa mama hapo baadae( Mungu anisaidie niondokane na hii hofu😓🥹🙏), hiii inatokana na lifestyle ambayo namwona mama yangu anaishi..

Huyu mwanamke sielewi hua anapumzika mda gani, yeye ndie mtu wa mwisho kulala kila siku. Yaani hawezi kulala kama kuna mtu bado hajaingia nyumbani, na anahakikisha kila mtu amekula amelala anafunga milango ndipo na yeye alale., Na hata akiingia kulala halitapita nusu saa anapita tena vyumba vyote kuhakikisha mmefunga madirisha, mmeshusha neti na mmejifunika vizuri ( anaweza akaamka hata mara 4 kwa usiku mmoja)..

Haitaishia hapo, Bado kuna sisi ambao inabidi asubuhi tuende kazini na wengine shuleni, wanaoamka usiku kusoma na wanaoamka kusali, kila mtu anamtajia mda wake wa kumwamsha hajawahi kukataa wala kupitiliza kutuamsha, always anakua on time… , Sijawahi kushuhudia ni saa ngapi ameamka ila kila tukiamka asubuhi tayari tunamkuta akiwa macho, kashafanya usafi na kashapika chai tunakunywa tunamwacha Nyumbani,. Hatujawahi kuona au kushuhudia akilala mchana, Labda itokee anaumwa ( Napo ni mara chache sana ).. Sijui hua anapumzika mda gani

Hajawahi kuishi na msaidizi wa kazi maisha yake yote, lakini hakuna aliyewahi kufua, kudeki , kupika, kuosha vyombo wala kufagia. Sio kwamba hatutaki kumsaidia Hapana, ni kwamba hatujawahi kuona uwanja ukiwa mchafu, vyombo vichafu na mda wowote ukirudi nyumbani unakuta chakula tayari na usafi wote ushafanywa na nguo zote ziko kambani zinakauka,,..

Licha ya hayo yote vilevile bado hajawahi kuacha kwenda kazini na shughuli zake nyingine zote za ujasiriamali hajawahi kuacha kufanya, hajawahi kuacha kwenda kwenye jumuiya wala kanisani hata jumapili moja, na kwenye dharura zote iwe hospitali au kikao chochote atakachohitajika mzazi awepo basi ni yeye ndio atakuwepo tena kwa wakati.. Na sijawahi kumwona akilalamika, akinung’unika wala akimlaumu mtu kwamba hakuna anayemsaidia kazi hata siku moja,..

Haya maisha yake yananiogopesha na yananifanya niogope hata kuwaza jinsi nitakavyoishi na watoto wangu huko mbeleni., Sometimes i wish ningekua wakiume labda ningeishi tu kama baba yangu anavyoishi😓😓😓 ( Em assume mtu anafanya haya maisha yake yote)
Anatengeneza kizazi kibovu sijawahi ona hapo ndipo inapopata hofu yawezekana hujui kupika, hujui kufua, hujui kudeki na nk hivi utaishije na mume hofu yako kaijenga mzazi mwenye bidii ya kazi usiku na mchana

Samahi lkn umeongelea mama tu baba vipi
 
[emoji12][emoji12]Nasubiria ushuhuda tu mengine yabaki historia, hakuna jambo gumu la kumshinda binadamu limitations tunajiwekewa wenyewe kwa kuamini au kwa kujinenea siwezi

Kuna andiko takatifu linasema hivi "uzima na umauti umo ndani midomo yetu" ukiongea uzima utaishi na ukiongea mauti hutaishi kwahiyo weka umakini katika kila neno litokalo kinywani mwako, badili mindset utaishi katika kufikia hatima yako na utashangaa
Amen, ubarikiwe sana mkuu kwa ushauri mzuri
 
Anatengeneza kizazi kibovu sijawahi ona hapo ndipo inapopata hofu yawezekana hujui kupika, hujui kufua, hujui kudeki na nk hivi utaishije na mume hofu yako kaijenga mzazi mwenye bidii ya kazi usiku na mchana

Samahi lkn umeongelea mama tu baba vipi
Baba yangu ni mtu ambaye yuko busy sana.. Lakini ndio provider wa kila kitu nyumbani
 
Hoja kuu ni woga wa wewe kuwa mama, majukumu makubwa aliyonayo mama, muda wa yeye kupumzika, kuhudumia watu wa nyumba yake kwa kila kitu.

Ila hoja nyingine inakuja, how come watu wa nyumbani wasimsaidie mama kazi? Mama analea watu wa aina gani asiowapa majukumu.

Anyway kila familia ina namna yake ya malezi.
 
Kuna kitu hujakitaja! Baba yako yupo au ni single mother? Kwa maangaiko haya hawezi kujiweka nadhifu kumvutia mumewe, hilo mosi! Pili, kwa umri ulionao huwezi msaidia mama yako inaonyesha jinsi gani kazaa kizazi zembe kitakachokuwa mzigo kwake mwenyewe nguvu zikiisha! Ndo maana hata wewe unaogopa kuolewa jinsi unavyomuona mama yako! Hopeless mama! Angetakiwa awe anawaamsha usiku saa10 mfanyekazi na kujiandalia mambo yao wenyewe na kuweka mambo ya nyumbani yaliyondani ya uwezo wao
Baba yupo , naye yuko busy sana. Ila ndio provider wa kila kitu nyumbani.. Tatizo n kwamba hapendi kusaidiwa
 
Hoja kuu ni woga wa wewe kuwa mama, majukumu makubwa aliyonayo mama, muda wa yeye kupumzika, kuhudumia watu wa nyumba yake kwa kila kitu.

Ila hoja nyingine inakuja, how come watu wa nyumbani wasimsaidie mama kazi? Mama analea watu wa aina gani asiowapa majukumu.

Anyway kila familia ina namna yake ya malezi.
Mama yangu hapendi kusaidiwa.. Baba kashaleta wasaidizi hadi amechoka saizi, hapendi kusaidiwa kabisa
 
Back
Top Bottom