Naomba kuelezwa ni nani Mwingine zaidi ya Dkt Tulia na David Kafulila amewahi kurejesha Chenji Serikalini?

Unakulaje pesa ya Mradi?

Sikiliza kidogo, Kwenye habari tunavitu viwili,

1. Tuna News
2. Tuna story

Mfano Mtu kumng'ata Mbuwa ni NEWS
but Mbwa kumng'ata Mtu ni STORY

Hivyo; Kafulila na Tulia kurudisha chenji ni NEWS.
Ila kiongozi mwingine yoyote kutekeleza miradi Kwa mujibu ya BOQ na kuikamilisha hiyo ni Story.

Kwanini ni story ni kwasababu ni jambo la kawaida la Kila siku.

Kwanini ni News ni kwasababu Sio jambo la Kawaida.

Maarifa ni kitu Cha muhimu sana kwenye maisha.
🤑🤑🤑🤑
 
Ww lucas ni mtoto mdgo sana mm mzee wangu alirudisha 400M zilizobaki kwenye ujenzi wa ...... simtaji jina wala kazi yake ila na record ipo mpaka leo ila ameshastaafu
 
Nakumbuka pia Marehemu Peter Kushoka aliyekuwa GM wa UDA alipokwenda kufunga deal ya ununuzi wa zile basi za Ikarus alipewa commission ya basi moja lile lilikuwa la rangi ya blue aliliingiza kwenye fleet ya UDA. Angekuwa hawa wa kula kaarwa urefu wa kamba zao angeomba apewe dollars zake akunje mfukoni.
 
Mimi sifadhiliwi na mtu yeyote yule ndugu yangu. Tuache uoga wa kukaa kimya bila kuwatia moyo na kutambua mchango wa watu wazalendo, wachapakazi, waaminifu, waadilifu kwa Taifa letu. Tusiache wakashambuliwa na waovu bila kuwasemea.tutakuwa tunawakatisha tamaa na kuwapa ushindi mafisadi
Thread nne mtu mmoja ambaye watendaji wanajua kabisa baba ufanisi is wrng

Uko ma politics kila wakati hata kwenye issue za kitendaji

Adui mkubwa wa maendeleo ya kisekta ya Tanzania ni watu wanaoleta siasa kila sehemu

China is succeeding because imeacha kufungamqnisha siasa na utendaji

You are not helping
 
Ni watumishi waandamizi waliopewa dhamana ya kusimamia pesa za umma.lakini kwa Tamaa wanaamua kukiuka viapo vyao na kufuja pesa za umma.
Hapa unammpiga mh rais kwamba hawasimamii vizuri

Kuna sehemu una shida dogo… too many unforced errors in your game plan
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kuna watu ni WAZALENDO kwelikweli,ni wasafi sana, ni waaminifu waliopitiliza,ni wacha Mungu na wenye Hofu ya Mungu sana na wana uchungu mkubwa Sana na Maisha ya watanzania. Miongoni mwa watu hao basi ni hawa watu wawili ambao wamewahi ishitua Tanzania na kugusa mioyo ya mamilioni ya watanzania.

Ngoja niwape story bila kuwachosha kuelekea wikendi. Ilikuwa hivi Mheshimiwa Chuma Mwenyewe David Kafulila akiwa katibu Tawala Mkoa wa Songwe alipewa Billion Sita kujenga mpaka kumaliza ujenzi wa Makao makuu ya mkoa wa Songwe yanayopatikana katika kata ya Mlowo Eneo la Nselewa. Lakini Chuma kwa kutumia mfumo wa Force Akaunti katika ujenzi wa Makao makuu hiyo hakumaliza pesa hiyo.

Ambapo mpaka jengo linamalizika na kukamilika Chuma Kafulila akabakisha Chenji ya Karibu Billion Mbili.Siku hiyo anasoma taarifa hiyo mbele ya waziri mkuu mwaka 2020 Ofisi za makao makuu ya mkoa ,watu wote walibaki Midomo wazo na kustaajabu Uzalendo alio uonyesha CHuma Kafulila. Nakumbuka siku hiyo alisoma taarifa hiyo kwa umakini na utulivu wa hali ya juu sana. Na kwa bahati nzuri mimi mwenyewe nilikuwepo siku hiyo na nilikuwa karibu sana eneo la Tukio na nilikuwa nimesimama jirani na Mheshimiwa David Silinde ambaye siku hiyo alipewa nafasi ya kuzungumza pia. Nilikuwa jirani maana nilikuwa ni kiongozi wakati huo kwenye jumuiya ya vijana yaani UVCCM.

Siku hiyo nakumbuka wakati tunarejea majumbani Chuma Kafulila alikuwa ni gumzo sana tena sana midomoni mwa watu ,kwa namna alivyo onyesha uzalendo wa kipekee na uaminifu wa kiwango cha juu sana.

Mwingine ni Dada wa Taifa na Rais wa IPU na msomi Nguli wa sheria kuwahi kutokea nyanda za juu kusini.huyu sina sababu ya kueleza mengi maana mnakumbuka Billion kadhaa alizorejesha serikalini baada ya kubana matumizi kule Bungeni.

Nimeamua niandike haya kueleza kuwa kuna watu ni waaminifu na wazalendo sana,ambao miongoni mwao ni hawa niliowataja hapa.

Jiulizeni ndugu zangu watanzania ni mara ngapi mmesikia kuwa mradi fulani Umepelekewa mamillioni kwa mamillioni ya pesa, lakini pesa zimekwisha na mradi haujafika hata nusu na hela haieleweki iliko kwenda? Mara ngapi mmesikia miradi kama vile ujenzi wa shule au kituo cha afya au barabara au usambazaji wa maji unakatu umekwama kukamilika kwa kuwa tu mapesa yaliyotolewa yameliwa na kuisha kabla hata mradi haujafika hata Nusu yake? Hamjaona haya wanapofanya ziara mawaziri wetu huko mikoani wakisikitika mpaka wanatamani kulia baada ya kukuta pesa zimeliwa? Hamjaona waziri mkuu wetu akiongea kwa uchungu na kwa huzuni na kuagiza ukaguzi na uchunguzi ufanyike kubaini waliotafuna pesa?

Lakini vyuma hivi Mheshimiwa Dkt Tulia pamoja na David Kafulila vilirejesha Chenji ya mamilioni kwa mamilioni,pesa ambazo wangeamua kuzichepusha kutunisha akaunti zao benki. Lakini kwa uzalendo wao wakasema hapana acha turejeshe pesa hizi ili zikajenge vituo vya afya ,shule, usambazaji wa maji safi na salama,umeme, barabara n.k.

Mwisho niseme tu kuwa mimi ni mzalendo na nimekuwa na tabia ya kutetea na kuwasemea wazalendo wote. Mimi sioni haya wala aibu kumtetea na kumsemea mzalendo bure kabisa pasipo malipo ya aina yoyote ile wala kupewa hata mia tano tu ya Vocha. Nataka Taifa liwe na utamaduni wa kuwaunga mkono wazalendo na wachapakazi wa Taifa letu ,tusiache wakachafuliwa na kushambuliwa na wabaya .ndio maana kuna watu awali wakasema mara nalipwa kwa uchawa ,wengine wakasema nalipwa na Mheshimiwa Dkt Tulia,wengine wakasema Nalipwa na Mwamba Mwenyewe Paul Makonda na sasa wengine wanasema nalipwa na Chuma Kafulila.ila hawasemi nalipwa shilingi ngapi na kwanini nilipwe na kila mtu na na kwa watu wote hao? Na hawasemi kwamba wao wanalipwa na nani kuchafua watu humu jukwaani na mitandaoni.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Siasa za hivi haziwezi kutufikisha popote.

Soma ulichoandika halafu ihoji nafsi yako. Unaposema wengeamua, wangetunisha mifuko yao ni wazi kuwa unasema nchi yetu ina mifumo mibovu. Pili, force account imeumiza sana wakandarasi.

Kojoa ukalale
 
Tulia ni mwadilifu sana labda abadilike Kafulil pia anarekodi nzuri
 
Back
Top Bottom