Naomba kufahamishwa kwa kina kuhusu picha maarufu ya Monalisa

Duuh
 
Mi nadhani hii picha ya kawaida ila wanajaribu kuipa historia na maana...
Unajua ukipata jibu kwa kutumia wrong approach nd ukajaribu kuprove jawabu kwa kitumia wrong approach utaona jawabu ni sahihi...
Let's say mzungu angeamua kusema pie iwe 5.4 au circle iwe na 500 degrees na kisha akaprove tungekubali ulimwengu mzima kuwa definetely wako sahihi.
Aliechora picha hakusema yote yanayozungumzwa ila sema kwa kuwa wameamua kuipa maana wanayotaka wenyewe ndo haya yanambazwa.
Nan kasema wapo watu wawili hapo,mara mtoto wa yesu,mara mke,wake mara alikuwa kipenzi cha mchoraji. Na hawa wanasaynsi wakiamua kukuonesha kuwa pana watu wawil hapo watakuonesha kwa kuwa wameamua.
Kuna hoja imezungumzwa hapa kuwa inahusishwa na Uzao wa Yesu,mm naona km wanajaribu kuuchafua ukristo,ili ionekane mafundisho yake sio ya kweli.
Tuache kuongea probabilities sababu mchoraji hakusema lolote juu ya mchoro wake ni watu wameamua kuipa maneno.
 
Acha uongo mkuu Yohana ni mwanafunzi wa Yesu soma jinsi alivyowachangua wanafunzi wake acheni kuweka vitu ambavyo havijaandikwa kwa Biblia. Tatizo mnatumia Lugha ya moja kwa moja mnashindwa kuitafasiri Biblia. Yesu alipokua msalabani alimkabidhi Mama Bikira Maria mikono Yohana na Yohana mikononi mwa Bikira Maria na sio kwa Magdalena. Mama Bikira Maria ni mama wa kwetu sote kutokana na Yesu kumkabidhi kwetu kutumia Yohana. Acha mkuu kueneza uongo uliza viongozi au waumini wa madhehebu mbali mbali kwa kuja ukweli mkuu. Kwenye mwamba Kanisa Kantoliki la Mitume lishajengwa mtafurunguta lakini wapi. Aksante mkuu.
 
Samahani mkuu nimeuliza swali hapo juu ila sijajibiwa nahaisi wewe unaweza nijibu, nimeuliza kuwa je yesu alikuwa hatakiwi kuwa na mtoto? Maana naona ndipo mada ilipohamia kwa sasa.
 
si Mariam *****... Yasemekana Mariam mwingine na ametajwa kwenye bible hata wanafunzi Wa Yesu walikuwa na wivu nae na walilalamika why anamkiss kwa muda mrefu na Mara kwa Mara... Pia yasemekana ni mkewe na ile harusi aliyo tengeneza pombe kimiujiza ilikuwa harudi yake... Kwa wana historian na pia inapatikana kwenye kitabu cha injili ya Barnaba... Nimesoma soma tu kwenye vyanzo mbali mbali
 
wewe ni bonge la mjinga yaani mambo ya dini kama huelewi ati waulizwe viongozi Wa dini???? Wewe biblia hujui kusoma? Walioandika ili nyie msome muelewe.. So usipoelewa ukamuilize mwingine aliyesoma ati akueleweshe? Tumia bongo
 
wewe ni binge la mjinga yaani mambo ya dini kama huelewi ati waulizwe viongozi Wa dini???? Wewe biblia hujui kusoma? Walioandika ili nyie msome muelewe.. So usipoelewa ukamuilize mwingine aliyesoma ati akueleweshe? Tumia bongo
Sasa mkuu kama hawezi kuielewa anapoisoma kwanini tusimpatie njia mbadara na hilo ni ujinga?
 
Haijaandikwa popote kwenye Biblia kuwa Yesu alioa. Haya mambo lazima ufike ukomo usiende beyond thinking. Munamchukulia Yesu kama mwanadamu wa kawaida kama sisi.
Mkuu acha kuifunga akili yako kwa kigezo cha imani. Biblia ina vitabu 66 wakati kuna vitabu vingi sana vimeondolewa mpaka kubaki idadi hiyo aliyeviondoa si Mungu bali ni binadamu kwa matakwa yake.
Moja kati ya vitabu vilivyoondolewa ni kitabu cha "gospel of peter" na "gospel of Marry magdalen"
Vitabu hivi sio tu vinaonesha ukaribu wa Yesu na Marry bali vinaelezea maisha ya yesu akiwa kawa binadamu wa kawaida tena kijana wa kiyahudi.
Katika biblia ya kawaida hakuna kitabu kinachoelezea maisha ya yesu kama mwanadamu wa kawaida bali vinamuelezea katika hali ya uungu.
Hii ni moja ya kazi ya mfalme constantine ya kuunganisha upagani na ukristo.
Inabidi tutafte kujua kweli na si kuamini tuu kwa kutumia source moja ya biblia tena iliyochakachuliwa
 
Hivi vitabu vya Gospel of Peter na Magdalene vinapatikana wapi aisee?
 
Mkuu naomba kujua kama Maria mama wa Yesu pamoja na mume wake Yusufu walipata watoto/mtoto baada ya kumzaa Yesu. Na kama walimpata, huo ukoo unajulikana kwa sasa ni akina nani? Natanguliza shukrani
Inaaminika Mariam alizaa watoto wengine na Yusufu, kati ya watatu au wanne.
 
Lini Yesu alitengeneza pombe kimiujiza?

Kitabu cha injili ya Barnaba ni kipi?

Lini wanafunzi wa Yesu walipatwa wivu kwa ajili ya maria magdalena? Ilikuwa wapi ambapo waliambatana naye?

Acha Uongo na Uzushi mkuu, havikusaidii.
 
Mkuu acha kuifunga akili yako kwa kigezo cha imani.
Kwanini unafikiri anaifunga akili yake..?
Biblia ina vitabu 66
huu ni uongo mwingine...Biblia halisi inavitabu 72/73
wakati kuna vitabu vingi sana vimeondolewa
unaweza ukatupa sababu ya kwanini vitabu hivyo vikaondolewa...? Unafahamu lengo la kuja kwa Yesu ulimwenguni...?
mpaka kubaki idadi hiyo aliyeviondoa si Mungu bali ni binadamu kwa matakwa yake.
sio kuondoa tu...pia aliyeandika vitabu hivyo ni binadamu pia...Hata hivyo ambavyo havikuondolewa pia viliandikwa na binadamu pia

Moja kati ya vitabu vilivyoondolewa ni kitabu cha "gospel of peter" na "gospel of Marry magdalen"
Ndio maana nikakuuliza unajua lengo la Yesu kuja duniani...??
Vitabu hivi sio tu vinaonesha ukaribu wa Yesu na Marry bali vinaelezea maisha ya yesu akiwa kawa binadamu wa kawaida tena kijana wa kiyahudi.
Sio akiwa kijana hata akiwa mtoto maisha yake watu walipata kuyaandika..."gospel of Nativity"... Unafikiri sisi Wakristo tunaotaka wokovu tuliitaji kujua utoto wa Yesu au Ujana wake..? Ili iweje...Yesu alianza kazi aliyotumwa na Baba yake akiwa na miaka 33... Sisi tuna-focus na kazi zake...Mambo ya utoto na ujana wake ni mambo ya kishabiki tuu..
Katika biblia ya kawaida
Ambayo siyo ya Kawaida ndio unaamini inaelezea ubinadamu wa Yesu..?
akuna kitabu kinachoelezea maisha ya yesu kama mwanadamu wa kawaida bali vinamuelezea katika hali ya uungu.
Yes! Kwakuwa Yesu ni Mungu...

Hii ni moja ya kazi ya mfalme constantine ya kuunganisha upagani na ukristo.
kabla huyo Constantine hajazaliwa Kanisa lilikuwepo ma Neno la Mungu lilikuwepo ..Sijui ulitaka kituambia kitu gani hapa..
Inabidi tutafte kujua kweli na si kuamini tuu kwa kutumia source moja ya biblia tena iliyochakachuliwa
umeshawahi kuona hiyo ambayo haijachakachuliwa...?
 
Hivi vitabu vya Gospel of Peter na Magdalene vinapatikana wapi aisee?

Achana na huyo...Vitabu ambavyo kanisa Katoliki wakati inakusanya na kutengeneza Biblia iliviacha kwa ujumla vinatwa Apocrypha books...Huko zipo pia Injili zaidi ya 20 ...zote hizo zilijaa ushabiki na mambo ambayo yalikuwa si lengo la kutuletea wokovu..

Sasa mf. Injili ya Nativity inaonesha jinsi Yesu alivyokuwa mdogo akiwasaidia wenzake dhidi ya watoto wakorofi....Akiwasaidia wenzake wadiadhibiwe na wazazi wao pindi wanapochelewa kurudi nyumbani....Yes ni mambo mazuri ila hayana msingi na lengo halisi la Yesu kuja duniani...?

Mengine ni uzushi tuu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…