Naomba kufundishwa mbinu za kuepuka watu wa Jumuiya na Parokia

Naomba kufundishwa mbinu za kuepuka watu wa Jumuiya na Parokia

Wabongo wape kichwa cha habari. Stori watatengeneza wenyewe.

Binafsi nilisikia mengi sana kuhusu wasabato. Ila siku niliyoenda kusali kwao. Nikajua kwamba niliyoyasikia nje mengi sio ya kweli. Ni chumvi tu za watu.

Mfano wewe mtu mzima kabisa akili yako inaamini SDA huwa hawapiki jumamosi wala kuosha vyombo ?
Ni kweli, mimi niliishi Bunda na SDA, wakishapika chakula cha jioini, jiko linanuna mpaka jioini ya j.mosi.
Watoto wanakula vipolo visivyochemshwa. Amini amini nakwambia, sabato wanakula viporo.
 
Kuna siku nilienda home wazee wamepata gawio Kila muumini 300K wako wawili jumla 600k kuna mradi wa ujenzi niliwasikitikia Sana jinsi wananyonywa nikawaeleza hawaelewi wanasema Sisi tutatoa Tu wakila shauri Yao
Kuanzia siku hiyo sitoi tena cash nyumbani
Aisee! Hizi dini ni Chuma ulete. Wanamanipulate wazee wa watu bila huruma. Kitendo cha mwanadamu kupenda kujumuika na kuabudu isiwe sababu ya kumtumikisha na kumnyonya.
 
Hata Ushoga ulianza na hoja kama hizi hizi, mwishowe unaanza kuenea kwa Kasi. Hili nalo ni eneo lingine la wanaompinga Mungu linavyoanza.

Hamia Freemason, wanamuabudu Shetani na pesa za kula Bata wanapata.
Usiweke kigezo cha ushoga wako kuwalazimisha watu kitu kilicholetwa na wahuni ili wapige hela,wewe freemason huwajui hata ukiomba ushahidi utaanza kujinyea tu
 
jitahidi kila wakija wakukute umelewa halafu umejinyea na unataka kuwasalimia kwa kuwakumbatia hawata rudi kwako milele na mile amina
 
Mimi ni Mkristu dhehebu la RC na nililelewa kwenye familia yenye kufuata mafundisho ya RC na nimebatizwa,kupata komunyo ya kwanza hadi kipaimara na kufunga ndoa ya kikatoliki.

Lililonileta ni kuwa nimekuwa sipendezwi na imani yoyote haswa hizi za dini naona kama uongo na ni mifumo ya watu fulani hapa namanisha Ukristu na madhehebu yake yote naona kama udwanzi na uislam ndo kabisa siulewagi kabisa kwa kifupi siamini kama Mungu yupo(nina ground zangu) na kama yupo hatambui hii mifumo iliyowekwa na makundi ya binadamu(dini) na hana uwezo huo anaosifiwa na dini zote zilizoanzishwa.

Nimegundua kwenye kuifuata dini tunapoteza muda tu na hela mfano mimi huu mwaka wa 5 anaenda kanisani ni wife tu ila hajawahi leta chochote kutoka KANISANI zaidi ya sisi kupeleka vitu kibao include hela zetu(sadaka,zaka na michango mingine) na mavuno zaidi zaidi kuna matawi ya muwese la enzi za kuanza kwa mfungo wa kwa resma na bado hayo matawi alienda nayo yeye likabalikiwa akalileta home pamoja na maji ya baraka.

Changamoto niliyonayo ni kuwa wife kajiunga kwenye jumuia alafu huwa anawapa namba yangu viongozi wa jumuia na nimezinguana nae sana kwa hilo swala kiasi kwamba wananisumbua kwa kuniletea ma bahasha mengi ambayo hata nikitoa siamini kama lolote naongezewa zaidi zaidi naona kama napungukiwa kwa sababu natoa kitu live alafu narudishiwa ahadi ya kubarikiwa ambapo siwezi pima hizo baraka kama zinahusiana na kusali au kutoa kwangu.

OMBI LANGU
Nisaidien mbinu za kukwepa ushiriki wa hizi habari za kusali jumuia au kanisani maana nahisi wameona kuna magari matatu yard kwangu ndio maana wananisakama na ndio maana nikiweka hela ndogo kwenye bahasha wanapanic kuwa "huyu sio wa kuchangia elf 20". Kuna siku walifanya uchaguzi wakanichagua kuwa Mhasibu/Mweka hazina wa parokia na huku kwenye jumuia wakanichagua kuwa katibu wa jumuia nilishangazwa na uchaguzi wao wa kushinda bila kushiriki ikabidi nikatae kwa kisingizio cha muda wangu hautoshi kutokana na nature ya kazi yangu na wakataka kulazimisha sana ila walishindwa.

In short najiuliza nawezaje kuwatoka kistaarabu na wakatambua kuwa mimi sihitaji kuwa mshiriki wa hizi imani maana imani yangu mimi nikufight na maisha na kuinjoy matokeo kwa kuwekeza nguvu na akili chache nilizonazo.Naomba ushauri ili kuepuka kuwakwaza majirani na watu tunaoheshimiana nao wasije ona nimejaa kiburi kumbe mimi nimeona kuwa nawekeza effort za kufungua mlango uliochorwa ukutani.

Jamii kushiriki nayo kwenye mambo mengine nahitaji ila sio haya mambo ya kusali pamoja nipo tayari kama kuna umoja wa kuchangiana au kuwa na kikundi cha kusaidiana kwenye raha na shida ila sio hivi vikundi vya dini vikekaa kinyonyaji sana yaani wanatupa hewa(maombi) sisi tunawapa vitu tangible n valuable.
Ukituliza sana akili utagundua dini nyingi hasa ukristo ni utumwa na wapo wwny maslahi zao hmo hizi dini nimezichoka
 
Kiufupi HUNA IMANI TENA na mambo ya Mungu!! Sasa umebaki na hofu kwa jamii inayokuzunguka !!

Ni jambo jema !! Vp mahusiano yako na mkeo ? Maana yy nadhani angekuwa ni mjumbe mzuri kwa kufikisha taarifa zako kwa kiongozi wa JUMUIYA . Kuwa ww sasa si MUUMINI tena wa kanisa KATOLIKI .

Mwenyekiti wa Jumuiya atakuja kwako kupata uthibitisho na taarifa zako zitafikishwa kwa PAROKO , hutaona tena hizo unazoziita KERO.

JUMUIYA itasali nyumbani kwako kwa maana ya kufuata familia yako kama wao watabaki kuwa WAKATOLIKI , wala hutaona ukifatwa kubembelezwa ubadili uamuzi wako.


Na ikifika wakati ww mwenyewe ukitaka kurudia IMANI yako, utaandikisha mafundisho kwa muda wa miezi 6 kisha utarudi kuwa Mkatoliki.
 
Kiufupi HUNA IMANI TENA na mambo ya Mungu!! Sasa umebaki na hofu kwa jamii inayokuzunguka !!

Ni jambo jema !! Vp mahusiano yako na mkeo ? Maana yy nadhani angekuwa ni mjumbe mzuri kwa kufikisha taarifa zako kwa kiongozi wa JUMUIYA . Kuwa ww sasa si MUUMINI tena wa kanisa KATOLIKI .

Mwenyekiti wa Jumuiya atakuja kwako kupata uthibitisho na taarifa zako zitafikishwa kwa PAROKO , hutaona tena hizo unazoziita KERO.

JUMUIYA itasali nyumbani kwako kwa maana ya kufuata familia yako kama wao watabaki kuwa WAKATOLIKI , wala hutaona ukifatwa kubembelezwa ubadili uamuzi wako.


Na ikifika wakati ww mwenyewe ukitaka kurudia IMANI yako, utaandikisha mafundisho kwa muda wa miezi 6 kisha utarudi kuwa Mkatoliki.
Nirudi kufanya nini ?
 
Mnalazamisha na ndio maana asipoenda jumuiya hata kama anahudhuria Ibada kanisani mnaanza kumpa vitisho mara ooh ukifa padiri Haji kwenye maziko Yako, mara ooh kanisa linakutenga, basi kama vipi bomoeni makanisa ili tubaki na jumuiya tu.
Tunatishana sana! Tukifa Miili yetu ni Mizoga kama Mizoga mingine! Ata usomewe Misa million moja kama wa motoni ni Motoni tu azisaidii kitu- Thus why Thugs always Says this"ONLY GOD WILL JUDGE ME"Kikubwa kuwa karibu na Mungu wako hili Roho yako isiangamie
 
Mnalazamisha na ndio maana asipoenda jumuiya hata kama anahudhuria Ibada kanisani mnaanza kumpa vitisho mara ooh ukifa padiri Haji kwenye maziko Yako, mara ooh kanisa linakutenga, basi kama vipi bomoeni makanisa ili tubaki na jumuiya tu.
Huwa sielewi mantiki yao ya kugoma kuendesha ibaada ya mazishi, ni ujinga usio na maana kabisa.
 
Jifanye unasali dhehebu lingine. Wajue haujakimbia ukristo ila unasali dhehebu la baba yako. Mfano mimi mambo ya jumuiya yalinikera nikaamua kusali SDA sababu hawana hizo jumuiya.

Nikaja kugundua ukiondoa kusali jumamosi SDA taratibu zao tamu sana kwa mtu asiye na mambo mengi
Kwa kweli SDA usumbufu hakuna na michango hakuna kulazimishana, uwe tajiri uwe maskini utachangia kulingana na kubarikiwa kwako.
 
Back
Top Bottom