Naomba kuelimishwa; matrillion ya pesa yanayokusanywa kwenye kodi ya ‘Fuel marking’ yanaenda serikalini au kuna mtu anabugia asali?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Wakati najaribu kutafuta ‘uchawi’ unaotumika kufanya bei ya mafuta ambayo gharama zake zote hadi kuyafikisha bandarini Dar es Salaam ni 1,116/= kuuzwa kwa bei inayofika hadi 3,500/= baadhi ya mikoa (tofauti ya 2,500/= kwa lita), nilikutana na ‘kodi’ inaitwa ‘Fuel marking’

Katika kujaribu kudososa hii ni kodi ya aina gani, nikaja kugundua kwamba ‘fuel marking’ ni kitendo cha kuweka kemikali zenye vinasaba maalum kwenye mafuta ili kutofautisha mafuta yaliyolipiwa kodi na yake ambayo hayajalipowa kodi.

Sasa kucheki kiasi cha pesa kinacholiwa kwa lita kwa ajili ya kiwela hivyo vinasaba, nikakuta kwamba ni matrillion y pesa tunalipa kwa kila lita tunayonunua.

Sasa naomba kuelimishwa, haya matrillion ya ‘fuel marking’ yanaenda serikalini au kuna mtu analamba asali hapo kwa kubugia? Ni nani anahusika na hili zoezi la ‘Fuel marking’?
 
Kama kiasi kinacholipwa kwa ajili ya hiyo fuel marking ni kikubwa basi kilitakiwa kiondolewe.
Mafuta yenyewe yanaagizwa kwa pamoja, yakiingia bandarini ina maana wanayaona na kutoza kodi Kuna haja ya kuyawekea alama wakati yanapoingilia panajulikana? Tuelimishane jamani
 
Sasa kuna yale ya Transit labda ndio wanaogopa, kwamba mtu akasema anapeleka Rwanda halafu yakaishia Lake oil, ila hizi pesa zinaenda serikalini au kuna mtu binafsi analamba asali hapo, ni trillions and trillions!!
 
Kutakuwa kuna kikampuni chenye ubia na wakubwa kama kile cha TICTS kule bandarini. Hapo hela za Wadanganyika zitakuwa zinapigwa tu. Hata ulalamike vipi, unakuta mkataba hausitishwi.

Nchi ngumu sana hii.
 
Tusitoe shutuma kwanza, tuulize tu, hii kazi inafanywa na serikali au kuna kikampuni binafsi kinalambishwa asali hapo?! Tuambiwe!
 
Sasa naomba kuelimishwa, haya matrillion ya ‘fuel marking’ yanaenda serikalini au kuna mtu analamba asali hapo kwa kubugia? Ni nani anahusika na hili zoezi la ‘Fuel marking’?
(TBS) Tanzania Bureau of Standards ndio wauzaji wa hivyo vinasaba.....,,,baada ya hapo sijafahamu nini kinaendelea....

Hilo tu ndio nafahamu,,,
 
Wanamuuzia nani sasa? Serikali inawezaje kujiuzia yenyewe vinasaba? Nani analamba asali hapo sasa? Pia TBS ananunua kwa nani hivyo vinasaba, maana najua hazalishi hivyo vinasaba. Hizi sarakasi zinatugharimu waTz trillions, nani analamba asali ya hivyo vinasaba?
 
Wanaweka uchafu kwenye mafuta

Hizo additives hazina viwango sometimes mafuta yanakuwa na layers kabisa sisi watu wa porini tunaona kwenye madumu.

Labda wataalamu watuambie vinginevyo lakini in a long run tutaona shida katika vyombo vinavyotumia haya mafuta.
 
Wakati najaribu kutafuta ‘uchawi’ unaotumika kufanya bei ya mafuta ambayo gharama zake zote hadi kuyafikisha bandarini Dar es Salaam ni 1,116/= kuuzwa kwa bei inayofika hadi 3,500/= baadhi ya mikoa (tofauti ya 2,500/= kwa lita), nilikutana na ‘kodi’ inaitwa ‘Fuel marking’

Katika kujaribu kudososa hii ni kodi ya aina gani, nikaja kugundua kwamba ‘fuel marking’ ni kitendo cha kuweka kemikali zenye vinasaba maalum kwenye mafuta ili kutofautisha mafuta yaliyolipiwa kodi na yake ambayo hayajalipowa kodi.

Sasa kucheki kiasi cha pesa kinacholiwa kwa lita kwa ajili ya kiwela hivyo vinasaba, nikakuta kwamba ni matrillion y pesa tunalipa kwa kila lita tunayonunua.

Sasa naomba kuelimishwa, haya matrillion ya ‘fuel marking’ yanaenda serikalini au kuna mtu analamba asali hapo kwa kubugia? Ni nani anahusika na hili zoezi la ‘Fuel marking’?
Ungekuwa una nia nzuri sasa hivi ilitakiwa uwe mahakamani unafunga shtaka la kitengo hicho,sasa hapa umekosea kafungue kesi kabisa tuione gazeti la serikali na usiifungue peke yako, Afrika ni mahalo pagumu Sana kuishi Bora ufungue kesi hiyo utaweka legacy,sababu nimemwona mnufaika mmoja yuko kuhiji na kanzu yake nyeupe hebu chukua maamuzi magumu please.
 
Back
Top Bottom