Naomba kujua bei ya jumla ya nondo sasa hivi maana sisi tunaoishi mbali mafundi wanatupiga sana

Naomba kujua bei ya jumla ya nondo sasa hivi maana sisi tunaoishi mbali mafundi wanatupiga sana

Mbongo4life

Senior Member
Joined
Nov 1, 2021
Posts
132
Reaction score
270
Waungwana naomba kujua bei ya jumla ya nondo sasa hivi maana sisi tunaoishi mbali mafundi wanatupiga sana. Natanguliza shukrani.

Ndugu zangu naomba msaada wa kujua bei za jumla za nondo Dar
 
Mwezi uliopita nimenunua 2.6M per tonne BS na 2.4M per tonne Local. Hizi ni bei za Arusha pale Bulk. Kwa dsm itakuwa chini kidogo.
 
Huwa zinaandikwa mkuu, strength yake huwa ni 500 wakati za local huwa ni 300 au 350. Hata bei tu zinautofauti karibu robo ya bei.
mmmh hapa tupate elimu kidogo aseeee huenda huku tunapigwa na local kwa bei ya bs
 
BS nyingi zinatoka nje. Ingawa vipo viwanda vya ndani vinazalisha BS. Mfano Kamal pale bagamoyo na aim steel pale Mbezi beach.
Shukran sana mkuu kwa jibu je nondo hizi ni nzuri (zina ubora) kwa ujenzi wa nyumba ghorofa moja au ni vizuri tu kutumia nondo za nje ya nchi?
 
Shukran sana mkuu kwa jibu je nondo hizi ni nzuri (zina ubora) kwa ujenzi wa nyumba ghorofa moja au ni vizuri tu kutumia nondo za nje ya nchi?
Nyumba ya ghorofa moja inategemea ni eneo lipi. Hata hivyo kama unafuatisha mchoro wa structural local zinatosha.
 
Waungwana naomba kujua bei ya jumla ya nondo sasa hivi maana sisi tunaoishi mbali mafundi wanatupiga sana. Natanguliza shukrani.

Ndugu zangu naomba msaada wa kujua bei za jumla za nondo Dar
Ukishasema nondo tu tayari inakua imeeleweka kinachohitajika?
Nondo hazina grades wala vipimo tofauti?
 
Ukishasema nindo tu tayari inakua imeeleweka kinachohitajika?
Nondo hazina grades wala vipimo tofauti?
Nadhani huwa zinauzwa kama misumari, bei ya misumari kwa Kg ni tsh 4000 haijalishi ni misumari ya nchi ngapi. Ukinunua kg 1 ya misumari ya nchi 3 utapata misumari mingi tofauti na ukinunua Kg 1 ya misumari ya nchi 4 lakini uzito ni ule ule

Ukinunua tani moja ya nondo za 12mm unapata 94pcs lakini ukinunua tani moja ya nondo za 16mm unapata 53pcs
 
Shukran sana mkuu kwa jibu je nondo hizi ni nzuri (zina ubora) kwa ujenzi wa nyumba ghorofa moja au ni vizuri tu kutumia nondo za nje ya nchi?
kwa kuelewa zaidi roughly nyumba ya ghorofa moja ya kawaida inaweza tumia tone ngapi za nondo kwa makisio!
 
kwa kuelewa zaidi roughly nyumba ya ghorofa moja ya kawaida inaweza tumia tone ngapi za nondo kwa makisio!
Itategemea sasa na ramani yenyewe jinsi ilivyo, lazima uwe na michoro ya nondo ili mtaalam akuandalie bar bending schedule (hii ni document ambayo inaonesha mikunjo ya nondo,idadi, urefu n.k) kiujumla hiyo ndio itamuongoza mfunga chuma (steel fixer) kufanya kazi kwa usahihi na kwa uharaka zaidi
 
Back
Top Bottom