Naomba kuelezwa : Iran akimiliki Nuclear Israeli inamhusu nini?

Mambo yanakuwa magumu na magumu.

Hivyo, uvamizi wa Israel ni wa uongo.
Sasa ulitaka Iran awe na silaha za nuclear ndipo Israel ivamie? Hujui ule usemi hi heri kuzuia kuliko kutibu?
 
Nimekuelewa....but this has nothing to do with the lefties and right.

Nataka kujua Kama Israel anamiliki nuclear kwanini anakataa Iran awe nazo?
Kwa sababu Israel hana shida na wasio na imani kama yake ila Iran ni nchi ya kigaidi.Itazitumia kuifuta Israel na nchi za kikristo.
Hawashindwi kusema takbir kisha wanalishusha pale Rome.

Hao wehu hawapaswi hata kumiliki gobore.

Hakuna ugonjwa unavuruga kichwa kama kuwa extrimist wa dini.
Fvck all religions
 
Ndio ushangae ndugu yangu. Hii dunia hakuna haki kabisa. US, Israel wana nyuklia ila wameenda kumpiga Iran na hiyo nuclear hata hana. Tuliambiwaga hata Iraq ana nuclear akapigwa wakamuua Saddam Hussein bure tu.

In fact hiyo ni sababu feki waliyoitunga ila in reality hawautaki uongozi wa Iran wanataka viongozi wao wawe kama kina Salman na wafalme wengine wa nchi za kiarabu ambao ni wanafiki wamewekwa kwa maslahi yao
 
Ukisikia jirani yako anafanya mipango ya kukukodia majambazi ili wafute familia yako kisa mgogoro wa shamba utafanyaje au serikali itachukua hatua gani?
 
Kinachomponza Iran ni kufadhili vikundi vya jihadi kujaribu kuifuta Israel ili wabaki na Gaza matokeo yake anawaponza hata hao wa Palestine, na sasa wanahangaika kung'oa mzizi
 
Kwa hiyo issue hapa ni nani mwenye nguvu!
Mshangao wangu unaenda mbali kwanini mataifa mengi hasa G7 yanamuunga mkono Israel sasa !

Nuclear is a world threat, Taifa lolote lenye akili litachangia vita za kichaa yeyote anayewaza nuclear
 
.well
 
Kwa hiyo sheria za umoja wa mataifa zinaruhusu Kenya akianza kutengeneza nuclear Tanzania tumvamie?
Jibu ni ndio iwapo ndoto yake ni kutufuta kwenye uso wa dunia na iwapo tutajiridhisha kuwa hayupo sawa kichwani.
 
Sina uhakika kama nchi nyinginezo zinazomiliki nuclear weapons sipo sehemu bayana... Kiasi kwamba hata sisi watoto wa Kizimkazi Tunaweza fanya matembezi ya kitalii
Tafuta point ya Israel kuipiga Iran, utakutana na hy point
 
Haya Ni Mambo Mazito Ya Intelligence
Machoni Ni Ya Kawaida Ila Ndani Mazito
Tanzania Home Ground, Sheria Inaruhusu Siasa Za Vyama Vingi Ila Wapo Wanaokatazwa Na Chama
 
Kweli kwa swali hili, umeboa mkuu
 
Ukiruhusu nchi inayo ongozwa na Waislam wenye itkadi kali wamiliki nyuklia ujue dunia sio salama. Huo utawala wa imani kali wa Iran waliapa kuondoa Israel kwenye ramani ya dunia, ndio maana haruhusiwi
Na ninavyowajua hao wehu trust me hawataishia Israel.Nchi zote za Kikristo zitakua hatarini.
 
Irani anafadhili vikundi vingi ambavyo ni tishio kwa Israel,fikiria kama wanashambulia kwa makombora ya kawaida cku wakipata mzigo itakuwaje?
 
Dunia nzima wanafahamu Iran alikuwa hataki kutengeneza Nuclear Boom angetaka angeisha kuwa nayo zamani.

Wao hawataki Iran iendelee sababu akiwa nayo watapiga hatua kubwa sana kwenye maendeleo.

Kwa sasa wamemchokoza nadhani atakuwa nayo tu siku za mbele time itaongea
 
Ni kama umkabidhi kichaa kisu kwenye sherehe
 
Nuclear facilities za Iran zote zipo zinafatiliwa na International Atomic Energy Agency (IAEA) na mpaa jana wamesema Nuclear facilities zao hakuna dalili wanataka kutengeneza Nuclear Boom. Wakati Israel anazo na kisheria hatakiwi kuwa nazo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…