Naomba kufahamishwa dawa nzuri ya kuua Panya, unga mweusi umedunda

Naomba kufahamishwa dawa nzuri ya kuua Panya, unga mweusi umedunda

Aliyeandika kuhusu cement jinsi inavyoua panya naomba atoe ufafanuzi Kwa undani kidogo, maana msimu wa kilimo Wananisumbua sana shambani
 
Hiyo ni mitego ya YouTube Tu Babu haifanyi kazi kwa panya wakiswahili hawa

Panya wa siku hizi ni wajanja balaa, ukiweka sumu ambayo inaharufu isiyo ya Kawaida hawali....

Ukiwatega kwa kuweka sumu kwenye pande kubwa la nyama/samaki kitu ambacho sio kawaida kwa pande la nyama/samaki kuwekwa kizembe zembe,wanajua... hawali....

Ukiwatega kwa mtego wa kuingia au wa kufyatuka ili wanase, hawausogelei....

Ukifuga paka, paka wa siku hizi hawawindi tena kama paka wa zamani, nimeona sehem nyingi hii, yaani paka hawali tena panya siku hizi

Njia sahihi ya kuwaondosha ni kutumia dawa ya indocin inapatikana pharmacy, hii dawa uzuri wake ni haina harufu kabisa kwahyo hawawezi tambua uwepo wake kwenye chakula

Kata nyanya au karoti vipande vidogo sana kiasi kwamba hata ukikiweka sehem wanajua kimedondoka bahati mbaya Tu (ukiweka kipande kikubwa wanajua kama wametegwa hawali). Utaleta mrejesho hapa baada ya kutumia hii

Uzuri wa hii dawa, panya wanakufa bila kutoa harufu (hawaozi) Yani utakuwa unawakuta Tu wamekufa hakuna harufu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumia maji na mafuta ya Mwamposa!
Ni miezi sasa panya wamekuwa wananisumbua sana! Nimejaribu dawa za unga mweusi zinazouzwa dukani zimeshindwa, zile za pellets ndiyo hamna kitu!!

Panya hawa huingia ndani mwangu kuanzia jioni na hunichachafya hadi asubuhi! Nimewafuatilia naona wanatoka kwa jirani

Kwangu kuna fence ajabu wanaivuka na kuingia na kutoka! Nikiri ninaishi mazingira ambapo watu wakivuna mazao wanayahifadhi wenyewe tena wengine hufanya hivyo kienyeji, ndiyo maana hata panya wana afya kwa sababu hupata mlo kamili!

Imefikia hatua kwa kuwa huwa hata wanakimbizana wakiwa juu, panya akikudondokea maumivu yake ni kama umetupiwa jiwe la manati!

Naombeni msaada wa dawa nzuri ili niwateketeze!!
 
Kama uko Dar,nenda pale usalama sokoni Magomeni, kanunue mitego yako miwili...ukitega ile ndani ya siku 2 wote wanaisha.
 
Acha izo mshana, hawa ni panya wafata chakula tu
Kwanini mnakuwa na vichwa vigumu kuelewa? Soma tena nilichoandika soma taratibu na kwa umakini halafu soma alichoandika mleta mada[emoji1541][emoji1541][emoji1541]

Nikiri ninaishi mazingira ambapo watu wakivuna mazao wanayahifadhi wenyewe tena wengine hufanya hivyo kienyeji, ndiyo maana hata panya wana afya kwa sababu hupata mlo kamili!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni miezi sasa panya wamekuwa wananisumbua sana! Nimejaribu dawa za unga mweusi zinazouzwa dukani zimeshindwa, zile za pellets ndiyo hamna kitu!!

Panya hawa huingia ndani mwangu kuanzia jioni na hunichachafya hadi asubuhi! Nimewafuatilia naona wanatoka kwa jirani

Kwangu kuna fence ajabu wanaivuka na kuingia na kutoka! Nikiri ninaishi mazingira ambapo watu wakivuna mazao wanayahifadhi wenyewe tena wengine hufanya hivyo kienyeji, ndiyo maana hata panya wana afya kwa sababu hupata mlo kamili!

Imefikia hatua kwa kuwa huwa hata wanakimbizana wakiwa juu, panya akikudondokea maumivu yake ni kama umetupiwa jiwe la manati!

Naombeni msaada wa dawa nzuri ili niwateketeze!!

1686894627539.png
 
Wanapatikana wapi,mbona siwafahamu!!Msaada tafadhali
Nenda malia asili kuna wataalam pale watakupatia wauzaji.

Zamani kuna mzee mmoja 9marehemu sasa) aliyekuwa mmoaja katika waanzilishi wa NCR akiitwa Kassim Maguto alikuwa akiwauza kule Mlandizi, unaweza kuulizia kama warithi wake wamerithi hiyo kazi. Nnaongelea miaka mingi nyuma.

Nafahamu Chalinze na vijiji vya karibu ya hapo kuna wataalamu wa nyoka wengi, unaweza kuulizia pia.
 
Mkuu Tafuta Paka,
Awe mdogo mdogo, sio haya makubwa.
Paka akilia tui panya wanakimbia achilia mbali kukamatwa.
 
Back
Top Bottom