Naomba kufundishwa mbinu za kuepuka watu wa Jumuiya na Parokia

Naomba kufundishwa mbinu za kuepuka watu wa Jumuiya na Parokia

Njia rahisi ni kuwakwepa kwepa kijanja hivyo hivyo. Ikitokea event yoyote unatengeneza excuse usijumuike nao ingawa usiache kwenda katika ibada. Mwishoe watachoka na kukupotezea. Kwetu sisi introverts ni kazi rahisi mno hiyo.
K
😂 katibu unakataa ukatibu wakati kuna watu wanajisifu hata kusoma neno pale mbele na wamewekeana zamu!, ila haka ka dunia katamu sana mi nimekapenda na nilichokipendea ni kitu kimoja waumini sio wachoyo!..😂
Wa hiyo
Mnalazamisha na ndio maana asipoenda jumuiya hata kama anahudhuria Ibada kanisani mnaanza kumpa vitisho mara ooh ukifa padiri Haji kwenye maziko Yako, mara ooh kanisa linakutenga, basi kama vipi bomoeni makanisa ili tubaki na jumuiya tu.
Wanatutisha watu badala ya Mungu mwenyewe aje kututisha huwa nashangaa sana
 
Ah ah sasa mkuu hiyo jazba,kama kiongozi wewe sekunde tu utavunja muunganiko wa jamii.

Huwezi mlazimisha mtu atoe kitu asichojisikia kutoa sadaka,kutoa ni moyo.
mfano kwenye ujenzi kila mtu anapewa goli lake kutokana na tunavyomwona katika jamii na alivyobarikiwa huyu muumini aache kukwepa wakati huku anahitaji huduma za sakrameti za kanisa
 
Ukitaka watu wakuvue jukumu wewe waangushe tu. Yaani unapotakiwa kutokea usitokee, unapotakiwa kufaya usifanye. Mwezi 1 tu uko huru.

Hii ni plan B nimekupa maana wewe plan A ya kuwa tu muwazi nimegundua huiwezi
 
Hata Ushoga ulianza na hoja kama hizi hizi, mwishowe unaanza kuenea kwa Kasi. Hili nalo ni eneo lingine la wanaompinga Mungu linavyoanza.

Hamia Freemason, wanamuabudu Shetani na pesa za kula Bata wanapata.
We kenge Mungu unayemuabudu amekufanyia nini ambacho unaweza ukajitokeza hadharani kujidai kuwa alikupa yeye kwa ushahidi.Kuna watu kibao wanamuabudu Mungu na wanatoa hadi hela zao za kibindoni na bado wanagongwa njaa na dhiki kama kawaida.
Africa tuna akili nyeusi kama ngozi za ..... yaani tumeletewa Dini zao tumezishupalia kuliko hata dini zetu maana tulikuwa na Miungu yetu ambayo ni culture yetu(mizimu) tukaaminishwa mizimu ni ushirikina tukaachana nayo ama kweli ukiwa huna akili unaweza ukatupa dhahabu na ukaokota jiwe
 
We kenge unaemuabudu Mungu amelufanyia nini ambacho unaweza ukajitokeza kujidai kuwa alikupa Mungu.Kuna watu kibao wanamuabudu Mungu na wanatoa hadi hela zao za kibindoni na wagongwa njaa kama kawaida.
Africa tuna akili nyeusi kama ngozi za ..... yaani tumeletewa Dini tumezishupalia kuliko hata aliezitengeneza tukaacha Miungu yetu ambyo ni culture yetu tukaaminishwa ni uahirikina ama kweli ukiwa huna akili unaweza ukatupa dhahabu na ukaokota jiwe
Mungu amekuumba, unavuta pumzi bure. mshukuru kwa hayo
ila hizi mbilingembilinge za kutotaka kujumuika na wenzio isikufanye ukamkosea Mungu
 
Ni swala la maamuzi tu, mimi tangu 2000, sijui mlango wa kanisa au msikiti, niligundua ni miradi ya wajanja. Jiulize ni Mungu gani anaetoa kafara kama binadamu? Mungu mwenye uwezo wote hawezi akafanya hivyo,basi sio Mungu wa kweli. Mimi nafuata jadi yangu, hata nikifa nizikwe kijadi. Abaki kuwa Mungu wa Waisraeli, sisi tutafute wetu wa Kiafrika.
 
Mnalazamisha na ndio maana asipoenda jumuiya hata kama anahudhuria Ibada kanisani mnaanza kumpa vitisho mara ooh ukifa padiri Haji kwenye maziko Yako, mara ooh kanisa linakutenga, basi kama vipi bomoeni makanisa ili tubaki na jumuiya tu.
Kama unataka huduma zao mf. maziko, shart ujumuike nao vinginevyo wewe ndo mzinguaji.
Btw uzikwe ama usizikwe na padre, ni umekufa tu.
 
Mimi ni Mkristu dhehebu la RC na nililelewa kwenye familia yenye kufuata mafundisho ya RC na nimebatizwa,kupata komunyo ya kwanza hadi kipaimara na kufunga ndoa ya kikatoliki.

Lililonileta ni kuwa nimekuwa sipendezwi na imani yoyote haswa hizi za dini naona kama uongo na ni mifumo ya watu fulani hapa namanisha Ukristu na madhehebu yake yote naona kama udwanzi na uislam ndo kabisa siulewagi kabisa kwa kifupi siamini kama Mungu yupo(nina ground zangu) na kama yupo hatambui hii mifumo iliyowekwa na makundi ya binadamu(dini) na hana uwezo huo anaosifiwa na dini zote zilizoanzishwa.

Nimegundua kwenye kuifuata dini tunapoteza muda tu na hela mfano mimi huu mwaka wa 5 anaenda kanisani ni wife tu ila hajawahi leta chochote kutoka KANISANI zaidi ya sisi kupeleka vitu kibao include hela zetu(sadaka,zaka na michango mingine) na mavuno zaidi zaidi kuna matawi ya muwese la enzi za kuanza kwa mfungo wa kwa resma na bado hayo matawi alienda nayo yeye likabalikiwa akalileta home pamoja na maji ya baraka.

Changamoto niliyonayo ni kuwa wife kajiunga kwenye jumuia alafu huwa anawapa namba yangu viongozi wa jumuia na nimezinguana nae sana kwa hilo swala kiasi kwamba wananisumbua kwa kuniletea ma bahasha mengi ambayo hata nikitoa siamini kama lolote naongezewa zaidi zaidi naona kama napungukiwa kwa sababu natoa kitu live alafu narudishiwa ahadi ya kubarikiwa ambapo siwezi pima hizo baraka kama zinahusiana na kusali au kutoa kwangu.

OMBI LANGU
Nisaidien mbinu za kukwepa ushiriki wa hizi habari za kusali jumuia au kanisani maana nahisi wameona kuna magari matatu yard kwangu ndio maana wananisakama na ndio maana nikiweka hela ndogo kwenye bahasha wanapanic kuwa "huyu sio wa kuchangia elf 20". Kuna siku walifanya uchaguzi wakanichagua kuwa Mhasibu/Mweka hazina wa parokia na huku kwenye jumuia wakanichagua kuwa katibu wa jumuia nilishangazwa na uchaguzi wao wa kushinda bila kushiriki ikabidi nikatae kwa kisingizio cha muda wangu hautoshi kutokana na nature ya kazi yangu na wakataka kulazimisha sana ila walishindwa.

In short najiuliza nawezaje kuwatoka kistaarabu na wakatambua kuwa mimi sihitaji kuwa mshiriki wa hizi imani maana imani yangu mimi nikufight na maisha na kuinjoy matokeo kwa kuwekeza nguvu na akili chache nilizonazo.Naomba ushauri ili kuepuka kuwakwaza majirani na watu tunaoheshimiana nao wasije ona nimejaa kiburi kumbe mimi nimeona kuwa nawekeza effort za kufungua mlango uliochorwa ukutani.

Jamii kushiri nayo kwenye mambo mengine nahitaji ila sio haya mambo ya kusali pamoja nipo tayari kama kuna umoja wa kuchangiana au kuwa na kikundi cha kusaidiana kwenye raha na shida ila sio hivi vikundi vya dini vikekaa kinyonyaji sana yaani wanatupa hewa(maombi) sisi tunawapa vitu tangible n valuable.
SUBIRI UFE UTAWAELEWA KAA HIVYOHIVYO USIENDE
 
mfano kwenye ujenzi kila mtu anapewa goli lake kutokana na tunavyomwona katika jamii na alivyobarikiwa huyu muumini aache kukwepa wakati huku anahitaji huduma za sakrameti za kanisa
Mnamuangalia ninyi kama nani?nyie ni Mungu?je kama ameiba au kapata mafanikio kiuganga na hataki amshirikishe Mungu wake?

Na dizain yenu ndiyo mkienda kwa mwenzenu kusali badala mfanye kilichowapeleka huwa mnaishia kumchunguza baadae asipotoa mchango wowote mnamuona hana akili,kutoa ni moyo hata akitoa mill 100 kila mwaka kama hakuzitoa kwa mapenzi yake huko ni kumnyang'anya na hakumjengi kiimani
 
Nisaidien mbinu za kukwepa ushiriki wa hizi habari za kusali jumuia
Subiria Jumuiya ifike kwako alafu HIO siku waambie wewe umejitoa sababu wape hizo hizo ulizo Andika watakuacha na kukuondoa km mwanajumuiya na hawatokusumbua tena, kuna Mzee aliwahi kufanya hivyo yeye sababu aliyoitoa ni masadaka mengi na yeye hana Pesa za kutoatoa ovyo kwa hio anaomba wamuondoe kwenye orodha ya wanajumuiya na kuanzia siku hatosali tena Jumuiya na ikawa HIVYO huu unaenda Mwaka wa 15 Mzee hajawahi kusumbuliwa na Jumuiya
 
Back
Top Bottom