Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi ni Mkristu dhehebu la RC na nililelewa kwenye familia yenye kufuata mafundisho ya RC na nimebatizwa,kupata komunyo ya kwanza hadi kipaimara na kufunga ndoa ya kikatoliki.
Lililonileta ni kuwa nimekuwa sipendezwi na imani yoyote haswa hizi za dini naona kama uongo na ni mifumo ya watu fulani hapa namanisha Ukristu na madhehebu yake yote naona kama udwanzi na uislam ndo kabisa siulewagi kabisa kwa kifupi siamini kama Mungu yupo(nina ground zangu) na kama yupo hatambui hii mifumo iliyowekwa na makundi ya binadamu(dini) na hana uwezo huo anaosifiwa na dini zote zilizoanzishwa.
Nimegundua kwenye kuifuata dini tunapoteza muda tu na hela mfano mimi huu mwaka wa 5 anaenda kanisani ni wife tu ila hajawahi leta chochote kutoka KANISANI zaidi ya sisi kupeleka vitu kibao include hela zetu(sadaka,zaka na michango mingine) na mavuno zaidi zaidi kuna matawi ya muwese la enzi za kuanza kwa mfungo wa kwa resma na bado hayo matawi alienda nayo yeye likabalikiwa akalileta home pamoja na maji ya baraka.
Changamoto niliyonayo ni kuwa wife kajiunga kwenye jumuia alafu huwa anawapa namba yangu viongozi wa jumuia na nimezinguana nae sana kwa hilo swala kiasi kwamba wananisumbua kwa kuniletea ma bahasha mengi ambayo hata nikitoa siamini kama lolote naongezewa zaidi zaidi naona kama napungukiwa kwa sababu natoa kitu live alafu narudishiwa ahadi ya kubarikiwa ambapo siwezi pima hizo baraka kama zinahusiana na kusali au kutoa kwangu.
OMBI LANGU
Nisaidien mbinu za kukwepa ushiriki wa hizi habari za kusali jumuia au kanisani maana nahisi wameona kuna magari matatu yard kwangu ndio maana wananisakama na ndio maana nikiweka hela ndogo kwenye bahasha wanapanic kuwa "huyu sio wa kuchangia elf 20". Kuna siku walifanya uchaguzi wakanichagua kuwa Mhasibu/Mweka hazina wa parokia na huku kwenye jumuia wakanichagua kuwa katibu wa jumuia nilishangazwa na uchaguzi wao wa kushinda bila kushiriki ikabidi nikatae kwa kisingizio cha muda wangu hautoshi kutokana na nature ya kazi yangu na wakataka kulazimisha sana ila walishindwa.
In short najiuliza nawezaje kuwatoka kistaarabu na wakatambua kuwa mimi sihitaji kuwa mshiriki wa hizi imani maana imani yangu mimi nikufight na maisha na kuinjoy matokeo kwa kuwekeza nguvu na akili chache nilizonazo.Naomba ushauri ili kuepuka kuwakwaza majirani na watu tunaoheshimiana nao wasije ona nimejaa kiburi kumbe mimi nimeona kuwa nawekeza effort za kufungua mlango uliochorwa ukutani.
Jamii kushiri nayo kwenye mambo mengine nahitaji ila sio haya mambo ya kusali pamoja nipo tayari kama kuna umoja wa kuchangiana au kuwa na kikundi cha kusaidiana kwenye raha na shida ila sio hivi vikundi vya dini vikekaa kinyonyaji sana yaani wanatupa hewa(maombi) sisi tunawapa vitu tangible n valuable.
Acha wenge mzee wewe ukifa popote unazikwa bila kujali wewe ni Mkatoliki sijui mlokole Buddhist etc hakuna wa kuiuliza maiti yako ulikuwa dini gani.Nisipo zikwa nawanukia watanifukia na hapo watakuwa wamenizika
Nao wameiga siku hizi wanaboa tena Lutheran huwa makanisa yao hayaishi kwa sababu wachungaji wansomesha watoto wao nje ya nchi na pia kuna muda huwa wanagombana kwa sababu ya sadaka za wauminiILa wanachoshaga RC kweli wanachosha hadi unataka uhamie dhehebu jingine njoo lutheran utatoa mochango ila ukishatoka church ufuatwi fuatwi
Una busara sana aiseePole Mkuu, kikubwa hapo ni umepoteza Imani, hata sadaka unazotoa pia unatoa bila Imani ndio maana inakusumbua, na unahisi kama unawapa viongozi wa kanisa badala ya kumtolea Mungu.
Ndugu yangu, Mungu yupo, na anakupenda, ila amekupa wewe kuchagua kumuamini au kutoamini, Uzima au Mauti. Japo utaratibu wetu wa kumtafuta unaweza kuwa kikwazo kwako kulingana na mapokeo ya viongozi wa kanisa lako, uwe tu na ujasiri wa kuwaambia kwamba hauamini sawasawa na wao, kwahiyo wakuache, nafikiri wana kuzingatia maana wanajua mko pamoja.
Yes mkuu na jiran alikuwa rc akachana na jumuiya alipokufa waliwauliza viongozi wa jumuiya akajibiwa alijitoa padre akagoma tukaenda kutaftaa mlokole akameza 50000 yake akasalisha tukazikaKuna maiti ambayo hawakuizika kwa sababu kama zangu?
Mi sitaki hata kuombewa au kuzikwa na kiongozi yoyote wa dini mi hata nikiumwa mahututi sitaki nipelekwe kwenye maombezi wala kwa waganga nataka nipelekwe hospitalini tu ikishindikana biashara inikate huko huko.Yes mkuu na jiran alikuwa rc akachana na jumuiya alipokufa waliwauliza viongozi wa jumuiya akajibiwa alijitoa padre akagoma tukaenda kutaftaa mlokole akameza 50000 yake akasalisha tutukazika
Kuzikwa utazikwa tu ibada noMi sitaki hata kuombewa au kuzikwa na kiongozi yoyote wa dini mi hata nikiumwa mahututi sitaki nipelekwe kwenye maombezi wala kwa waganga nataka nipelekwe hospitalini tu ikishindikana biashara inikate huko huko.