Naomba kufahamishwa dawa nzuri ya kuua Panya, unga mweusi umedunda

Naomba kufahamishwa dawa nzuri ya kuua Panya, unga mweusi umedunda

Ni miezi sasa panya wamekuwa wananisumbua sana! Nimejaribu dawa za unga mweusi zinazouzwa dukani zimeshindwa, zile za pellets ndiyo hamna kitu!!

Panya hawa huingia ndani mwangu kuanzia jioni na hunichachafya hadi asubuhi! Nimewafuatilia naona wanatoka kwa jirani

Kwangu kuna fence ajabu wanaivuka na kuingia na kutoka! Nikiri ninaishi mazingira ambapo watu wakivuna mazao wanayahifadhi wenyewe tena wengine hufanya hivyo kienyeji, ndiyo maana hata panya wana afya kwa sababu hupata mlo kamili!

Imefikia hatua kwa kuwa huwa hata wanakimbizana wakiwa juu, panya akikudondokea maumivu yake ni kama umetupiwa jiwe la manati!

Naombeni msaada wa dawa nzuri ili niwateketeze!!
Fugaa paka panya wote watakimbia
 
Niku deal nao aggressively;
yaani unanunua sumu ya panya- hata hiyo ya unga mweusi ni nzuri tu ila uweke kidogo kwenye chakula chenye harufu kali kuizidi, kama vile dagaa waliokaangwa, ufuta au karanga zilizokaangwa, weka kiasi kidogo tu na changanya vizuri.. ukiweka nyingi hawagusi ng'oo. Pia baada ya kutega sumu hakikisha unafuta maji yote chini au vyombo vya wazi, na mabaki ya vyakula holela yote yaondolewe.

Aidha, kama umezijua njia zao pia weka mitego ya kunasa (ulimbo) au mtego wa panya wa kufyatuka. Tegesha ki ufundi kabisa. Akinasa mmoja tu akalialia swiii swiiii wenzake watahama na itachukua muda kuwaona.
 
Niseme tuuu hakuna Kiumbe Mwenye akili na mjanja Kama Panya.
Akishagundua Unamtega haji na wala Humuoni,
Anakuja kwa timing sanaa na Anakula anachokula…Humkamati kizembe
 
Aaante kwa ushauri nitaufanyia kazi!Kuhusu unga wanakula unga upi?Maana nilijaribu kutumia sembe hawakula au nitumie unga wa muhogo?
indocine kuipata ni tabu hata kama ipo wanaweza kukuficha tz haiuzwi kihalali kwa hio kuwa makini namna wa kuipata...angalia chakula walichokula kama nyanya nyunyizia pale walipokula watarudi kesho au baadae katakata nyanya weka wanaipenda sana uzuri wanakufa hadharani miguuu huishiwa nguvu ikimkolea unaweza mshika kwa mkono...inaua taratibu ila wataisha....Hio ndo Dawa yangu pigo la mwisho.
 
Nenda pharmacy kanunue vidonge vinaitwa indomethacin changanya na unga wale

Sorry hivi vidonge Unachanganya na nini?
Au ni vidonge peke yake tuuu?
Vinapatikana Pharmacy au maduka ya kilimo na Mifugo?
Nataka nijaribu na hii!
 
Sorry hivi vidonge Unachanganya na nini?
Au ni vidonge peke yake tuuu?
Vinapatikana Pharmacy au maduka ya kilimo na Mifugo?
Nataka nijaribu na hii!
phamacy..unachanganya na nyanya nyunyuzia ukiwa umeshaikata....
 
Sorry hivi vidonge Unachanganya na nini?
Au ni vidonge peke yake tuuu?
Vinapatikana Pharmacy au maduka ya kilimo na Mifugo?
Nataka nijaribu na hii!
Pharmacy zote vinauzwa shilingi elf moja vipo kumi,ni vya unga vipo ndani ya kava la plastic
 
Attachments

  • Screenshot_20231004-080926.png
    Screenshot_20231004-080926.png
    212 KB · Views: 20
Binafsi nilihangaika saana kipindi fulani kukabiliana na panya hawa wa kisasa lakini matokeo hayakuwa kama nilivyotarajia.

Kila mchangiaji ameandika ushauri wake hapo juu.

Kwangu mimi dawa ya panya ninayoiaminia ni ''PAKA''

Jaribu hata kuazima PAKA kwa muda kama huwezi kumfuga, watakaosalia watahama
 
Kutumia Madawa Ni kupoteza Muda

Kuna mitego mikubwa size Kama ya begi la kusafiri lile la kuburuta chini. So nimitego ambayo wakiingia humo wahatoki inaweza trap hata panya 20 ukawakutamo humo asubuhi. Nenda YouTube ukatizame ni namna gani it works
 
Mkuu, dawa ya panya ni paka tu. Paka hufia mafichoni sana na hunuka mno. Kumuua kwa sumu ni kujitafutia tatizo. Paka ndiyo kila kitu.
 
Ni miezi sasa panya wamekuwa wananisumbua sana! Nimejaribu dawa za unga mweusi zinazouzwa dukani zimeshindwa, zile za pellets ndiyo hamna kitu!!

Panya hawa huingia ndani mwangu kuanzia jioni na hunichachafya hadi asubuhi! Nimewafuatilia naona wanatoka kwa jirani

Kwangu kuna fence ajabu wanaivuka na kuingia na kutoka! Nikiri ninaishi mazingira ambapo watu wakivuna mazao wanayahifadhi wenyewe tena wengine hufanya hivyo kienyeji, ndiyo maana hata panya wana afya kwa sababu hupata mlo kamili!

Imefikia hatua kwa kuwa huwa hata wanakimbizana wakiwa juu, panya akikudondokea maumivu yake ni kama umetupiwa jiwe la manati!

Naombeni msaada wa dawa nzuri ili niwateketeze!!
Indosidi changanya na pilton Kazi imeisha,wanakula na wanakuga tatatibu na hawajui chanzo chan kufa ni nini
 
Dawa nzuri ya panya ni ile ya tambi tambi ile wanaita Rat Cide.
 
Back
Top Bottom